in , , ,

Arsenal waka waka

Arsenal wametwaa ubingwa wa Kombe la FA kwa kuweka rekodi kubwa zaidi England, kwani ndio wametwaa mara nyingi zaidi.
Walitwaa ubingwa huo baada ya kuwanyuka Aston Villa 4-0 katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Wembley, likiwa ni kombe lao la 12 katika michuano hiii.

Arsenal walitawala mchezo na washabiki wao hawakuwa na shaka hata kidogo, lakini iliwachukua hadi dakika tano kabla ya mapumziko kupata bao la kwanza kwa bao la Theo Walcott.

Bao la pili lilitiwa kimiani na Alexis Sanchez, la tatu na naibu nahodha Per Mertesacker na la mwisho likatokana na mpachika mabao wao, Olivier Giroud.

Villa ambao walimaliza ligi kuu wakiwa nafasi moja tu juu ya walishuka daraja walicheza hawakuweza kuwamuud Arsenal katika mechi ambayo ilikuwa na watazamaji 89,283 ikichezeshwa na Jonatham Moss walirejea Uwanja wa Wembley katika fainali ya Kombe la FA kwa mwaka wa pili mfululizo.

Aaron Ramsey

Msimu uliopita waliibuka kidedea kwa kuwafunga Hull 3-2 katika mechi ambayo vijana wa Arsene Wenger walianza kulala 2-0 kabla ya kuzinduka.

Arsenal wamekuwa timu ya kwanza kutetea kombe hilo kwa mara ya kwanza tangu Chelsea walipofanya hivyo 2010.

Kocha mpya wa Villa, Tim Sherwood aliyewawezesha vijana wake kubaki Ligi Kuu, japokuwa walimaliza nafasi moja tu juu ya zile zilizoshuka daraja, alikuwa ameipania mechi hiyo.

Mara ya mwisho kwa Villa kuwafunga Arsenal kwenye michuano hii ilikuwa 1974 ambapo walikwenda 1-1 Highbury na katika mechi ya marudiano Villa walishinda 2-0 dimbani Villa Park.

Villa wameshinda mechi moja tu kati ya tisa zilizopita dhidi ya Arsenal kwenye mashindano yote, nayo ilikuwa mechi ya ufunguzi wa ligi Agosti 2013 walipowapiga Arsenal 3-1 dimbani Emirates.

Arsenal wanaoshikilia kombe hilo ndio waliofanikiwa zaidi katika historia ya Kombe la FA, wakiwa wamelitwaa mara 12, mara moja zaidi ya Manchester United.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

TETESI ZA USAJILI LEO

Blatter kung’oka Fifa