in , , ,

Chelsea, Liverpool wapigwa

 

*Man City waendelea kushinda

 

Mabingwa watetezi wa England, Chelsea na Liverpool wamefungwa katika mechi za mkondo wa nne za Ligi Kuu ya England, tena wote wakicheza viwanja vya nyumbani.

 

Chelsea wameangukia tena pua, baada ya kufungwa 2-1 na Crystal Palace katika mechi iliyochezwa Stamford Bridge, ikija siku ambayo alitamani kusherehekea mechi yake ya 100 nyumbani hapo. Walipata kufungwa 3-0 na Man City msimu huu.

 

Baada ya nusu ya kwanza kumalizika bila bao, Chelsea walitawala mchezo kwa kiasi kikubwa, lakini Palace wanaofundishwa na Alan Pardew wakapata bao kupitia kwa Bakary Sako aliyeunganisha majalo ya chini chini iliyopigwa na Yannick Bolasie.

 

Chelsea walijibu dakika ya 79 baada ya Radamel Falcao aliyeingia kuchukua nafasi ya Willian kufunga kwa kichwa, lakini Palace wakaongeza shinikizo dhidi ya Chelsea na kupata bao dakika mbili tu baadaye kupitiwa kwa Joel Ward stabbed. Mabingwa hao watetezi sasa wapo nyuma ya Manchester City kwa pointi nane.

Manuel Lanzini
Manuel Lanzini

 

Katika mechi nyingine, Liverpool wakiwa nyumbani walichezea kichapo cha 3-0 kutoka kwa West Ham, ikiwa ni mara ya kwanza kwa Hammers kushinda mechi ya ligi Angield tangu 1963, hivyo kumwongezea kocha wa Liver, Brendan Rodgers rekodi mbaya.

 

Mabao ya wageni yalifungwa na Manuel Lanzini aliyecheza kwa mara ya kwanza, Michael Noble na Diafra Sakho, kwenye mechi ambayo Philippe Coutinho wa Liver alipewa kadi nyekundu kama ilivyokuwa kwa Noble kutokana na mchezo mbaya.

 

Man City wameendeleza rekodi ya kutopoteza mchezo katika msimu huu kwenye mechi yao ya nne, baada ya kuwafunga Watford waliopanda daraja msimu huu kwa 2-0.

 

Raheem Sterling aliyesajiliwa kiangazi hiki kutoka Liverpool alikuwa na siku nzuri baada ya kufunga bao lake la kwanza kwa waajiri wake hao wapya, akipokea vyema mpira wa majalo kutoka kwa beki Bacary Sagna.

 

Bao la pili la City wanaofundishwa na Manuel Pellegrini lilitiwa kimiani na Fernandinho aliyemalizia vyema pasi ya David Silva. Watford hawakumudu kulenga hata shuti moja golini, wakati Man City walipiga mara tano.

 

Katika mechi nyingine, Aston Villa walikwenda sare ya 2-2 na Sunderland, Bournemouth wakatoshana nguvu 1-1 na Leicester na Stoke wakalala nyumbani walipocheza na West Bromwich Albion kwa bao moja. Wachezaji wawili wa Stoke, Charlie Adam na Ibrahim Afellay walipewa kadi nyekundu.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Arsenal ushindi mwembamba

Tanzania Sports

Farah, Bolt usipime