- Chagua mmoja tu kati ya Ødegaard au Zubimendi
- Tumia Eze au mchezaji wa aina hiyo ili kuleta nguvu na uimara
Kwa kweli, kwa takribani mechi tano sasa, viwango vya uchezaji wa Arsenal vimekuwa vya kutia wasiwasi, hasa katika ubunifu na kasi ya mashambulizi.
Tatizo la Ødegaard + Zubimendi
kusema kwamba wote wawili wanacheza maeneo yanayofanana wakiwa na mpira. Wote wanapenda kupokea mpira upande wa kulia wa nusu-uwanja (right half-space), wanataka kudhibiti tempo, lakini hakuna anayefanya mbio za marudio (second-phase runs). Matokeo yake ni:
- Msongamano wa wachezaji katikati ya uwanja
- Mzunguko wa mpira kuwa wa polepole sana
- Ujenzi wa mashambulizi unaotabirika na adui
Zubimendi, ni imara zaidi kiulinzi:
- Anashinda mapambano ya mwili, ana nguvu sana, kumbuka goli lake kule UEFA
- Ana nidhamu nzuri ya nafasi yake uwanjani
- Yuko tayari kubaki kwenye nafasi yake, badala ya kuzurura ovyo uwanjani
Ødegaard, kwa upande mwingine, anashuka chini kupokea mpira kwa sababu hakuna presha, jambo linalomtoa kwenye maeneo hatari na:
- Linakatisha muunganiko na safu ya mbele
- Linamuacha Saka afanye kazi peke yake
- Linapunguza ubunifu wake karibu na lango
Awamu ya ulinzi ya Ødegaard
Hili ni kosa halali kabisa kulizungumzia. Presha yake mara nyingi ni ya kuonekana tu, si ya kushinda mpira. anapanda juu ili kuzuia njia za pasi, lakini haingii kwenye mapambano ya ana kwa ana. Hilo linaweza kufanya kazi kama timu iko imara, lakini mfumo unapovunjika, inaonekana kama anajiondoa kwenye mapambano.
Ukilinganisha na Eze:
- Anapresha kwa nia nzuri na tija, pia yuko tayari kujaribu kufunga nje ya mfumo wa ‘MAGOLI YA KIMAPENZI’
- Anacheza kwa nguvu na yuko tayari kwa mapambano
- Analazimisha mabeki kufanya maamuzi ya haraka
“Kurudi kwenye kilichofanya kazi”
Hapa ndipo kwenye tatizo:.
Mfumo wa Eze kama namba 10 ulifanya kazi kwa sababu:
- Alikaa juu zaidi kwenye ushambuliaji
- Alishambulia nafasi, si tu uwanja mzima
- Aliruhusu Arsenal kucheza kwa kitimu zaidi
Dhidi ya Bayern, Newcastle na Spurs, Arsenal ilikuwa:
- Alikuwa hatari na maamuzi ya haraka katika mashambulizi
- Anakuwa sehemu ya mbinu za mabadiliko ya mashambulizi
- Ngumu zaidi kusomwa na adai hatua au anataka kufanya nini
Tangu Ødegaard arudi kuwa mhimili wa eneo hilo:
- Umiliki umekuwa tasa
- Mipira ya pembeni imeongezeka
- Ubora wa nafasi za kufunga umeshuka
Tatizo la kweli (na hili ni kwa Arteta)
Suala si Ødegaard kuwepo kwenye timu ya kwanza. Tatizo ni kwamba Arteta hamuwekei mipaka ya kiufundi.
Ikiwa Ødegaard anacheza:
- Lazima akae juu zaidi ya ukanda wa mashambulizi
- Lazima ashambulie lango mara kwa mara
- Lazima awajibike kimwili bila kujificha kwenye rundo la wachezaji wenzake
Vinginevyo:
- Chagua mmoja tu kati ya Ødegaard au Zubimendi
- Tumia Eze au mchezaji wa aina hiyo ili kuleta nguvu na wima
Kwa sasa, Arsenal inaonekana timu inayojaribu kucheza vizuri, na si kushinda. Na hilo ndilo tatizo kubwa.Timu nyingine zinacheza ovyo na kushinda kwa uwiano wa magoli mengi.

