in , , ,

Mertesacker na moto mpya Arsenal

*Ferguson alimwa faini kwa utovu wa nidhamu

*David Beckham aanguka akipiga penati China

 

Beki wa kati wa Arsenal, Mjerumani Per Mertesacker anaibukia kuwa kiongozi mzuri Arsenal, akiwarejesha pamoja wachezaji katika wakati huu mgumu.

Mertesacker aliyekabidhiwa mikoba kwenye mechi ya Arsenal dhidi ya Bayern Munich na ile dhidi ya Swansea, ameonesha kiwango cha juu.

Mertesacker (28) ni tunda la timu ya vijana ya Hannover 96, alisajiliwa 2011 kutoka Werder Bremen na sasa alikuwa akihusishwa na kurejea Bundesliga kujiunga na Wolfsburg.

Hata hivyo, Mertesacker aliyeongoza vyema beki yake kutoruhusu bao hata moja kwenye mechi mbili hizo muhimu, anasema haendi popote, na anataka kuiimarisha Arsenal.

“Kocha wetu Arsene Wenger ana imani kubwa nami, na sasa sina ninachofikiria zaidi ya kuitumikia Arsenal,” anasema beki huyo mrefu, mwenye nguvu lakini mkimya.

Mertesacker anasema tangu walipofungwa 2-1 na Tottenham Hotspurs, wamechukua hatua kama mabeki, kujitazama upya, kuangalia mikanda ya mechi na kuangalia panapotakiwa kurekebishwa.

Katika kuwekana kitimoto na kupangana upya, Mertesacker ndiye ametokea kuwa mzungumzaji mkuu, isivyo kawaida, na ameanza kuwapanga wenzake na kujituma kwa nguvu uwanjani.

Alifanya hivyo Ujerumani, kisha Swansea na pia Ijumaa kwenye mechi ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Kazakhstan, ambapo pia Ujerumani walishinda mabao 3-0.

Mertesacker alisajiliwa katika dakika za mwisho za usajili mwaka juzi, na uzoefu wake katika mechi za kimataifa unaeekea kumpa nafasi hata zaidi ya nahodha, Thomas Vermaelen aliyepigwa benchi mechi mbili mfululizo.

300px-Arsenal_end_of_2008-09_season_walkabout

Anaonekana kucheza vyema na kuipa timu mafanikio akiwa na Mfaransa Laurent Koscienly, ambapo kuwekwa benchi kwa kipa Wojciech Szczesny na kurejeshwa Lukasz Fabianski pia kumelipa.

“Kwa kweli tulijihisi vibaya sana baada ya mechi ya Tottenham, tukaona tulistahili kufanya jitihada zaidi, kwa hiyo kila mmoja wetu alishirikishwa na sote tukaona tunatakiwa kuboresha uchezaji na kubadilishana mawazo.

“Sasa tunajiona kama kitu kimoja na tunatakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa ili kuitoa timu hapa ilipo na kuipa mafanikio, tumeanza uwanjani na mafanikio yanaonekana,” anasema Mertecacker.

Mjerumani huyo amenukuliwa akisema angependa kucheza kwa muda mrefu Emirates, kwa sababu ameanza kupata mrejesho mzuri kutoka kwa kocha wake.

Anasema ni hivyo hata kwao Ujerumani, ambapo wanamtaka aende haraka iwezekanavyo kujiunga Bundesliga, lakini hana mpango huo, lakini anachukulia Wajerumani wenzake wanampenda.

Ferguson apigwa faini ya pauni 8,500

photot

Katika tukio jingine, Kocha wa Manchester United, Alex Ferguson amepigwa faini ya pauni 8,500 kwa utovu wake wa nidhamu baada ya mechi dhidi ya Real Madrid iliyofanyika Old Trafford mapema mwezi huu.

Ferguson aliyekasirishwa na mwamuzi wa mechi hiyo kumpa kadi nyekundu Nani, alikacha kuzungumza na wanahabari baada ya mechi hiyo, wakati ni moja ya taratibu za kila mechi kwa makocha.

Nani kwa upande wake amefungiwa mechi moja, kutokana na kadi nyekundu aliyopewa kwenye mechi ambayo United walitupwa nje ya Kombe la Mabingwa Ulaya baada ya kulala 2-1.

Beckham aanguka akipiga penati

Nyota wa soka wa Uingereza, David Beckham ametelezana kuanguka chini wakati akiwaonesha vijana jinsi ya kupiga penati nchini China.

Beckham aliyepewa heshima ya ubalozi ili kukuza michezo China, alikuwa nchini humo kutekeleza jukumu hilo, lakini katika wakati muhimu, aliishia kuanguka kwa nyuma hadi kulala chini.

Wachina waliishia kucheka, lakini ni wazi nyota huyo mwenye umri wa miaka 37 alidhalilika, hasa kutokana na ufanisi wake wa kupiga na hata kufunga mipira ya adhabu.

 

 

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Rio Ferdinand amejimaliza

Tanzania yatikisa Kombe la Dunia