MIAKA ya karibuni wachezaji wa Kibrazil waliadimika kwenye timu kubwa za England, Italia, Ufaransa, Ujerumani na Hispania na badala yake makipa wakawa maarufu zaidi. Wengi wao walikuwa wanacheza soka katika Ligi ya Ureno na nyinginezo ndogo barani Ulaya. Lakini sasa mambo yanabdilika siku hadi siku. Wabrazil walikuwa kwenye timu za kaaida za EPL, mfano Bruno Guimares na Joelinton wapoi Newcastle United.
Timu ka Arsenal wana mastaa kama vile Gabriel Jesus, Gabriel, Martinelli, ambao ndiyo unaweza kusema walikuwa kwenye timu kubwa pamoja na Alisson Becker golikipa wa Liverpool. Manchester City walikuwa na Ederson, na sasa wamemsajili Savinho. Manchester United walimsajili Casemiro. Kwa ujumla wachezaji wa Kibrazil wamekuwa wakielekea Ligi za Italia na Hispania lakini hawakuwa wengi wenye vipaji vikubwa. Imezoeleka wachezaji wengi wa Kibrazil wanakuwa wale wenye uwezo mkubwa katika soka, lakini kuadimika huko haikuwa na maana ya kupotea kabisa bali lili wimbi la wachezaji mahiri ndilo lilioadimika.
Wachezaji wa Brazil walikuwa wanacheza timu ndogo ndogo jambo ambalo si kawaida yao. hata hivyo EPL inatarajia kupokea mgeni mpya kutoka nchini Brazil kuanzia msimu ujao. TANZANIASPORTS inakuletea uchambuzi kuhusiana na mgeni huyu mpya anayeingia kwenye Ligi Kuu England kuendelea kukuza hadhi na thamani ya soka la Kibrazil. Je Estevao ni nani?
Tiago Silva alikuwa nahodha na beki kisiki wa Chelsea.
Nyota huyo anatokea Brazil na alijiunga Chelsea katika nyakati za mwisho za kustaafu soka. Lakini kutokana na uhaba wa mabeki Tiago Silva alionekana bado lulu huku mwenzake David Luiz akiwa ameondoka kwenye soka la ushindani. Lakini ni Chelsea hao wameibuka tena kwa usajili wa kipaji kutoka Brazil.
Palmeiras kama shamba la vigogo
Kwa miaka ya karibuni klabu ya Palmeiras imegeuzwa kuwa shamba la mavuno ya timu vigogo. Endrick aliondoka Palmeiras, Rodrygo Goes aliondoka Palmeiras, Vitor Reis ameondoka Palmeiras. Na sasa Estevao Willian anaondoka Palmeiras kwenda Chelsea ya England.
Estevao Willian anatarajiwa kujiunga na klabu ya Chelsea inayonolewa na Enzo Muresca akitokea klabuya Palmeiras kwa ada ya pauni milioni 56 sawa na Dola milioni 71. Mengi yanatarajiwa kutoka kwa kinda huyo wa Kibrazil ambaye ameonekana kuwa nyota mahiri wa baadaye katika ulimwengu wa soka. Akiwa katika umri mdogo Estevao Willian amekuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Palmeiras ya Brazil.
Akizungumzia usajili wa kinda huyo, staa wa Brazil Neymar Junior amesema anamtakia kila lenye heri Estevao Willian na kusisitiza kuwa siku moja maelfu ya watu watampigia kura ya uchezaji bora wa Dunia. Neymar anaamini kuwa Estevao atakuwa mchezaji wa aina yake wa Kibrazil. Neymar na Estevao walikutana siku za hivi karibuni katika klabu za starehe, ambapo alitumia muda wake kumpa ushauri kinda huyo kuhusu maisha ya Ulaya kwa ujumla licha ya kwamba staa huyo hakuwahi kucheza soka England kama wengine.
Naye rais wa Palmeiras, Leila Pereira, amesema Estevao Willian ndiye mchezaji bora wa Dunia ajaye na mashabiki wajiandae.
Nyota huyo ameonesha kiwango bora katika klabu yake na anatarajiwa kudumisha akiwa kwenye uzi wa Chelsea. Hata hivyo kabla ya kwenda Chelsea, Estevao atakuwa na kibarua cha mwisho kwenye fainali za klabu bingwa ya Dunia mwezi Juni mwaka huu akiwa na kikosi cha Palmeiras. Klabu hiyo itaanza kupepetana na Inter Miami ya Marekani kwenye hatua ya makundi, ambapo atakuwa anakipambana na nyota wa Dunia Lionel Messi.
Je Estevao ni nani?
Jina lake kamili ni Estevao Willian Almeida de Oliviera Goncalves. Alizaliwa Aprili 24, 2007. Ni maarufu kwa jina la Estevao Willian au Estevao. Nyota huyu alizaliwa huko Franca jijini Sao Paulo na alianza safari yake ya soka katika akademi ya Cruzeiro mwaka 2017. Mwaka 2018 akiwa na umri wa miaka 10 Estevao Willian alisaini mkataba wa mchezaji wa kulipwa na kampuni ya Nike, na kumfanya chipukizi wa Kibrazil wa kwanza kusainiwa na kampuni hiyo.
Mkataba wake ulivunja rekodi ya nyota mwenzake wa Kibrazil Rodrygo. Alihamia katika akademi ya Palmeiras mwaka 2021. Msimu wa 2022 alisaidia timu ya watoto ya Palmeiras kutwaa mataji kadhaa. Oktoba mwaka 2023 Estevao alifunga mabao matatu kwenye mchezo wa fainali wa mashindano ya Campeonato-Paulista chini ya miaka 17. Aliazna kusakata kandanda katika kikosi cha wakubwa desemba 2023 wakati akiingizwa katika dakika 78 kwenye mchezo kati ya Palmeiras na Cruzeiro. Akiwa na umri wa miaka 16 na miezi 8 alitajwa kuwa kinda wan ne wa klabu hiyo kucheza kwenye kikosi cha wakubwa.
Usajili wake Chelsea
Juni 22, 2024 klabu ya Chelsea ilitangaza kwamba Estevao Willian atajiunga klabuni hapo katika msimu wa 2025/2026 mara baada ya kutimiza miaka 18. Dili hilo lilifikia kasi cha pauni milini 34 pamoja na pauni milioni 23 zitalipwa Palmeiras kadiri atakavyoonesha kiwango bora.
Timu ya Taifa
Estevao aliitwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Brazil chini ya miaka 17 Oktoba mwaka 2022. Baadaye aliitwa kwenye kikosi cha timu ya wakubwa kwa mara kwanza Agosti 23, 2024 katika mechi za kuwnaia kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2026 dhidi ya Ecuador na Paraguay. Alianza kuichezea timu ya wakubwa septemba 6, 2024 kwenye mchezo dhidi ya Ecuador. Aliingia katika dakika 61 kuchukua nafasi ya Luiz Henrque katika ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ecuador.
Estevao ni mi mchezaji wa aina gani?
Estevao amekuwa akifananishwa na Lionel Messi na Pele. Jina lake la utani ni Messinho likiwa na maana ya Messi mdogo kutokana na aina yake ya uchezaji kufananishwa na nyota huyo wa Argentina. Anasifika kwa utulivu awapo uwanjani na mtaalamu wa kusoma mchezo pamoja na umahiri wake katika kufanya uamuzi wenye manufaa kwa timu. Ni mchezaji haswa wa kIbrazil.
Comments
Loading…