in , , ,

Corona na hatari ligi kubwa Ulaya


*Mechi ya Arsenal na Man City imeahirishwa


*Italia wamesitisha michezo ya Ligi Kuu yao


*Hispania, Ufaransa kucheza bila washabiki

Dunia inatikiswa kwa nguvu wakati huu na kirusi hatari cha Corona, ambapo athari kubwa ni Italia, lakini hadhari imeanza kuchukuliwa England, Hispania na Ufaransa.

Wakati Italia inao waathirika wengi wa maradhi yanayosababishwa na kirusi hicho kinachojulikana kitaalamu kama COVID-19, tayari wameahirisha Ligi Kuu ya Italia – Serie A.

Shirikisho la Soka la Italia (FIGC) linasema kwamba huenda ligi kuu yao isikamilike msimu huu kutokana na athari kubwa za ugonjwa huo. Walifikia hapo baada ya mkutano uliofanyika jana Jumanne.

Kwa sasa wamesitisha mechi zote za Serie A hadi Aprili 3, kutokana na maelekezo yaliyotolewa na serikali kusitisha mikusanyiko kukwepa kusambaa zaidi kwa ugonjwa huo uliosababishwa na kirusi kuingia baada ya kuwa wameacha mipaka yao wazi bila hadhari kutoka China.

Rais wa FIGC, Gabriele Gravina anasema uwezekano ni kuja kufanya mechi mbili mbili kwa walio juu nyumbani na ugenini ili kupata bingwa au kutangaza kwamba hadi walipofika ndipo mwisho wa msimu wa 2019/2020 kuendana na hali ya ugonjwa huo itakavyokuwa mwezi ujao.

Wakati hayo yakijiri Italia, nchini Hispania na Ufaransa wakuu wa soka wameamua kwamba kwa sasa mechi zichezwe bila washabiki baada ya wachezaji na maofisa wa klabu husika nao kuchukuliwa tahadhari inayotakiwa.

Bodi ya Ligi Kuu ya Hispania – La Liga imetangaza kwamba mechi za raundi ijayo zitafanyika bila waashabiki hadi Aprili 15 watakapofanya tathmini ya ugonjwa husika. Wanasema wamechukua hatua hiyo kwa kuitikia maelekezo ya Wizara ya Afya.

Ama Serikali ya Ufaransa imetangaza kupiga marufuku mikusanyiko ya zaidi ya watu 1,000 wakati nchini Ujerumani, mechi baina ya Borussia Monchengladbach dhidi ya Cologne katika Ligi Kuu ya Ujerumani – Bundesliga, itachezwa usiku wa Jumatano hii bila washabiki na ndivyo itakuwa pia wikiendi kwenye mechi nyingine tisa za ligi kuu hiyo.

Hata hivyo, mechi baina ya Union Berlin na Bayern Munich Jumamosi hii itaendelea kama kawaida wakiwamo washabiki huku hatima ya mechi nyingine tatu ikiwa haijaamuliwa. Waziri wa Afya wa Ujerumani, Jens Spahn ametangaza kuzuia mikusanyiko ya zaidi ya watu 1,000 katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo.

Nayo mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) baina ya Barcelonawa Hispania na Napoli wa Italia itafanyika kwenye uwanja mtupu wa Nou Camp Machi 18.

Nchini hapa England, mechi ya Ligi Kuu (EPL) baina ya Manchester City na Arsenal iliyoahirishwa awali kupisha mechi ya Kombe la Ligi baina ya City na Aston Villa, sasa imeahirishwa na leo Jumatano haitafanyika tena.

Hii imetokana na wachezaji wa Arsenal kukutana na mmiliki wa klabu ya Olympiakos,

Evangelos Marinakis contracted coronavirus.ambaye ametangaza kuwa ana virusi vya Corona. Arsenal wanasema kwamba mmiliki huyo mwenye umri wa miaka 52 alikutana na wachezaji wao kadhaa walipocheza wiki mbili zilizopita katika mechi ya Ligi ya Europa na Arsenal kupoteza na kutolewa mashindanoni.

Marinakis ambaye pia anamiliki klabu ya Ligi Daraja la Kwanza ya England – Nottingham Forest – alisema alipimwa na kukutwa na Covid-19. Olympiakos watachuana na Wolves kwneye Ligi ya Europa Alhamisi baada ya Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) kukataa maombi ya Wolves kuahirishwa kwa mechi hiyo.

Bodi ya EPL imesema kwamba bado haijapanga kuahirisha mechi nyingine na kwamba hatua zote muhimu zitachukuliwa kuhakikisha wachezaji na maofisa wapo salama kiafya. Brighton wanasema kwamba mechi baina yao na Arsenal Jumamosi ya wiki hii inatarajiwa kusonga mbele kama kawaida.

Hatari kwa wachezaji wa Arsenal juu ya maradhi hayo inaelezwa kuwa kidogo sana, wamesema Brighton, wakiongeza kwamba kipindi cha tathmini cha wiki mbili kitakuwa kimeshakamilika ifikapo siku ya mechi yao. Takwimu zinaonesha kwamba kuna watu 382 waliopata ugonjwa huo nchini Uingereza, na kuna vifo sita.

Maradhi hayo huweza kusababisha homa, kikohozi na matatizo kwenye kupumua na husambazwa sehemu mbalimbali duniani baada ya kuanzia China, ambapo zaidi ya watu 116 wameshaambukizwa.

Mechi nyingine za Ulaya kati ya Manchester United, Rangers na Chelsea zitachezwa bila washabiki nchini Austria na Ujerumani siku zijazo.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Samatta: Haikuwa sahihi kusaini Villa Januari

Tanzania Sports

Liverpool: Machungu kuvuliwa ubingwa UCL