in

Arsenal, Chelsea safi

Arteta na Lampard

Historia inaandikwa tena, na mwezi ujao Arsenal watacheza fainali ya Kombe la FA dhidi ya mahasimu wao wa London – Chelsea.

Arsenal wanashikilia rekodi ya kucheza fainali nyingi zaidi, na mwaka huu wamevuka vigingi licha ya kutokuwa vyema kwenye Ligi Kuu ya England (EPL), wakiwakalisha Manchester City 2-0 kwenye nusu fainali uwanjani Wembley.

Wakiwa chini ya kocha wao Mhispaniola, kiungo na nahodha wao wa zamani, Mikel Arteta, Arsenal walionesha mchezo wa kiwango cha juu sana, Arteta akimzidi maarifa mtu aliyemfunda katika ukocha – Pep Guardiola, na kuonesha upungufu wa wacheezaji wake na kikosi kwa ujumla.

Chelsea wao wamevuka baada ya kuwakandamiza Manchester United kwa 3-1 kwenye mechi ambayo Man U wanaofundishwa na mchezaji wao na kiungo wa zamani, Ole Gunnar Soslkjaer walionesha udhaifu tangu mwanzo, golikipa wao, David de Gea akifanya makosa makubwa na nahodha wao na beki ghali wa kati, Harry Maguire akijifunga.

Chelsea pia wanafundishwa na kiungo wao wa zamani, Frank Lampard na walihakikisha kwamba Mashetani Wekundu hawachomoki, wakawavurugia mserereko wao wa kutopoteza mechi kwa muda mrefu. Walikuwa wamekwenda mechi 19 bila kupoteza katika mashindano yote, wakitaka ushindi kwenye nusu fainali hiyo ili wafikie 20 na kujipa kujiamini zaidi lakini haikuwa.

Tanzania Sports
Arteta na Nahodha wake

Mabao ya Arsenal yalifungwa na nahodha wao anayesusua kusaini mkataba mpya, Mbenini Pierre-Emerick Aubameyang baada ya timu kuonesha ushirikiano mkubwa. Imekuwa wiki njema hasa kwa Arteta ambaye alitoka kuwafunga Liverpool 2-1 kwenye EPL na kutia ‘mchanga pilau’ la ubingwa wa Kops hao.

Arteta aliingia Emirates Desemba mwaka jana, akichukua nafasi ya Mhispania mwenzake, Unai Emery aliyeshindwa kuwarudisha Washika Bunduki wa London juu baada ya kuondoka kwa Arsene Wenger aliyedumu na klabu tangu 1996.

Itakuwa Agosti mosi Arsenal watakapokabiliana na Chelsea kwenye Uwanja wa Taifa – Wembley, wakati Man United na kocha wao wakitafakari iwapo umefika wakati wa kumbadili de Ge ana kipa mwingine. Makosa aliyofanya kwenye mechi ya nusu fainali alifanya pia dhidi ya Tottenham Hotspur mwezi uliopita na kutoka 1-1 wakiwa bado kwenye changamoto ya kufuzu kwa UCL msimu ujao.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

72 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Giroud

Mechi hizi za ‘kuwachinja’ Lampard na Solskjaer

Tanzania Sports

Makocha wetu hawana nafasi ya kudhaminiwa kusoma nje?