in , , , ,

Arsenal wawafyatua Marseille


*Chelsea hoi kwa Basel, Barcelona wapigwa
*Man U vs Bayer, Man City vs Viktoria leo

 
Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) inaelekea ukingoni ambapo Arsenal wamewafunga Marseille kutoka Ufaransa 2-0 kwenye dimba la Emirates.

Jack Wilshere ndiye alifunga mabao yote katika dakika ya kwanza na ya 65, Mesut Ozil akakosa penati ambayo hata hivyo ilitakiwa irudiwe kwa kuwa kipa wa Marseille, Mandanda, alitoka kabla haijapigwa hivyo kufupisha wigo.

Ushindi wa Arsenal umewaweka katika nafasi nzuri ya kufuzu, lakini itategemea matokeo ya mechi za mwisho.

Washindani wao wakubwa ni Borussia Dortmund wa Ujerumani waliowafunga Napoli kutoka Italia 3-1. Napoli nao pia wana nafasi, kwani wanafungana na Dortmund kwa pointi tisa wakati Arsenal wanazo 12 na mechi zijazo kwa kundi hili ni Dortmund dhidi ya Marseille ambao hawajapata kushinda mechi katika kundi lao huku Napoli wakiwakaribisha Arsenal.

Arsenal walitawala mchezo kwa asilimia 67 na kipa Wojciech Szczesny aliokoa mabao mawili ya wazi na beki wa kushoto kutoka Hispania, Nacho Monreal aliyecheza badala ya Kierran Gibbs akiokoa bao kwenye mstari wa goli.

Katika mechi nyingine, Chelsea walishindwa kupata nafasi ya kwanza kwa kufungwa mechi yao walipocheza ugenini kwa Basel, ambao pia waliwatundika walipocheza Stamford Bridge.
Hata hivyo, Chelsea wamefuzu kwenye kundi lao maana wana pointi tisa wakifuatiwa na Basel wenye nane kisha Schalke wenye saba na Steua Bucharest tatu.

Ajax walishangaza kwa kuwapiga mabao 2-1 Barcelona, lakini Barca tayari wamefuzu kwa hatua inayofuata. Celtic wakicheza nyumbani Uskochi walipigwa na Milan 3-0.

Steua Bucharest walitoka suluhu na Schalke, Zenit St Petersburg wakaenda sare ya 1-1 na Atletico Madrid lakini wana Madrid hao wamefuzu kwa awamu ijayo.

Porto nao wakicheza nyumbani wamekwenda sare ya 1-1 na FK Austria Vienna.
Jumatano hii Manchester United wanaalikwa na Bayer Leverkusen kwenye mechi muhimu wakati Shakhtar Donets wakicheza na Real Sociedad. Man U wanaongoza kundi kwa tofauti ya pointi moja wakifuatiwa na Bayer huku Shakhtar wakiwa na pointi tano na Real wanayo moja.

Manchester City watawakaribisha Viktoria Plzen, Juventus watacheza na FC Copenhagen, Real Madrid na Galatasaray, PSG na Olympiacos, RSC Anderlecht dhidi ya Benfica na CSKA Moscow wakiwakaribisha Bayern Munich.

Bayern wanaongoza kundi lao kwa pointi 12 wakifuatiwa na Man City wenye tisa, CSKA Moscow tatu na Viktoria hawana chochote.
 

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Bendtner wa Arsenal matatani tena

Ndege ya Man U yatua kwa tabu Ujerumani