in , , ,

Diego Costa ashitakiwa

*Gabriel naye anatakiwa kutoa maelezo*

 

Chama cha Soka (FA) kimemshitaki mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa kwa utovu wa nidhamu uwanjani.

Hatua hiyo imekuja siku mbili baada ya wadau wengi kuonesha kushangazwa na hatua za mwamuzi Mike Dean aliyechezesha mechi baina ya Arsenal na Chelsea kutompa adhabu mchezaji huyo.

Costa alikuwa tangu mwanzo wa mchezo huo akiwabughudhi mabeki wa Arsenal kwa maneno na mashambulizi ya mikono nyusoni na shingoni, ikiwa ni pamoja na tukio la kumkaba Gabriel Paulista aliyeshindwa kujizuia kiasi cha kupewa kadi nyekundu.

Alimpiga mara tatu mlinzi wa kati wa Arsenal, Laurent Koscielny lakini mwamuzi Dean alikaa kimya kisha baadaye akaamua kumpa kadi nyekundu Paulista, kwenye mechi ambayo Arsenal walishindwa 2-0.

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger alieleza wazi mapema kukerwa na Costa na kusema kwa mambo aliyofanya uwanjani alistahili si tu kadi nyekundu, bali pia kufungiwa mechi tatu. Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho alibaki akijidai kumshabikia Costa, huku akipambana na vyombo vya habari vilivyotaka maelezo juu ya tabia ya Mhispania huyo.

Mtafaruku uliopelekea Arsenal kumaliza mechi ikiwa na wachezaji tisa tu...
Mtafaruku uliopelekea Arsenal kumaliza mechi ikiwa na wachezaji tisa tu…

Costa, 26, ametakiwa na FA kutoa maelezo ya jinsi walivyohusika na kadhia hizo na klabu zote kwa kushindwa kuwadhibiti wachezaji wao. Tayari Arsenal wamekata rufaa dhidi ya kadi nyekundu ya moja kwa moja ya Paulista inayomaanisha atakosa mechi tatu.

Costa amepewa hadi saa 12 jioni ya Jumanne hii kujibu mashitaka dhidi yake, ambayo ni kuhusu mashambulizi dhidi ya Koscielny. Baada ya kuthibitisha kwamba waamuzi hawakuona tukio hilo, FA wametoa nakala ya video husika kwa jopo la waamuzi watatu wa zamani litakaloshughulikia suala hilo.

Watatakiwa kuupitia mkanda na kila mmoja atatoa uamuzi ikiwa ilikuwa kadi nyekundu ya moja kwa moja na baada ya hapo FA wataendelea na mashitaka yao. Ikiwa Costa atakubali kosa hilo kabla, ataanza kutumikia adhabu ya kukosa mechi tatu, lakini akikana itabidi tume huru ya udhibiti itoe uamuzi.

Mechi tatu za Chelsea zijazo ni dhidi ya Walsall, Newcastle na Southampton. Gabriel naye anatakiwa kutoa maelezo juu ya kadhia iliyotokea, huku kiungo Santi Cazorla aliyepewa kadi mbili za njano na kutolewa nje, ameonywa kwa aina yake ya mchezo. Gabriel na klabu zote mbili wanatakiwa kutoa maelezo ifikapo au kabla ya Alhamisi hii saa 12 jioni.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Samatta wa Ulaya

Tanzania Sports

SUNDERLAND AFC RETURN TO ZAMBIA