Kuona vilabu vyote 20 vya Premier League vikicheza moja kwa moja msimu huu..
Soka la England limekuwa kioo cha hisia, migogoro, utambulisho na tofauti za kijamii za kila zama. Baada ya enzi ya dhahabu ya miaka ya 1960, kulifuata kudorora kwa miaka ya 1970 na majanga ya miaka ya 1980, kisha kuja kujiamini upya kwa miaka ya 1990. Karne ya 21 imejaa utandawazi na biashara kupita kiasi. Baada ya msukumo huo mkali na mara nyingi usiojali hatari wa ukuaji usioisha, jamii na mchezo vimejikuta vikikabiliana na hali ya sintofahamu inayoakisi mwaka 2025.
Kuona vilabu vyote 20 vya Premier League vikicheza moja kwa moja msimu huu—nimepata bahati maishani ya kushuhudia mechi nyingi za EPL, moja kwa moja viwanjani hapa England, kuliko mechi zote za timu yangu ya ujana ya Dodoma, CDA, pale Jamuhuri Stadium, na uwanja wa barafu. Pia kwenye TV, na hivyo kukamilisha orodha hiyo Jumanne kwa kushuhudia Arsenal wakiipasua Aston Villa kipindi cha pili—kumekuwa ni somo la hali ya hali ya juu kutokuwa na uhakika. Kuanzia manung’uniko ya mashabiki, tabia za viburi dhaifu za makocha, hadi wachezaji wanaojikokota kwenye dakika 90 za presha isiyokoma, swali moja linajitokeza: je, bado kuna mtu anayefurahia kweli?
Labda Sunderland na hivi karibuni Leeds, kwa kupinga mkondo wa timu zilizopanda daraja kushuka mara moja, wanaweza kusema wanafurahia. Vilabu vinavyosifiwa kuwa “vinaendeshwa vizuri” kama Brighton na Bournemouth vimegonga dari la uwezo wao. Kuanzia kusuasua kwa ujenzi mpya wa Liverpool hadi miradi inayoyumba Manchester United na Chelsea, hadi mzunguko wa maangamizi unaoonekana Molineux, karibu hakuna aliye na furaha siku hizi. Hata katika mwaka wa ajabu wa Crystal Palace wa 2025 kulizuka mgawanyiko wa kusikitisha miongoni mwa mashabiki. Ikiwa kugombana kuhusu nyimbo za “stop the boats” si kielelezo cha nyakati za sasa, basi nini ni tatizo?
Kulipwa ili kuishi na utegemezi wa maisha yote ni baraka kubwa, ingawa kuna changamoto. Urembo wa mchezo umetupwa pembeni katika mbio za ufanisi. Kwa kutumia mbinu zilezile za biashara na teknolojia, soka la kubuni papo hapo limefunikwa na vitabu vya mbinu. Bado kuna sanaa fulani—kutoka ustadi wa kudumu wa Adam Wharton hadi kasi na chenga za Jérémy Doku—lakini ubunifu bila shaka umeathiriwa na takwimu na uchanganuzi.
Uvumi kwamba angalau vilabu viwili huteua vikosi kwa kutumia akili bandia unaonekana kuaminika unapoona soka lililopangwa kupita kiasi na lililofanyiwa mazoezi kupita kiasi. Kuongezeka kwa mabao ya dakika za majeruhi, ambayo yako juu kuliko wakati mwingine wowote, angalau kunaonyesha uchovu wa mwili bado haujadhibitiwa kikamilifu na wataalamu wa takwimu—kwa sasa.
Kupanda kwa umuhimu wa mipira ya adhabu (set pieces) ni dalili iliyo wazi zaidi ya ushawishi wa uchanganuzi. Miaka 15 iliyopita Sir Alex Ferguson alisema kwa mzaha kuwa kona za Charlie Adam, alipokuwa Blackpool, “zilikuwa na thamani ya pauni milioni 10 zenyewe”. Leo zingekuwa na thamani gani? Kuna wanaodhani Antoine Semenyo, anayetajwa kuelekea Manchester City, alivutiwa zaidi kwa sababu ya mipira yake mirefu kuliko sanaa aliyopamba Bournemouth. City ya Pep Guardiola bado inaonesha ubunifu uliobadilisha mchezo, na kwa Rayan Cherki, anafurahia kile kinachoitwa leo mchezaji mbunifu. Lakini Guardiola daima amekuwa akibadilika na nyakati. Erling Haaland, sasa kiongozi aliyekomaa, inasemekeana kuwa ndiye mchezaji anayefaa zaidi dhana ya Premier League ya 2025: nguvu ya mwili ikiendana na uzalishaji wa magoli mengi kupindukia.

