in , , ,

Arsenal hali mbaya

 
Arsenal wamepigwa mabao 5-1 kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) nchini Ujerumani.

Walipata kipigo hicho ikiwa ni majibu ya Bayern Munich ambao walifungwa 2-0 na Arsenal katika uwanja wa Emirates jijini London.

Kipigo hicho kinawaelekeza Arsenal kutoka kutupwa nje katika hatua ya makundi, kwani tayari wamepoteza mechi tatu kati ya nne walizocheza.

Arsenal walikuwa na wakati mgumu katika kipindi cha kwanza, ambapo mabao ya Robert Lewandowski, Thomas Muller na David Alaba yalitosha kuwapeleka mapumziko wakiwa nyuma kwa mabao matatu.

Arjen Robben alitokea na kufunga kipindi cha pili kabla ya Olivier Giroud wa Arsenal kufnga moja, lakini Muller tena akapigilia msumari wa mwisho alipotia bao la tano

Bayern na Olympiakos na sasa wamebakiwa na mechi mbili, hivyo kwamba kufuzu kwa hatua ya mtoano sasa itategemea fadhila za timu nyingine.

Katika mechi nyingine ya kundi hilo, Olympiakos waliwafunga Dinamo Zagreb 2-1, bao la ushindi likipatikana dakika ya 90. Zingetoka sare ingekuwa nafuu kwa Arsenal kufuzu.

Arsenal watajilaumu wenyewe kwa kuanza hovyo michuano hiyo kwa kufungwa na Zagreb na pia Olympiakos ambao wanasubiri kurudiana kwenye mechi mbili hizo. Arsenal wasipovuka itakuwa mara ya kwanza katika miaka 13.

Arsenal walikataliwa bao la Mesut Ozil la kusawazisha, ikielezwa kwamba mkono ulitumika. Walicheza bila beki wao mahiri wa kati, Laurent Koscielny mwenye majeraha ya paja, kufikisha idadi ya majeruhi 10 kwa klabu hiyo ya London Kaskazini.

CHELSEA WAWAPIGA KIEV

Chelsea walitakata jana
Chelsea walitakata jana

Katika matokeo mengine, Chelsea walimpunguzia shinikizo kocha Jose Mourinho kwa kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Dynamo Kiev.

Katika mechi iliyofanyika Stamford Bridge, washabiki walimshangilia kocha huyo kwa kulitaja jina lake, naye akawa anatabasamu.

Kiev walianza vibaya kwa kujifunga kupitia kwa Aleksandar Dragovic lakini alisawazisha makosa kwa kufunga bao la kusawazisha kutokana na kosa la kipa Asmir Begovic dakika 13 kabla ya mechi kumalizika.

Chelsea walipata bao la pili kupitia kwa Willian dakika saba kabla ya mechi kumalizika, akipiga mkwaju wa adhabu ndogo kutoka umbali wa yadi 25.

Ushindi huo unawaweka Chelsea katika nafasi ya pili kwenye kundi lao, pointi tatu nyuma ya vinara Porto na pointi mbili zaidi ya Kiev. Maccabi Tel Aviv hadi sasa hawana pointi na wameshatolewa.
MATOKEO MENGINE UCL

Screen Shot 2015-11-05 at 07.48.50
Katika matokeo mengine, Barcelona waliwafunga BATE Bor 3-0, Roma wakawashinda Bayer Leverkusen 3-2, KAA Gent wakawapiga Valencia 1-0 na Lyon wakapoteza kwa Zenit Saint Petersburg kwa 2-0.

Kutokana na matokeo hayo, kila timu ikiwa imebakisha mechi mbili kwa makundi yote, Real Madrid wanaongoza kundi A wakifuatiwa na Paris Saint-Germain.

Kundi B vinara ni Manchester United na PSV Eindhoven, kundi C ni Benfica na Atletico madridm wakati D ni Manchester City na Juventus.

Katika kundi E wanaoongoza ni Barcelona wakifuatiwa na Roma. Kundi F walio juu ni Bayern Munich na Olympiakos, kundi G ni Porto na Chelsea wakati kundi H vinara kwa mbali ni Zenit Saint Petersburg wakifuatiwa na Valencia.

Advertisement
Advertisement

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

BAYERN v. ARSENAL

Tanzania Sports

HAYA NDIYO MATATIZO YA CHELSEA