in , ,

Zlatan Muacheni ajifananishe na mvinyo

Kama nitapewa nafasi ya kutaja wanadamu wanaojiamini sana katika hii dunia kamwe sitaacha kumtaja mshambuliaji wa zamani wa Sweden na Man United anayekipiga katika klabu ya LA Galaxy kwa sasa inayoshiriki Ligi Kuu Marekani (MLS), Zlatan Ibrahimovic sijui kujiamini kwake kunatokana na nini hasa? Uwezo wake uwanjani ndio unamfanya ajiamini ndani na nje ya uwanja?

Bado nakosa jibu la moja kwa moja la kuweza kufahamu kujiamini sana kwa Zlatan Ibrahimovic kunatokana na nini, inawezekana maisha yake ya utukutu na utundu aliyokulia kwao Malmo Sweden akiwa katika maisha duni ndio yanayomfanya kujiamini wakati wote au kucheza kwake Taekwondo, sina jibu la moja kwa moja bado zaidi ya kukisia tu.

Zlatan bado anaendelea kuidhihirishia dunia kuwa uwezo wake wa kutoa kauli za kishujaa na kujisifia haujaishia mdomoni tu bali anathibitisha uwanjani, Zlatan aliwahi kunukuliwa akisema yeye ni kama ‘Red Wine’ kadri inavyozidi kukaa ndio inavyozidi kuwa kali zaidi, hivyo yeye kadri umri wake unavyozidi kuongezeka ndio anavyozidi kuwa bora zaidi uwanjani.

Unapata wapi ujasiri wa kumkosoa Zlatan kwa kauli hiyo wakati anafunga kila leo, tukiwa bado tunaamini anahitaji kuizoea Ligi Kuu Marekani akiwa na LA Galaxy msimu wa kwanza, anafunga hat-trick yake ya kwanza katika mchezo muhimu dhidi ya Orlando City July 29 2018 uliyomalizika kwa LA Galaxy kupata ushindi wa magoli 4-3, tukiwa bado tunaamini anahitaji kuizoea Ligi, hat-trick yake hiyo aliyoifunga dhidi ya Orlando City inamfanya afikishe jumla ya magoli 15 MLS akiwa amecheza game 17 pekee tofauti ya magoli 9 na mfungaji bora wa msimu ulioisha wa MLS David Villa wa New York City akiwa kaibuka mfungaji bora kwa kufunga magoli 24 katika mechi 33.

Zlatan anatudhihirishia kuwa yeye ni bora na kauli yake ya kujifananisha na mvinyo hajakosea ni baada ya kuweza kufunga magoli 15 katika Ligi ngeni kwake, akiwa katika kipindi kigumu katika maisha yake ya soka kwa mchezaji mwenye umri wa miaka 35 wakati huo, kupata jeraha la goti na kukaa nje kwa miezi takribani saba na bado akarudi uwanjani katika Ligi ngeni akiwa na umri wa miaka 36 na kufunga magoli 15.

Wengi tuliamini Zlatan baada ya kupata jeraha la goti (knee Ligament injury) April 20 2017 katika mchezo wa robo fainali ya Europa League wa Man United dhidi ya Anderletch ya Ubelgji katika dimba la Old Trafford na kushindwa kumaliza mchezo na kutolewaa nje dakika ya 92 na nafasi yake kuchukuliwa na Anthony Martial mchezo ukienda dakika 30 za nyongeza, Zlatan baada ya siku kadhaa alifanyiwa upasuaji wa goti lake la kulia na wengi kuamini inawezekana jeraha hilo likamaliza maisha yake ya soka kama ilivyokuwa kwa mshambuliaji wa Chelsea (1998-2000) Pierluigi Casiraghi aliyestafishwa na jeraha la goti (Knee ligament injury) mwaka 1998 akiwa na umri wa miaka 28 akiwa kaichezea Chelsea game 10 pekee, japokuwa alitangaza rasmi kustaafu 2002 lakini game yake ya mwisho alicheza akiwa na miaka 28 baada ya hapo alikuwa akifanyiwa upasuaji wa mara kwa mara.

Sitashangaa ikitokea Zlatan akawa mfungaji bora MLS mwaka 2018 kwa kasi anayokwenda nayo, sishangai kwa sasa kumuona namba mbili kwa wanaoongoza kwa ufungaji wa magoli MLS akiwa na magoli 15 nyuma ya Josef Martínez wa Atalanta FC anayeongoza kwa kuwa na magoli 24 akiwa kacheza mechi 23 hadi sasa, Zlatan ni mshindi kwa sababu amefanikiwa kupambana na vita ya jeraha la goti ambalo ingeweza kukatisha maisha yake ya soka kama ilivyokuwa kwa Casiraghi, hivyo tumuache Zlatan aendeleze tambo zake za kujiita majina tofauti tofauti kama Simba, Mungu wa Manchester, Mungu wa LA na ‘Red Wine’.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

HARRY MAGUIRE, ILIOKUWA SILAHA YA SIRI ENGLAND

Tanzania Sports

SIMBA HAIJUI CHA KUFANYA SIMBA DAY, YANGA IKO USINGIZINI