in

Bado tunamhitaji Chama timu ya Taifa

Juzi timu ya taifa imerusha karata yake ya kwanza katika michuano ya CHAN. Michuano ambayo hushikirisha wachezaji ambao wanacheza ligi ya ndani tu.

Tuachane na matokeo ya jana ambapo Taifa Stars walifungwa goli 2-0. Kuna kitu kimoja ambacho natamani sana tukitazame vyema. Kitu chenyewe ni aina ya uchezaji wa timu yetu ya taifa katika eneo la mbele.

Moja ya kitu ambacho muda mwingi tumekuwa tukilia ni kukosekana kwa washambuliaji ambao wanauwezo mkubwa wa kufunga magoli ambao ni wazawa hasa kwenye timu yetu ya taifa na ligi yetu ya ndani.

Ukitazama kwenye ligi kuu yetu ni John Bocco pekee ambaye amekuwa na mwendelezo mzuri kwenye ligi yetu tofauti na washambuliaji wengine wazawa.

Washambuliaji wengi wazawa huvuma msimu mmoja na hukosa mwendelezo wa wao kuvuma msimu unaofuata. Tuliwahi kumshuhudia Abraham Musa akivuma msimu mmoja tu baada ya hapo hatukumsikia tena.

Misimu miwili nyuma ligi yetu ilimpata Salim Aiyee , alikuwa ni mmoja ya washambuliaji ambao walikuwa kwenye mbio za ufungaji bora wa ligi kuu Tanzania bara. Salim Aiyee na yeye alivuma siku msimu mmoja tu baada ya hapo hatujamsikia tena.

Tatizo la kupata wafungaji wa magoli kwenye ligi kuu yetu ni kubwa . Hatuna washambuliaji ambao wanaweza kuibeba timu katika mwendelezo ule ule.

Tatizo hili la washambuliaji wazawa kutokuwa na mwendelezo mzuri kwenye ligi kuu ya Tanzania linaonekana kuiathiri timu yetu ya taifa kwenye michuano ya CHAN.

Wakati naitazama jana mechi ya Tanzania na Zambia niligundua kitu kimoja, washambuliaji wa Tanzania waliocheza jana Yusuph Mhilu, Ayoub Lyanga na Ditram Nchimbi walikuwa wanakimbia nyuma ya washambuliaji.

Unapokimbia nyuma ya washambuliaji unakuwa unajipa nafasi kubwa ya kutengeneza uwazi eneo la mpinzani. Washambuliaji wanapotengeneza uwazi katika eneo la mpinzani huwa anahitajika kiungo mshambuliaji wa kutumia huo uwazi katika eneo la timu pinzani.

Kwetu sisi hatuna kiungo wa kati ambaye anaweza akatumia uwazi unaotengenezwa katika eneo la mpinzani. Uwazi ambao anaweza kuitumia kufunga magoli au kutengeneza nafasi za kufunga.

Timu yetu na ligi kuu ya Tanzania haina wa kushambulia ambao wanauwezo wa kufunga na kutoa pasi za mwisho. Viungo aina ya Claoutus Chota Chama.

Pamoja na matatizo mengi ambao tunayo, hili ni moja ya tatizo ambalo tunalo kwenye timu yetu ya taifa . Hatuna kiungo ambaye anaweza kuibeba timu kwa kufunga magoli kipindi ambacho washambuliaji wameshindwa kufanya hivo.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Taifa Stars

Taifa Stars, bila Jonas Mkude..

Miraji

Tuachane na kina Morrison tuwekeze kwa kina Miraji Athumani