in , ,

Fergie alitaka mshahara wa Rooney

*Warithi Mourinho, Ancelotti, Guardiola, Gaal, Klop

*Awahusudu sana Cantona, Giggs, Scholes, Ronaldo

 

 

Kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amebainisha kwamba ilifika mahali akawadai waajiri wake wamwongezee mshahara mara mbili ili ulingane na wa mshambuliaji wa kati, Wayne Rooney.

Hali hiyo ilitokea baada ya Rooney kutishia kuondoka United, ambapo aliongezewa mkataba na kupewa ofa ya pauni 250,000 kwa wiki, ambapo Fergie anaeleza mambo kadhaa kwenye kitabu alichochapisha.

“Niliwaambia sidhani kuwa ni sawa Rooney apate mshahara mara mbili zaidi yangu. Joel Glazer (Mwenyekiti Mwenza wa United) alisema; ‘nakubali kabisa, lakini tufanyeje?’ Ilikuwa rahisi. Tulikubaliana tu kwamba hakuna mchezaji anayetakiwa kulipwa zaidi yangu,” anasema kocha huyo aliyekaa Manchester United kwa miaka 26.

Mskochi huyo anaeleza kwenye kitabu hicho juu ya masuala ya ukocha anaeleza alivyojikuta kwenye wakati mgumu katika kipindi cha mpito tangu alipong’atuka na kumwachia David Moyes. Mskochi mwenzake huyo alikuja kufukuzwa kabla hajafikisha mwaka, Ryan Giggs akakaimu kabla ya kupatikana kocha wa sasa, Louis van Gaal.

Fergie, 73, aliyetwaa ubingwa wa Ulaya mara mbili, ubingwa wa England mara 13, makombe matano ya FA na manne ya ligi, anasema kwamba bado anaamini kuwa Moyes alikuwa mtu sahihi wa kumrithi, baada ya kushindwa kuwashawishi makocha wengine kadhaa.

Anasema lengo lake lilikuwa kumwachia kocha wa zamani wa Barcelona, Pep Guardiola aliyehamia Bayern Munich. Anataja makocha wengine ambao wangeweza kuchukua nafasi yake kuwa ni wa Chelsea, Jose Mourinho, yule wa zamani wa Real Madrid boss Carlo Ancelotti, aliyekuwa bosi wa Borussia Dortmund, Jurgen Klopp na Van Gaal.

advertisement
Advertisement

“Nilimpenda sana Pep. Nilikuwa nimemwambia anipigie simu kabla ya kupokea ofa kutoka klabu yoyote ile, lakini hakufanya hivyo, akaishia kujiunga na Bayern Munich Julai 2013. Tulipoanza mchakato wa kutafuta mrithi wangu tulibaini kwamba wale ambao tungewahitaji hawangepatikana,” anasema.

Kocha huyu mkongwe akizungumzia suala la Paul Pogba aliyemwachia kwenda Juventus, anasema alikuwa na mkataba wa miaka mitatu na uwezekano wa kuongeza mmoja, lakini wakala wake, Mino Raiola alionekana akizungumzia uwezekano wa Pogba kuhama.

“Mara wakala wake akatokea akazungumzia masuala ya kuhama na mkutano wetu wa kwanza ukawa vurugu tupu, yeye na mimi tulikuwa kama mafuta na maji,” akasema Fergie kuonesha jinsi wasivyoelewana na wakala huyo kiasi cha kuachana na Pogba ambaye sasa ni ‘lulu’.

Akimzungumzia mchezaji tata na mshambuliaji wa kati, Mario Balotelli, Fergie anasema alipata wazo la kumsajili 2010, akafanya kazi yake kwanza kisha akajadiliana na Wataliano kadhaa na mrejesho aliopata ni kwamba ingekuwa hatari kumsajili kutokana na tabia zake, akaachana na wazo hilo

Fergie anasema kwamba katika muda wote aliokaa Old Trafford, wachezaji aliowaona kuwa katika kiwango cha kimataifa hasa ni wanne; Eric Cantona, Paul Scholes, Cristiano Ronaldo na Ryan Giggs ambaye sasa ni kocha msaidizi. Anasema Giggs angeweza kuwa msaidizi wake iwapo angestaafu soka akiwa na umri wa miaka 30 na ushee, badala ya kuendelea hadi miaka 40.

Hata hivyo, anawasifu pia akina Wayne Rooney,David Beckham, Roy Keane, Carlos Tevez, Rio Ferdinand na Peter Schmeichel kwa kazi kubwa waliyofanya Old Trafford.

Akizungumzia alivyokuwa akikasirika na kubwatuka akiwa kwenye eneo lake la ufundi, Ferguson anasema wakati fulani alikuwa akipandwa na mzuka na kuwa kana kwamba anataka kuitawala dunia yote.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

SUNDERLAND AFC RETURN TO ZAMBIA

Tanzania Sports

Costa kifungoni, Paulista huru