in , , , ,

FIFA yakunjua makucha dhidi ya ubaguzi


Timu zinazouendekeza zinaweza kushushwa daraja

Kampeni dhidi ya ubaguzi wa rangi kwenye soka imeshika kasi, ambapo Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limetoa onyo kwamba timu zitakazohusishwa nao zinaweza kupata adhabu kali, ikiwamo kushushwa daraja.
Hatua hizo zinakuja wakati vitendo vya ubaguzi vikikithiri katika siku za karibuni, na viongozi wa Fifa walipiga kura kupitisha hatua mpya na kali, ambapo timu zinaweza pia kuondoshwa kabisa kwenye mashindano zinayishiriki.
Makosa madogo ya kwanza yatasababisha timu kupokea maonyo, kutozwa faini au kuamriwa mechi yao ichezwe bila watazamaji. Kadiri makosa yatakavyorudiwa au makubwa zaidi kufanywa, adhabu zitaongezeka, kuanzia kupokonywa pointi, kuondoshwa kwenye mashindano au kushushwa daraja.
Mkuu wa Kamati Maalumu ya Fifa Dhidi ya Ubaguzi wa Rangi, Jeffrey Webb, anasema uamuzi huo ni mwafaka, kwa sababu soka ni kama familia, na wale wote wanaoendekeza vitendo vichafu vya kuivuruga familia hawatakiwi kuvumiliwa.
“Familia yetu ya soka inatambua kwamba kinachoripotiwa kwenye vyombo vya habari ni pungufu ya asilimia moja ya matukio ya kibaguzi yanayotokea kote duniani. Tunatakiwa kuchukua hatua sasa, ili kujiweka vyema kwa miaka 20 au 50 ijayo, kuwe hakuna kitu kama ubaguzi kabisa,” akasema Webb.
Kamati ya Utendaji ya Fifa ilipitisha azimio dhidi ya ubaguzi wa rangi kwa asilimia 99 ya kura, katika mkutano wake nchini Mauritius.
Baadhi ya adhabu kubwa zilizopata kutolewa ni pamoja na ile ya £65,000 dhidi ya Chama cha Soka cha Serbia, kutokana na matukio ya kibaguzi yaliyohusisha timu yake ya vijana chini ya umri wa miaka 21 na ile ya England Oktoba mwaka jana.
Baadhi ya viongozi wa Fifa walionesha kutofurahishwa na washiriki wa kikao waliopiga kura kupinga adhabu kali dhidi ya wabaguzi, ambapo mjumbe kutoka Afrika Kusini aliyepata kutupwa jela enzi za ubaguzi wa rangi, Tokyo Sexwale alitaka kamera zitumiwe kubaini waliokataa azimio hilo.
Nchini Uingereza, ubaguzi michezoni ulitikisa hivi karibuni, baada ya aliyekuwa nahodha wa England, John Terry kutiwa hatiani kwa kumkashifu kibaguzi beki wa Queen Park Rangers, Anton Ferdinand. Terry ni nahodha wa Chelsea. Alivuliwa unahodha wa Engand, akajibu kwa kujiuzulu kuchezea timu hiyo. Alipigwa faini na kuzuiwa kucheza mechi nne.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

BALOZI BISWARO AWAPA CHANGAMOTO STARS

TAIFA STARS, SUDAN ZATOKA SULUHU