in , , ,

Diaby kupiga ‘deiwaka’ Arsenal?

 

 

Kiungo wa Arsenal, Abou Diaby anamaliza mkataba wake Emirates akiwa amecheza mechi 16 tu katika misimu minne, lakini The Gunners wanaona ugumu kumuacha aondoke.

 

Ameshindwa kucheza kwa sababu ya majeraha ya kila mara, hivyo kwamba amekuwa akilipwa mshahara bila kufanya kazi na sasa ‘Profesa’ Arsene Wenger anafikiria kuandika mkataba mpya, ambapo Mfaransa huyu atalipwa kwa kadiri atakavyocheza.

 

Wenger ni mtu mwenye heshima kubwa kwa mchezaji wa kaliba ya Diaby na amekuwa wakati wote akitafuta jinsi ya kumrejesha kwenye kikosi cha kwanza. Amepona majeraha yake na majuzi alicheza na kikosi cha U-20 sambamba na Mikel Arteta na Mathieu Debuchy.

 

Kadhalika inaelezwa kwamba Wenger yu tayari kuona Diaby (28) akiendelea kupewa huduma na Washika Bunduki wa London hadi arejee hali ya kawaida hata kama hakutakuwapo mkataba rasmi, ili baada ya muda afanyiwe tathmini juu ya utimamu wa mwili wake.

 

Ni katika hali hiyo, Wenger amependekeza kwamba ikiwa Diaby atakubali basi alipwe kwa kadiri ya mechi atakazokuwa akicheza, kwa sababu haieleweki ni lini na wapi ataumia.

 

Imekuwa kawaida akirejea uwanjani hakosi kuondoka na majeraha katika kipindi kifupi na humweka nje kwa muda mrefu. Licha ya kifundo cha mguu amepata kuugua goti

 

Matatizo yake yalitibuka baada ya kuvunjika kifundo cha mguu 2006 na tangu hapo amekuwa akiumia hapo au kiungo kingine. Wenger amekuwa akisema rafu ya beki wa Sunderland, Dan Smith ndicho chanzo cha matatizo ya Mfaransa mwenzake huyo anayelipwa pauni 65,000 kwa wiki.

 

“Diaby hana tatizo la akili bali la kuumia. Ni mchezaji ninayemheshimu sana. Kila akirudi uwanjani anaumia na kuanza tena kwenye sifuri, aliharibiwa na rafu mbaya inayomsumbua hadi sasa. Akirudi nitambakiza kundini, daima ninamwamini,” anasema Wenger.

 

Mkataba wa Diaby aliyesajiliwa Januari 2006 unamalizika msimu wa kiangazi na Wengere anasema ameshazungumza naye, ni kiasi cha mwenyewe kufanya uamuzi kabla ya kukutana tena kuhitimisha mazungumzo

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Yanga na mfupa wa ubingwa Tanzania

LIGI YA MABINGWA ULAYA