in

EPL washabiki kurudi

Tukiwa uwanjani kwenye moja ya mechi za EPL, na aliyekuwa Balozi wetu Uingereza, Mhe, Peter Kallaghe.

*Je, wataimba, kukumbatiana, kunywa?

Pamekuwapo tofauti kubwa ya soka wakati wa janga la Covid-19 na kabla ya matokeo yake, na kwa hakika ilipooza.

Hii ni kwa sababu washabiki walizuiwa kuingia uwanjani kwa ajili ya kukinga maambukizi ya virusi vya Corona. Sasa washabiki katika Ligi Kuu ya England (EPL) wataruhusiwa kurejea viwanjani.

Lakini bado kuna sintofahamu juu ya wakati huu ambapo pamekuwapo ahueni ya janga hili; watu wakijiuliza iwapo wataingia uwanjani na kutakiwa kukaa kimya tu kana kwamba wamejikunyata au wataruhusiwa kuwa na bashasha zile kama za kuimba, kukumbatiana kufurahi au hata kuingia na vinywaji kama zamani.

Washabiki wa soka, hasa wale kindakindaki hawakufurahia hali iliyowakuta, ambapo zama zile washabiki hadi 60,000 walikuwa wakijazana viwanjani. Majuzi tuliona washabiki 8,000 tu wakiruhusiwa kwenye mechi Uwanja wa Taifa – Wembley kwenye fainali ya Kombe la Ligi – Carabao ambapo Manchester City waliwapiga Tottenham Hotspur 1 – 0 mwezi jana.

Ama kwenye fainali ya Kombe la FA ambapo Leicester waliwatungua Chelsea waliingia watu zaidi ya 20,000. Na sasa, baada ya miezi mingi mno, washabiki wataanza kurejea kwa wingi viwanjani kwa ajili ya EPL.

Licha ya uchache wa washabiki walioruhusiwa kuingia, wachezaji kwenye fainali hizo za nyumbani walizungumza kwa namna chanya juu ya umuhimu wa washabiki. Kumbe kurejea kwa washabiki viwanjani kunatarajiwa kuwa na maana kubwa kwenye mechi husika.

Haitakuwa saw ana kile watu walichozoea, lakini Mkurugenzi wa Leeds United, Angus Kinnear, anaamini kwamba wageni wa Elland Road wanaweza kutarajia hali wasiyoitegemea kutokana na kupunguzwa kwa idadi ya watu.

Tanzania Sports
Mashabiki uwanjani

Ni wazi kwamba idadi si ile ya 40,000 au zaidi wanaokuwa katika chereko na hekaheka kubwa uwanjani n ahata nje, lakini ukweli ni kwamba tupo kwenye mwelekeo sahihi, ikiwa ni hatua moja kuelekea kuvijaza viwanja kama zamani, kukumbatiana, kushabikia kwa nguvu, wengine kulia na mengine yanayoambatana na matukio ya wakati husika.

Zipi basi ni kanuni za Bodi ya EPL kuhusiana na washabiki kurejea? Ni kwamba wanarudi lakini si kuvijaza viwanja; ni kwa idadi maalumu. Timu zitaweza kuchukua washabiki 10,000 au asilimia 25 ya uwezo wa uwanja – idadi itakayokuwa ndogo zaidi na hiyo pia ni kwa mwongozo wa Serikali ya Uingereza.

Washabiki wanaorejea lazima wajaze fomu ya maswali kabla ya kuhudhuria mechi, lengo likiwa ni kupunguza kwa kiasi kikubwa maambukizi ya Covid-19. Klabu nyingi zitatoa kanuni za maadili kwa washabiki wao, zikieleza kwa kina masuala mahsusi ya klabu na juu ya viwanja vyao, namna ya kupata tiketi na hatua za kiusalama kujikinga.

Ilivyo kwa sasa ni kwamba washabiki watakaoruhusiwa ni wa timu ya nyumbani tu huku wale wa ugenini wakiwa bado hawatakiwi. Hii ilifanyika baada ya mashauriano ya Bodi na klabu za EPL. Hii inamaanisha kwamba timu ya nyumbani ndiyo inafaidika na si vinginevyo.

Bodi ya EPL, hata hivyo, inatarajia kwamba kwa msimu ujao, yaani 2021/2022 viwanja vitarudi katika hali ya kawaida kwa washabiki kuruhudiwa kujaa kwa nafasi zao. Hii iitategmea na mpango wa serikali wa kuondokana na kanuni kali za lockdown.

Juni 21 kuna maelekezo mapya yatakayotoka kuhusiana na janga hili na kipi watu wafanye kutokana na shaka kubwa inayoingia kwa sababu ya virusi aina mpya vya India kwa Covid-19. Hata hivyo, kwa sasa, washabiki hawatatakiwa kuwa na cheti cha kupima Covid-19 ili kuweza kuhuduria mechi japokuwa kuna protokali za kufuata.

Vyombo vikubwa vya soka Uingereza, ikiwamo Bodi ya EPL na EFL viliiandikia Serikali Aprili kuunga mkono pasi za kusafiria za Covid-19. Hiyo inajumuisha taarifa juu ya chanjo na kinga ya mwili lakini wazo hilo bado lipo katika mchakato, lengo kubwa likiwa ni kuondokana na vitu kama kukaa kwa umbali kati ya mtu na mtu na matumizi ya barakoa.

Kwa sasa lazima watu wavae barako viwanjani, isipokuwa kwa sababu maaluu. Itaruhusiwa kunywa uwanjani na kwingineko nje na marafiki japokuwa kutakuwa na masharti. Itakuwa ngumu kushangilia kama zamani kwa sababu ya ulazima wa kukaa kwa umbali na hiyo ndiyo sababu ya kupunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya washabiki viwanjani.

Kukumbatiana ni suala la watu kuamua, ambapo Serikali ya Uingereza imetaka watu waamue binafsi kuona iwapo wapo salama kukumbatia wengine. Kuimba ni uamuzi wa washabiki pia na tumeona wakifanya hivyo kwenye fainali ya Kombe la Ligi na Kombe la FA.

Washabiki wanashauriwa kuwasili mapema viwanjani ili kuepuka misongamano wakati wa kuingia – ili kila mtu aingie kwa nafasi ya kutosha. Si rahisi kwa watu, hata wenye tiketi za msimu, kukaa kwenye siti zao maalumu walizozoea kutokana na ulazima wa kuketi mbalimbali.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
SIMBA SPORTS CLUB

Simba wametoa onyo Afrika

Manchester City vs Chelsea Champions League final

Fainali ya UEFA bila washambuliaji