in , , ,

Bendtner wa Arsenal matatani tena


*Avunja kitasa cha nyumba anakokaa
*Alipata kulimwa faini ya Euro 100,000

Ni kama sikio la kufa lisilosikia dawa, mshambuliaji wa kati wa Arsenal, Nicklas Bendtner ameingia matatani kwa kosa la jinai la kuharibu mlango.
Bendtner, mchezaji wa kimataifa wa Denmark alidakwa na polisi, akajulishwa makosa yake na kupewa onyo baada ya kupiga na kuharibu mlango kwenye kotaz anazokaa Hertfordshire.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 25 alikamatwa usiku wa kuamkia Jumanne hii katika eneo la Bushey anakoishi baada ya kufanya fujo hiyo.

Ameomba radhi kwenye mtandao wake wa Instagram akidai kwamba aliharibu mlango alipokuwa akijaribu kuufungua.
Bendtner anadai kwamba baada ya ushindi wao dhidi ya Southampton Jumamosi walikuwa na mtoko kwa ajili ya kupata chakula cha usiku yeye na familia na marafiki na baadaye usiku huo huo akajisikia kuogelea kwa hiyo akaenda gym kufanya hivyo.

Hata hivyo anasema hakufanya makusudi kuvunja mlango kwa sababu kidude cha ufunguo kwenye mlango kilibadilika rangi na kuwa kijani kuashiria mlango uko wazi badala ya nyekundu kwamba umefungwa, hivyo waliamua kutumia nguvu ndipo wakavunja.
Amewaomba radhi majirani kwa usumbufu aliowasababishia kwa kelele za usiku huo na kwamba amelipa gharama za hasara aliyosababisha na wameshamalizana na polisi pia.

Kwa onyo alilopewa, inamaanisha Bendtner hatafikishwa mahakamani lakini itabidi awe makini siku zijazo na Msemaji wa Arsenal ameonya kwamba wanatarajia nidhamu ndani na nje ya dimba na wamemjulisha hivyo mchezaji huyo ambaye kwa muda sasa amekuwa akililia kuhama kwa kukosa namba.

Mshambuliaji huyo amefunga mabao 45 tangu ajiunge na Arsenal msimu wa 2005/6
Juni mwaka jana, Bendtner alilimwa faini ya Euro 100,000 na Shirikisho la Soka la Ulaya (Uefa) kwa kitendo chake cha kushusha bukta uwanjani kuonesha chupi iliyokuwa ikitangaza kampuni ya Paddy Power.

20131126-150525.jpg

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

KILIMANJARO STARS YATUA SALAMA NAIROBI

Arsenal wawafyatua Marseille