in , , , ,

Arsenal wajivuruga UCL

*Liverpool chuma lakini wapigwa

Arsenal wameshindwa kujihakikishia kuingia hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) baada ya kuvuruga matokeo ya hadi dakika 60 walipokuwa mbele kwa 3-0 na kuishia sare ya 3-3 dhidi ya Anderlecht.

The Gunners wamerudia mambo ya 2011 walipokuwa mbele kwa mabao hayo dhidi ya Newcastle, lakini wakaja kuishia sare ya 4-4. Mbele ya maelfu ya washabiki wao, wachezaji na makocha walisikitika baada ya mechi kana kwamba walikuwa wamefungwa.

Sasa Arsenal wanahitaji pointi moja katika mechi zao mbili zilizobaki ili wafuzu kuingia hatua hiyo. Penati ya nahodha Mikel Arteta iliyotokana na Chancel Mbemba kumchezea rafu
Danny Welbeck iliwaweka Arsenal mbele kabla ya Alexis Sanchez kupachika bao zuri kutoka umbali wa yadi 20 na Alex Oxlade-Chamberlain kuweka la tatu.

Hata hivyo Anthony Vanden Borre aliwapunguza kasi Arsenal kwa mabao mawili, la kwanza japo alikuwa ameotea likakubalika, kabla ya Aleksandar Mitrovic kusawazisha katika dakika ya mwisho na kuwaacha Arsenal wakiduwaa. Arsenal sasa wameruhusu mabao saba katika mechi nne zilizopita za UCL.

Vijana wa Arsene Wenger watakutana na Borussia Dortmund Novemba 26 jijini London kabla ya kucheza na Galatasaray Desemba 9 kujua hatima yao. Dortmund wanaongoza kundi kwa tofauti ya pointi tano na tayari wamefuzu kwa hatua inayofuata.
 
LIVERPOOL WAGANGAMALA LAKINI WAPIGWA

Soccer - UEFA Champions League - Group B - Real Madrid v Liverpool - Santiago Bernabeu

Liverpool waliosafiri hadi Madrid wakiwa na hofu ya kupokea kichapo kizito, walicheza vyema na kukubali bao moja tu lililofungwa na Karim Benzema katika dakika ya 27 na Real tayari wamefuzu kwa hatua ya timu 16.

Kocha Brendan Rodgers alifanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi chake kilichofanya vibaya katika mechi kadhaa zilizopita, ambapo nahodha Steven Gerrard, winga chipukizi Raheem Sterling, Jordan Henderson na Mario Balotelli walianzia benchi, huku Kolo Toure akitumiwa na kucheza vyema kwenye ulinzi.
 
MATOKEO MENGINE YA UCL
 
Katika mechi nyinginezo, Juventus walifanikiwa kuwashinda Olympiakos 3-2, Malmo FF wakazidiwa na Atletico Madrid 0-2, FC Basel wakawakandika Ludo Razgd 4-0, Zenit Saint Pettersbug wakafungwa 2-1 na Bayer Leverkusen, Benfica wakawalaza Monaco 1-0 na Dortmund wakawafagilia mbali Galatasaray 4-1.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Liverpool waliwazidi Arsenal kwa Sanchez lakini …

Mjadala wa Liverpool kuacha vigogo nje