in

LoveLove SurprisedSurprised

Tanzania na utumiaji wa viwanja vya michezo

Tanzania moja ya nchi nyingi barani Afrika ambazo zimejaliwa kuwa na viwanja vingi vya mchezo wa mpira wa miguu ambavyo matumizi yake yanastaajabisha ulimwengu.

Wakati mwingine  unaweza kukubali ule msemo unaosema kuwa Afrika ni dunia ya tatu, hii ni kweli kama ukikasirika basi dawa itakuwa imekuingia.

Kwanini dunia ya tatu vitu vyetu huku vinaenda kinyume kabisa na vitu vya Ulaya na nchi nyingine duniani, hapa sasa hata maisha ya kawaida, Hospital,Shule na katika michezo.

Labda tukae humu katika michezo huko katika shule na hospitali watazungunza watu wa habari za kisiasa na uchumi ‘Hard news’.

Viwanja vilivyopo vinamatumizi zaidi ya moja ni zaidi ya kusudio la viwanja vyenyewe, maana kama ulijengwa kwa ajiri ya mpira wa miguu ‘Football’ kwanini utumike na watu wa Magwaride ? kwanini utumike na watu wa burudani ?

Maswali mengi kwa wakati mmoja, taratibu utajua kwanini tumekuwa dunia ya tatu.

Mfano mzuri msimu huu tu wa ligi kuu Tanzania Bara kilichotokea uwanja wa Sokoine baada ya kufanyiwa shughuli ya burudani hali yake kila mmoja aliona, uwanja ulilowa maji na matope hadi mchezo mmoja kati ya Yanga na Tanzani Prisons ulipelekwa katika uwanja wa Samora mkoani Iringa.

Hii sio mara moja pia iliwahi kutokea uwanja wa Kambarage kule Shinyanga, aina hii hii iliwahi kutokea na shughuli za michezo zilisimama kwa muda kupisha hali ya uwanja ikae sawa kwa mecho zilizopangwa mkoani humo.

Shughuli za kijeshi zitafutiwe sehemu zake zijengewe utaratibu unaofaa na inawezekana, si wanasema kuwa seriklali inamkono mrefu ? . Unaweza ukaangalia ukweli ambao nausema hapa na mambo ya kufikirika ambayo bado umeyajenga kichwani kuwa haiwezekani kutengeneza utaritbu mzuri ili tufike huko.

Hapa sasa natolea mfano kuwa ule uwanja wa uhuru ungetengwa kwa ajiri ya shughuli nyingine tu, ikiwemo majeshi, haraiki na mambo mengine ambayo hayahusiani na soka kabisa. Huku pale kwa mchina kungebaki na michezo tu, mchakato huu ungewekwa kwa mikoa yote na utaweza kuona mabadiliko makubwa sana ya soka na pia shughuli nyinge nazo zitaenda vizuri.

Nilishawahi kuona hapa Dar es Salaam katika uwanja wa Uhuru na Taifa kuna mechi zilipangwa uwanja wa kwa Mchina baadae ratiba waliibadilisha wakachezea Uhuru, tatizo kulikuwa na shughuli za kiserikali.

Wale watu wanaojiita wanaharakati wa michezo hizi ndio vitu za kupigia kelele sio kila siku mnakaa ndani ya studio na kuchambua timu na wachezaji wakati hamuwezi kuchambua maendeleo ya huo mchezo wenyewe.

Mnatamani sana Tanzania ipeleke wachezaji wengi nje ila kwa namna hii mtakuwa mnapaka mafuta kwa mgongo wa chupa, au mnatwanga maji katika kinu.

Sio kwamba nakataa wasifanye shughuli niyngine bali utengenezwe utaratibu mpya utakaojitofautisha na haya yanayoendelea, hii ndio itakuwa jawabu la kuelekea katika weledi.

Twende katika weledi sasa tuanzie hapa hapa Afrika Rwanda wao hawana tofauti na Tanzania ila walichokifanya wametengeneza mfumo mzuri kwa wasanii wao kufanyia ‘shows’ zao sehemu moja sio uwanjani kama huku.

Wao wametengeneza Arena ambayo inatumika katika shughuli zote za burudani, yaani Ali Kiba akienda Rwanda au Diamond akienda huko atafanya shughuli zake hapo, hayo yote yamefanywa na serikali ya nchi hiyo niwape kongole kunyweni mtori nitakuja kulipa.

Ila bado katika mambo mengine wanabakia kama ilivyo Tanzania kwa mfano shughuli za Kiserikali zinafanyika katika ‘Pitch’ kama kawaida.

Ulaya wenzetu wanavyofanya viwanja vyao vya kuchezea mechi vinabaki kwa shughuli hiyo tu, ila wanasemu maalumu ya kufanyia mazoezi mfano Arsenal wanayosehemu ya mazoezi iliyopo maeneo ya jiji la London Colney.

Hivyo hivyo Manchester United nao wanasehemu yao ya kupiga tizi upo kule Carrington, wanafanya yao huku kisha katika mechi wanarejea Old Trafford.

Karibuni vilabu vingi Ulaya vinafanya hivi, hii ndio tunaita Weledi ama kwa lguha ya kizungu ‘Professionalism’.

Maisha ya soka yanatakiwa yawe namna hii ila kwakuwa uwezo wa bongo mdogo basi tufanye mazoezi katika viwanja husika ila tusiingize shughuli nyingine ndani yake tunafeli sana.

Tanzania Sports
Wanamichezo

Huenda mawazo yangu yakawa mbele zaidi ya hapa ila hili litakapothibiti utarudi kuisoma makala hii huku ukitabasamu, kwani kuna aliyewahi kuiona ‘Compture’ wakati Sunday Manara anacheza na wamempa jina hilo si imekaa kitambo kisha ndio wengi wameanza kuona matumizi yake.

Je baada ya kusoma matumizi ya viwanja hivyo maendeleo tunayoyataka kweli yatafika, wachezaji wetu tunaowataka wakacheze kimataifa kweli watafika leo? Hilo baki nalo kichwani kwako siku wakitegua kitendawili hiki basi nitarudi na karamu yangu kuelezea namna gani sasa tunapiga hatua.

Nignependa niendelee na mjadala huu maada ya matumizi ya viwanja ni ndefu mfno ila tosheka kidogo na hiki nimejaribu kukustua ili uone jinsi gani tupo nyuma ya maendeleo.

Bila kusahau kuwa viwanja vingi hapa Tanzania vinamilikiwa na chama tawala basi fanyeni maamuzi mambo yaende muswano.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

75 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply
  1. I read your article on Torres he sounded like a very grounded young man with huge potential and quite a clear plan of where he wants to go.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Ligi kuu England

EPL bila udambwidambwi itawezekana kweli?

Tanzania Sports

Kriketi Tanzania inafelishwa na viongozi