in , ,

Feisal Salum “Fei Toto” atawasumbua Simba leo

Emmanuel Amunike hayupo Kwa sasa Tanzania, Mwinyi Zahera naye hayupo Tanzania. Hawa ni makocha ambao waliwahi kumwamini sana Feisal Salum “Fei Toto” wakati wakiwa wanafundisha mpira hapa Tanzania.

Mwinyi Zahera aliwahi kumwamini sana Feisal Salum “Fei Toto ” katika kikosi cha Yanga akiwa anacheza kama kiungo wa chini, Emmanuel Amunike naye alimwamini sana katika kikosi cha timu ya Taifa na ilifikia wakati alisema Feisal Salum “Fei Toto” anauwezo wa kuchezea Barcelona.

Baada ya makocha hawa kuondoka kiungo Feisal Salum “Fei Toto” ni kama alikuwa amesahaulika hivi katika kikosi cha Yanga baada ya kukosa nafasi hata ya kukaa benchi katika michezo ya Yanga ya hivi karibuni katika Ligi Kuu Bara na kombe la shirikisho.

Mwalimu Luc Eymael wa Yanga amekua akiwatumia Haruna Niyonzima, Balama Mapinduzi, Papy Tshishimbi na Mohammed Banka katika eneo la kiungo la Yanga na hivyo Feisal Salum kukosa kabisa nafasi katika kikosi cha kwanza Yanga.

Lakini katika mchezo uliopita wa Ligi kati ya Yanga na Alliance Feisal alipata nafasi ya kuanza na kuonyesha kua bado yumo huku akichangia kwa kiasi kikubwa ushindi wa mabao mawili wa Yanga.

JINSI ATAKAVYOKUWA NA MSAADA LEO

Kama Leo akipata nafasi kwenye kikosi cha Yanga atakuwa na nafasi kubwa ya kuisaidia timu katika maeneo yafuatayo.

1: Yanga walikuwa hawana kiungo ambaye alikuwa na uwezo wa kuchukua mipira katika eneo la nyuma na kuipeleka mbele kwa kuisukuma kwenda mbele . Feisal Salum “Fei Toto” anauwezo wa kusukuma timu kwenda mbele tofauti na namba sita wengi wa Yanga.

2: Feisal Salum “Fei Toto” anauwezo mkubwa wa kupiga pasi, hivo anaweza kuwasaidia Yanga katika eneo la umiliki wa mpira kwa kuwahakikishia usambazaji wa pasi kwenye kikosi cha Yanga.

3: Kuwapa uhuru kina Haruna Niyonzima, Papy Tshishimbi kusogea mbele zaidi kwa kuacha kushuka chini ili kuchukua mipira kwa sababu mipira itakuwa inachukuliwa na Feisal Salum “Fei Toto” na kuisambaza kwao.

Kuhusu kiwango cha Feisal Salum Mwalimu wa Yanga, Luc Eymael alikiri kuwa Feisal ameimarika mazoezini na kwenye mechi na hivyo kuonekana yupo kwenye mipango yake katika mchezo wa Derby March 8 ambao Yanga ndio wenyeji wa mchezo huo.

Luc Eymael alinukuliwa akisema “Feisal ni mchezaji mzuri sana na ana kipaji kikubwa pia, ukimuangalia mazoezini basi utamgundua ni mchezaji wa aina gani, kuna vitu vidogo sana vilikuwa vinamfanya ashindwe kufanya vizuri, nadhani kwa sasa vimemalizika na unaona jinsi ambavyo amecheza vizuri, hakika natamani acheze hivi kila siku,”

Ama kwa hakika kwa Feisal amefufuka wakati muafaka haswa katika kulekea mchezo dhidi ya Simba na hivyo kumpa mwalimu uchaguzi mwingi katika eneo la kiungo.

Feisal anakua tumaini jingine kwa Wanayanga katika eneo la kiungo na kutengeneza muunganiko mzuri kati yake na viungo wengine kina Haruna Niyonzima , Balama Mapinduzi na Papy Tshishimbi ili kuweza kuwadhibiti kina Jonas Mkude, Chama,Francis Kahata na Luiz Miquissone wa Simba.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Manchester Derby: Pambano lisilotabirika

mtanange wa YANGA NA SIMBA

Simba walishinda nje ya uwanja , Yanga wakashinda ndani ya uwanja