in , , ,

CHANETA IJIFUFUE UPYA KUENDANA NA WAKATI

Kwa sasa chama hicho bado kipo hai ila kuna uwezekano umaarufu wake umepungua kidogo tofauti na huko nyuma

Chaneta ni mojawapo ya vyama vikongwe vya michezo nchini Tanzania. Chama hichi kilianzishwa mnamo mwaka 1966. Chama hichi kipo kwa ajili ya kusimamia, kuendesha na kusambaza mchezo wa Netiboli ama mpira wa pete nchini Tanzania. Mchezo huu ulitambulishwa nchini Tanzania wakati wa utawala wa ukoloni wa muingereza. Mchezo huu uliasisiwa kama burudani na ulipelekwa mashuleni kote ambako kulikuwa kuna shule kwa wakati huo. Hali hii iliendelea hadi baada ya uhuru wa nchi na ndio maana sehemu kubwa ya shule nchini Tanzania zina viwanja vya mchezo huo. Katika zama za huko nyuma mashirika na taasisi za umma karibia zote zilikuwa na timu za netiboli miongoni mwa wafanyakazi wake.na suala hilo lilitimia hamasa kubwa sana ya mchezo huo na kuufanya mchezo huo kuwa ni miongoni mwa michezo maarufu nchini Tanzania. 

Maendeleo ya mchezo huu yalianza kushuka ilipofika miaka ya 1990 na hili ilitokana na miundombinu chakavu na pia kutokuwepo na mashindano makubwa ya ligi katika maeneo mbalimbali nchini. Halikadhalika ubinfsishaji wa baaadhi ya mashirika ya umma nao inawezekana uliathiri maendeleo ya mchezo huu kwani sehemu kubwa ya timu zilitokana na mashirika na taasisi za umma na baada ya kubinafsishwa hayo mashirika hayakuwa na sera ya kusapoti sana michezo. Halikadhalika kusimamishwa kwa mashindano ya Umiseta kwa miaka kadhaa nako kuliathiri maendeleo ya mchezo huu kwani wanamichezo wengi mahiri wa mchezo huu walitokana na mashindano hayo. 

Kwa sasa chama hicho bado kipo hai ila kuna uwezekano umaarufu wake umepungua kidogo tofauti na huko nyuma. Mchezo huu unachezwa kuanzia kwenye ngazi za  chini mpaka za juu. Yaani kuanzia kwenye shule za msingi kupitia UMITASHUMTA, shule za sekondari kupitia UMISETA, vyuo vikuu kupitia TUSA, serikali za mitaa kupitia SHEMISEMITA na kwingineko. Sambamba na hayo mchezo huo unachezwa katika mashindano ya Muungano na Taifa. Timu maarufu za mchezo huo ni pamoja na Bandari na Posta.

Kwa mda Fulani chama hicho kilikuwa hakivumi sana kwenye habari za michezo lakini mwanzoni mwa mwezi wa tatu chama hichi kiliingia katika kutajwa na vyombo vya habari baada ya katibu mkuu wa chama hicho mama Rose Mkisi kutuhumiwa kutoa matamshi ambayo yalishutumu serikali kutoa sapoti kubwa katika timu za taifa za soka na kutoasapoti michezo midogo. Kauli hii ilishitua kidogo na ikapelekea kuitwa kwenye kamati ya maadili ya baraza la michezo na ilipofika mnamo machi 5 katibu mkuu huyo alijiuzulu nafasi yake kwa hiari kutokana na tuhuma zilizokuwa dhidi yake za kukiuka sharia na taratibu zinazoongoza vyama vya michezo nchini Tanzania. Chaneta halikadhalika walitoa tamko kwamba hali ya sintofahamu iliyokuwa inaashiria hali iliyokuwa imejitokeza imeshashughulikiwa na kila kitu kiko sawa. Baada ya siku kadhaa timu ya taifa ya mchezo wa netiboli chini ya miaka 21 ilisafiri kwenda kwenye mashindano ya kufuzu kushiriki mashindano ya dunia.

Chama hichi kama vilivyo vyama vingine inaonekana kwamba hakipo katika hali nzuri kifedha kwani kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya mtandaoni inaonekana kwamba chama kilishindwa kupeleka wanamichezo kwenye mashindano ya Afrika yaliyokuwa yanafanyika mnamo disemba 6 mwaka 2023 katika uwanja wa ndani wa chuo kikuu cha Botswana. Mwaka huu kwa usaidizi wa serikali wamefanikiwa kusafirisha timu ya taifa ya vijana kwenda kushiriki mashindano ya kufuzu kombe la dunia la mchezo wa pete.

Chaneta inatakiwa ijifufue upya na nikisema kujifufua haimaniishi kwamba chama hicho kimekufa la hasha najua chama hicho bado kipo hai ila kuna mambo kinatakiwa kiyafanye ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya dunia kwani kwa sasa michezo ni biashara na sio riadha tena na hata huku kwetu inatakiwa ifikie hatua mchezo wa Netiboli nao ufikie hadhi hiyo. Baadhi ya mambo ambayo wanaweza kuyafanya ni kama ifuatayo:

  1. Kuviboresha vilabu wanachama viendane na mifumo ya kisasa: Chaneta inatakiwa iandae mafunzo rasmi kwa vilavu vyake vya juu ya namna ya uendeshaji wa vilabu kisasa na namna kubidhaisha vilabu hivyo ili viweze kupata udhamini mkubwa Zaidi. Pia kuvijengea uwezo vilabi hivyo kuwa na wasemaji wa vilabu hivyo na hatimaye viweze kuwa na hamasa ambayo itawapelekea kuwa na washabiki
  2. Mashindano ya vijana kwa wingi kuwepo na mashindano ya ndani kwa vijana kwa wingi na mashindano hayo yanaweza yakawa yanaendeshwa na chama au chama kihamasishe mawakala na mapromota wa michezo waandae mashindano hayo. Na ili mapromota  waweze kuandaa mashindano hayo inatakiwa chama kiandae mazingira rafiki ambazo zitavutia mapromota kuweza kuandaa mashindano hayo. Kunaweza kukawa na mashindano kama ya Ndondo Cup lakini kwa upande wa Netiboli na yanaweza kufanyika kikanda na wala sio lazima nchi nzima.
  3. Kuanzisha mashindano kwa upande wa wanaume: imefika hatua sasa mchezo huo usionekane kama ni wa wanawake peke yao bali inatakiwa wanaume nao wacheze kwani kwenye mashindano ya kimataifa mchezo huo huchezwa hadi na wanaume kwa hiyo kwa hapa kwetu Tanzania nako kuanzishwe mashindano ya wanaume. Kufanyika huko kutaongeza hamasa katika mchezo huo.
  4. Kubidhaisha wachezaji wakashiriki ligi za kulipwa za netiboli. Kuna mataifa kadhaa kama vile England ambako kuna mashindano ya ligi za kulipwa za netiboli basi Chaneta kitengeneza mazingira rafiki wachezaji wetu waweze kusajiliwa na kwenda kushiriki ligi hizo hata kama huwa ni za mda mfupi. Kufanyika huko kutaongeza hamasa ya watu kushiriki mchezo huo.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Mdhibiti huru wa soka ni nani?

Tanzania Sports

KANUNI ZA KIFEDHA KWENYE SOKA LETU….