in , ,

FADLU DAVIDS ANA NAFASI SIMBA

LIGI KUU imetamatika na Kila timu imevuna ilichopanda. Mashabiki wameshangilia tangu mwanzo hadi mwisho wa Ligi. Hali kadhalika wapo walioumizwa na matokeo mabaya mara kadhaa. Hata hivyo Ligi imetamatika ikiwa na sura tofauti Kwa vilabu mbalimbali ikiwemo Simba. TANZANIA SPORTS katika tathimini yake, inaonesha kuwa Simba ni klabu ambayo inatakiwa kutembea kufua mbele licha ya kukosa Mataji muhimu msimu huu. Pamoja na Kwamba timu zinacheza ili kutwaa Mataji lakini sio Kila wakati matokeo hayo huwa yanakuja kadiri wanavyopenda. Kuna wakati klabu inacheza vema lakini mwisho wa mchezo matokeo yanakuwa kinyume.

Hapo ndipo anapoingia Fadlu Davis, kocha wa klabu ha Simba. Ni kocha ambaye unaweza kusema ana nafasi kubwa Simba kufanya vizuri endapo atapewa nafasi hiyo. 

MSIMU WA KWANZA FAINALI YA KWANZA. 

Imepita miaka.mingi Kwa klabu ya Simba kucheza mchezo wa fainali katika mashindano ya CAF. Simba wanakuwa wakishriki mara kadhaa kwenye mashindano ya CAF na kuishia nafasi ya robo fainali kwenye Ligi ya Mabingwa au Kombe la Shirikisho. Kocha Fadlu Davids ameingiza Imani Kwa mashabiki wa Simba. Aliwafanya waamini kuwa inawezekana kutwaa ubingwa wa Afrika. Simba walifika fainali ya Kombe la CAF mwaka 1993, ni kipindi kirefu ambacho hata baadhi ya mashabiki hawajui utamu wake ulikuwaje na shangwe lake likoje. Lakini katika zama za Teknolojia, mashabiki wa Simba wamefanikiwa kushuhudia timu yao ikitinga fainali ya Kombe la Shirikisho na kulikosa Kwa idadi ya mabao tu. Sina Nia ya kukumbusha matokeo ya mechi mbili za fainali kati ya  Simba ya Tanzania na RS Berkane ya Morocco bali kuonesha umuhimu wa kufikia hatua hiyo. 

Fadlu Davids ameongoza Simba katika msimu wake wa kwanza na kufikisha fainali. Huyu ni kocha ambaye hakulalamikia usajili Wala aina ya viwanja alivyotumia katika mazoezi popote Tanzania lakini ameifanya Simba iwe timu iloyoongeza thamani mikononi mwake. Ametumia wachezaji walewale aliokabidhiwa na kuifikisha nusu fainali ya Kombe la Shirikisho ya CRDB na kumaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu. Inafahamika kuwa Simba ni timu ya makombe lakini ukweli ni kwamba kocha huyu ana nafasi kubwa ya kuongeza tija Kwa klabu hiyo. 

USHAMBULIAJI

Hivi karibuni kocha huyo alinukuliwa kuwa anategemea kuwasilisha mapenzekezo yake Kwa uongozi na kuona namna wanavyoweza kufikia malengo. Eneo ambalo bila shaka Simba wanatakiwa kuboresha ni safu ya ushambuliaji. Ni safu ambayo Ina mabao machache na hivyo Jean Ahoua anabaki kuwa kiungo mwenye mabao mengi kuliko washambuliaji. Safu hii inatakiwa kuongezewa nguvu au kufanyiwa mabadiliko ili kumsaidia Fadlu Davids kuwa na mchango Mkubwa kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao. Ili Simba ipige hatua zaidi kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa inatakiwa kusajili washambuliaji wawili au mmoja ambaye ataongeza mchango kwa klabu hiyo. Mshambuliaji huyo anatakiwa kuwa na uzoefu na sifa katika Soka la Kimataifa ili kuipa hadhi nafasi hiyo na kupachika mabao ha kutosha. 

Fadlu Davids anahitaji mshambuliaji mwenye uwezo wa kufunga magoli si chini ya 20 kwa msimu upande wa Ligi Kuu kisha Ligi ya Mabingwa awe na uwezo wa kupachika si chini ya mabao 15. Hii Ina maana Simba wanahitaji safu ya ushambuliaji yenye uwezo wa kufanga mabao 50 kwa msimu mbali ha mchango wa viungo na mabeki wao.

NAMBA 8

Debora Fernandez alikuwa mchezaji anayetegemewa kuongoza safu hii akiwa sambamba na Jean Ahoua. Hata hivyo Fernandez alipotezwa vibaya kwenye kikosi cha kwanza kutokana na ushindani wa namba. Kocha wa Simba anatakiwa kusikilizwa katika idara ha kiungo namba 8 kwani imekuwa ikitumia wachezaji tofauti bila kupata matokeo makubwa. Awesu anaweza kucheza namba hiyo lakini haionekani kuwa atamudu kudumu kikosini. Ni nafasi muhimu ambayo ni sehemu ya injini ya Simba kwahiyo usajili mpya unahitajika ama wachezaji wawili hawa waandaliwe kubeba mzigo mzito msimu ujao. 

MAKOSA BINAFSI

Wachezaji wa safu za Ulinzi na ushambuliaji ndio wanaoongoza Kwa kufanya makosa. Safu ya ushambuliaji inafanya makosa Kwa kushindwa kupachika magoli, wakati walinzi wanasababisha timu pinzania kupata magoli. Mara kadhaa safu ya ulinzi ya Simba imesababisha wapinzani wao kupata magoli mepesi ama kusababisha Simba kufungwa. Kwa maana hiyo safu hizi mbili zinatakiwa kuandaliwa vyema msimu ujao wakati wanaenda kushiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

USTAHIMILIVU WA UONGOZI 

Hakuna Siri yoyote ambayo italeta mafanikio kama viongozi watakubali kuwa wavumilivu wakati Wanaingia msimu mpya wa 2025/2026. 

Viongozi wa Simba wanatakiwa kumpa nafasi na mamlaka kwenye suala la ujio wa wachezaji na aina yake anayotaka. Kocha huyo ameonesha uthabiti katika mechi kadhaa za msimu wake wa kwanza. Ni Imani Kwa kocha ndiyo itaipa Simba mafanikio. Hapo ilipofika msimu huu inaweza kuendelea kumwamini ili waweze kupata mafanikio. Bila shaka kocha huyu anawindwa na vigogo wa Soka Afrika kwahiyo ni suala la viongozi wa Simba kuwa wavumilivu kuhakikisha kocha wao anapata mahitaji muhimu katika kikosi chake ili asiingiliwe na mawazo ya kuondoka klabuni hapo.

Report

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

What do you think?

50 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Sakata la dabi ya Kariakoo, tumejifunza nini?

Tanzania Sports

Ibenge ni ‘Jose Mourinho’ wa Afrika mashariki