in , , ,

Cesc Fabregas ataka kurudi England

*Klabu nne kubwa zamuwania

*David Luiz atahamia PSG?

Kiungo wa Barcelona, Cesc Fabregas anadaiwa kutaka kurudi Ligi Kuu ya England, ambapo klabu nne zipo macho nje kumdaka – Arsena, Chelsea, Manchester City na Manchester United.

Fabregas aliyepata kuwa nahodha wa Arsenal chini ya Arsene Wenger ana wasiwasi kama atapata namba kwenye kikosi cha Barcelona chini ya Kocha Luis Enrique ambaye kwenye mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari hakukanusha uwezekano wa kumuuza.

Baada ya kumfanya Lionel Messi kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi zaidi duniani kwa kumkatia kiasi cha pauni milioni 16.3 kwa mwaka na kutumia dola milioni 74 kumsajili Neymar kiangazi kilichopita, wanahitaji fedha ili kuboresha kikosi kilichochoka.

 Fabregas (27) anatambua kwamba Barca wanamchukulia kama moja ya bidhaa zinazoweza kuingizwa sokoni na baadhi ya washabiki walielekeza shutuma zao kwake jinsi alivyocheza kwenye msimu ambao wametoka bila kikombe hata kimoja.

“Hatujafanya uamuzi wowote, kila kitu kina wakati wake,” ndiyo yalikuwa majibu ya Enrique alipoulizwa juu ya wasiwasi ulioppo kuhusu hatima ya Fabregas hapo Camp Nou.

Arsenal wana nafasi kubwa zaidi ya kumpata Fabregas kwa sababu kuna kifungu cha mkataba walipowauzia Barca mchezaji huyo kinachotaka wajulishwe anapouzwa na watakuwa na kipaumbele cha kumchukua.

Akiamua kuondoka Barca au Barca wakitaka kumuuza, basi Arsenal wanaweza kumpata kwa pauni milioni 25 hivi wakati walimuuza kwa pauni milioni 35 mwaka 2011. Wenger amepata kusema kwamba siku moja Fabregas atacheza tena Arsenal.

Hata hivyo, itakuwa ngumu kupanga kikosi kwenye kiungo, kwa sababu kuna Mesut Ozil, Sanri Cazorla, Aaron Ramsey na Jack Wilshere ambao ni wazuri, ukiachilia mbali majeruhi aliyerudi, Abou Diaby. Fabregas analipwa pauni 100,000 kwa wiki, kiwango ambacho Arsenal wanamudu na wanaweza kumwongezea.

Hata hivyo, Fabregas anaweza pia kwenda Manchester United kama anataka changamoto mpya, na huko Robin van Persie ni rafiki yake mkubwa ambaye kocha Louis van Gaal anaweza kumtumia kumshawishi wakati huu inapoelezwa kwamba kitita kikubwa kitatolewa kujenga upya kikosi cha United.

Barca wanaweza pia kumtoa mchezaji huyo kwa njia ya ubadilishaji na mwingine katika klabu za Man City na Chelsea. Yaya Toure kutikisa kiberiti kunaweza kutumiwa na matajiri wa Falme za Kiarabu kumtoa kwa Barca nao wapewe Fabregas, ili wasitumie fedha nyingi wakati huu wanapoadhibiwa kwa kuzidisha matumizi msimu uliopita. Pia wanaweza kumtoa Fabregas ili wamchukue Sergio Agüero.

Kadhalika Chelsea wanaweza kukubali kulipa kiasi kikubwa cha fedha kama ada au hata kumtoa mchezaji wao, David Luiz ili wabadilishiwe na Fabregas, maana Kocha Jose Mourinho anaelekea kutomhitaji sana Luiz huku Barca wakimtaka.
Zemanta Related Posts Thumbnail

Hata hivyo, kuna habari kwamba Luiz anakwenda Paris Saint Germain kwa ada ya pauni milioni 40 ambazo Chelsea watafurahi kuzipata ili itemize malengo ya kununua wachezaji wengine wazuri, hasa mshambuliaji wa aina ya Diego Costa wa Atletico Madrid au Mario Mandzukic wa Bayern Munich.
davidluizLuiz

Barca walikuwa tayari kumtoa Alex Songa na fedha juu kwa Chelsea ili wampate Luiz, na ikitokea kwamba haendi PSG, basi wanaweza kutumia fursa ya Fabregas kama ‘bidhaa’ mbadala.

Mourinho sasa anafikiria kumnasa kiungo wa Tottenham Hotspur, Paulinho kama mrithi wa muda mrefu ujao wa Frank Lampard, lakini Fabregas anaweza kufaa zaidi hapo. Fabregas anatakiwa pia na klabu nyingine England lakini Pep Guardiola wa Bayern Munich angepata fursa hii hangeipoteza.

Fabragas alijiunga na Arsenal akiwa na umri wa miaka 16 mwaka 2003 akitokea akademia ya Barcelona ya La Masia kabla ya kurudi huko mwaka 2011 na sasa miaka mitatu tu baada anafikiria kuhama.
 

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Usajili Man United bado

Ulaya: Vita ya Real na Atletico Madrid