in , ,

Azam FC na hekaheka, bila wivu kwa Yanga, Simba

Kila msimu Azam Fc wamekuwa na hekaheka nyingi lakini ufanisi wao bado hauridhishi kabisa…

JUHUDI zinazofanya na timu za Nyumbani Tanzania wakati wa usajili huwa zinawavutia wengi. Kati ya wengi hao TANZANIASPORTS imekuwa ikifuatilia na kufanya tathmini ya utendaji wa wachezaji, makocha na viongozi wa vilabu vya Ligi Kuu Tanzania. Kwa misimu kadhaa sasa mabwanyenye wa Chamazi, Klabu ya Azam Fc imekuwa katika hekaheka nyingi. Lakini hekaheka hizo hazijawaletea matunda mazuri kuanzia soka la ndania hadi kimataifa. Bado Azam Fc wana safari ndefu ya kuweka alama katika soka la kimataifa.Β 

Tathmini inaonesha kuwa Azam Fc ni timu inayonunua wachezaji kutoka kila Kona ya Afrika na wanao uwezo wa kuajiri walimu wazuri kwa kila idara. Anzia mtaalamu qa viungo, kocha wa makipa, kocha wa mabeki na kocha mkuu akiwa anaongoza benchi zima kutafuta mafanikio. 

Hata hivyo Azam Fc imepitia vipindi vya tabu. Kwenye mashindano ya kimataifa mara ya mwisho walitolewa kwa idadi ya mabao. Walikosa bao moja tu ambalo lingewapeleka hatua nyingine. 

Kimsingi klabu ya Azam Fc haina mafanikio makubwa kimataifa kama vilabu vikongwe vya Simba na Yanga. Kumekuwa na dhana kuwa timu zilizo nje ya Yanga na Simba kufanyiwa fitina za Kisoka, lakini swali linalokuja inakuwaje fitina hizo zisiwepo kimataifa ambako hawakabonoa? 

Ni muhimu sana kuzingatia kuwa Azam Fc kama klabu wana nyenzo zote muhimu, uwanja wa mazoezi, mishahara minono, vipaji kutoka nje ya Nchi, makocha wenye viwango vya kimataifa na zaidi uongozi ambao umekuwa bega kwa bega na wachezaji na benchi la ufundi lakini hawana alama kimataifa. 

Azam Fc wanayo kila sababu ya kuchambua na kutafakari juu ya hekaheka nyingi wanazofanya kila msimu. Hekaheka ambazo zimekuwa ngumu kuleta matunda mazuri. Usajili wa nyota wakali kama Prince Dube, James Akamiko, Issah Ndala, Kipre Junior na wengineo bado hauonekani kuwaendea vizuri. 

Kwamba kila msimu unapokaribia kuanza unaona klabu inatangaza usajili au mipango kadhaa lakini ndani ya kiwanja inaweza kuwa timu isiyoleta ushindani. Kwao mechi nne tu ndio zenye kuwaonesha wakicheza kwa ushindani. Ni mechi za Azam Fc vs Simba (nyumbani na ugenini) na Azam Fc vs Yanga ) nyumbani na ugenini). 

Mechi hizo unaweza kuona namna Azam Fc wanavyojipanga kukabiliana na vigogo hao kisha wanaweza kuja kukubali kipigo kwa Ihefu ya Mbeya au Namungo ya Lindi. Kufika hapo unaweza kupata tafakari kwamba ni timu inayokamia mechi kubwa tu lakini haiwezi kutoboa mbele vilabu vidogo. 

Makocha bingwa duniani wanaamini timu yoyote inayotaka kuchuka ubingwa inatakiwa kuzibana timu kongwe na ambazo ndizo washindani wao. Kisha inatakiwa kuhakikisha inazichapa timu karibia zote za ndogo kama sehemu ya kukusanya pointi. Sasa ikiwa Azam Fc hata kwa Timu ndogo haitoboi maana yake uwezo wao wa kuhombania ubingwa unakuwa mdogo. Hata linapofika suala la mashindano ya kimataifa unaona Azam Fc hawaonekani kuwa na wivu na kile ambacho Yanga na Simba wanakifanya ndani ya kiwanja. 

Kila msimu Azam Fc wamekuwa na hekaheka nyingi lakini ufanisi wao bado hauridhishi kabisa. 

Ni muhimu kwa viongozi wa klabu hiyo kuangalia sababu za kutofanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa. Ni wakati wa kuzingatia kuwa upo wakati wachezaji wataikimbia kwa sababu itaonekana haina mipango ya kuwaendeleza na kukuza vipaji vyao kupitia mashindano ya Kimataifa. 

Watanzania wanazipenda timu zao, na nina uhakika Azam Fc wakifanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa basi wataungwa mkono na kushangiliwa sana kama zawadi ya mashabiki kwao na matokeo kazi nzuri. Nina imani hata fedha za Rais Samia Suluhu Hassan kwa kila bal watakalofunga zitamiminika kwa klabu hiyo. Itoshe kusema inakuwaje Azam Fc wanakosa fursa ya hamasa ya Rais Samia kwa soka la Kimataifa? Je hekaheka zao zitakuwa na tija gani ikiwa matunda mazuri hayaonekani? Hawajachelewa. Muda ungalipo.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Leandre Willy Essomba Onana

Nyota wapya Simba wana zigo zito

THE PRESIDENT

TFF WANGELETA SUPER LEAGUE YAO