in , , ,

Arsenal kwa raha zao wanapeta

ZAMA huja na kupita, na kwa Arsenal, hakika wamekuwa na wakati mzuri, baada ya kuachana na kocha Arsene Wenger na kumwingiza Unai Emery.

Japo alianza kwa kuchechemea na kufungwa mechi mbili za kwanza kwenye Ligi Kuu ya England (EPL), sasa Arsenal wamethibitisha kwamba ni wagumu, wakicheza kwa kushambulia na kurejesha imani ya washabiki wao.

Wamefikisha mechi 19 bila kupoteza mchezo, lakini la muhimu zaidi ni ushindi wao dhidi ya mahasimu wa London Kaskazini – Tottenham Hotspur, wakiwapiga 4-2 na kupanda nafasi ya nne na kuwashusha Spurs hadi ya tano.

Ilikuwa mechi muhimu sana, na wadau wa soka waliona hilo kama jaribio kubwa mno kwa Mhispania Emery, lakini alienedelea na mbinu zake za kucheza kutoka nyuma na kushambulia bila kuchoka.

Mmoja wa wachezaji wanaoonekana kuwa kiboko ni Pierre-Emerick Aubameyang ambaye moto wake hauzimiki na kujituma kwake kunaongezeka kila mara, akiwa sasa amefunga mabao 10 akiiongoza safu ya ushambuliaji ya Arsenal na alifunga pia kwenye mechi hiyo muhimu ya watani wa jadi ambapo Spurs walikuwa wakipewa nafasi zaidi ya kushinda.

Alikuwa mchezaji mahiri sana kwenye mechi hiyo, sawa kama alivyokuwa kiungo Lucas Toreira, ambapo sasa ile Arsenal ya akina Patrick Vieira inaonekana kurejea na makali yake, baada ya misimu miwili ya hovyo chini ya Wenger.

Kwa mwendo wao sasa Arsenal ni wa nne, wakiwa nyuma ya Manchester City wanaoongoza ligi kwa tofauti ya alama nane, kwani Man City wanazo alama 38, Liverpool 36 na Chelsea 31. Ni Chelsea hawa waliowafunga Spurs kwenye mechi iliyotangulia.

Spurs wao wana alama 30 pia, lakini uwiano mbovu wa mabao kulinganisha na Arsenal wakati nafasi ya sita wakiwa Everton na Manchester United wa Jose Mourinho wakishika nafasi ya saba kwa alama 22 tu.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Arsenal: Mwamko wao si wa uongo

Tanzania Sports

Arsenal wamewapa somo kubwa Manchester United!