Zamani, mipira ya adhabu ilikuwa silaha ya makocha wenye rasilimali ndogo wakicheza pembezoni. Sasa kila mtu anatafuta faida hiyo, na kutokuwa makini katika eneo hili ni maangamizi. Aaron Briggs, aliyeondoka Liverpool wiki hii, amebeba lawama kwa udhaifu wa mipira ya adhabu chini ya Arne Slot—onyo kwa Nicolas Jover na Austin MacPhee kwamba taaluma yao ni mchezo wa namba. Wewe ni mzuri kwa mbinu yako ya mwisho ya mchanganyiko wa ‘zonal’ na ‘man-marking’. Shinda mipira ya pili, jamani.
Uwanjani, mipira mirefu kama mikuki kutoka kwa wachezaji kama Semenyo na Michael Kayode wa Brentford—kwa sasa ni bora zaidi katika eneo hilo—imekuwa kivutio kwa mashabiki waliobaki na makombo. Bao la kwanza la Arsenal dhidi ya Villa kupitia kichwa cha Gabriel Magalhães kutoka kona ya Bukayo Saka lilikuwa faraja. Kuanzia hapo, baada ya kipindi cha kwanza cha wasiwasi, mashabiki na timu waliungana tena huku nguvu ya mapema ya msimu ikirejea.
Kwenye majukwaa ya Premier League, mabadiliko ya mashabiki kutoka kuwa wafuasi hadi wateja yanaendelea. Malalamiko ya “wateja” ni mengi, yakionyesha pia pesa kutotosha kama zamani katika jamii kwa ujumla. Uwanja wa Tottenham Hotspur ulijengwa kama kumbukumbu ya uzoefu wa mteja uliokusudiwa kuendeleza mauzo—ambao wageni wa Kombe la Dunia 2026 watauona—lakini viti vyake vya starehe mara nyingi hubeba hasira kali inayolingana na ghasia zinazoandamana na kudorora kwa Wolves.

Wakati huohuo, taarifa—za kuaminika au la—zinapatikana kwa kubonyeza kitufe, na kusababisha kusawazishwa kwa utamaduni. Makubaliano miongoni mwa mashabiki yanaendelea kupinga vikali VAR, huku waamuzi wenyewe wakibaki kuwa watu wa kulaumiwa, bila kujali kiwango chao. Majina yao hutajwa kwa hasira, taaluma yao kutiliwa shaka baada ya karibu kila uamuzi, haswa wakati wa mipira ya kutupwa. Nyimbo za uwanjani pia hupoteza nguvu haraka.
Ikilinganishwa na zamani, mbali na miguno inayoendelea, mashabiki wengi hutimiza wajibu wao kama mandhari ya bidhaa inayouzwa duniani. Ufahamu wa pamoja bado haujajikusanya hadi kufikia mgomo wa jumla dhidi ya bei za tiketi na vilabu vinavyotumia uaminifu wa mashabiki huku vikivizia wateja wapita njia wanaotumia pesa nyingi kwenye bidhaa. Je, hilo linaweza kutokea? Ikiwa soka la kisasa bado ni kioo cha dunia iliyo nje ya mistari ya uwanja, basi huenda enzi ya maandamano iko karibu.


Comments
Loading…