WIMBI la makocha wapya kuingia kwenye tasnia hiyo limezidi kubamba sehemu mbalimbali duniani. Kuna aina tatu za makocha hadi sasa; wapo makocha ambao waliingia kwenye kazi hiyo baada ya kustaafu kucheza soka kwa mafanikio makubwa, pili wapo makocha ambao wameingia kazi hiyo bila kucheza soka, na tatu wapo makocha ambao walilazimika kuachana na mchezo wa soka mapema sana na wakiwa hawana mafanikio yoyote kutokana na sababu za kiafya.
Katika makundi yote hayo wapo Pep Guardiola, Carlo Ancelotti, Rafa Benitez, Jose Mourinho, Rube Amorim, Nuri Sahin, Vincent Kompany, Xavi Alonso na wengineo akiwemo kocha wa Ipswich Town. Makocha ambao hawakucheza soka wanawakilishwa na Jose Mourinho na Andre Villa-Boas na wale waliocheza soka kwa mafanikio wanawakilishwa na Ancelotti, Didier Deschamps na Zinedine Zidane. Hata hivyo jina moja ambalo linagonga vichwa vya wasomi, wadau na wataalamu wa soka ni nadharia ya ukocha aliyonayo Zinedine Zidane.
Kocha huyo alijitokeza kwa mara ya kwanza akiwa msaidizi wa Carlo Ancelotti ambapo mwaka 2014 walifanikiwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya likiwa ni taji la kumi kwa Real Madrid maarufu kama La Decima. Baada ya kutwaa taji hilo Zidane alipekwa kukinoa kikosi cha vijana cha Real Madrid, Castilla. Ujio wa kocha Rafa Benitez ulichangia Zidane kuondoka kwneye nafasi ya usaidizi hivyo kwenda kuwanoa vijana. Lakini Benitez hakudumu kikosi baada ya miezi kadhaa alifukuzwa na nafasi yake akapewa Zinedine Zidane.
Tangu alipokabidhiwa jukumu hilo Zidane alitwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mara tatu mfululizo kuanzia mwaka 2016 hadi 2018, kisha ajizulu nagasi yake. Katika hali isiyotarajiwa wengi walishtushwa na uamuzi ule. Lakini miezi kadhaa baadaye alirudi kikosi mwaka 2019 na kuondoka mwaka 2021. Tangu mwaka 2021 Zidane amekaa pembeni katika ukocha. Timu mbalimbali zimekuwa zikipiga simu kuomba huduma yake, lakini majibu yake yamekuwa yenye maneno tatu tu; “Hapana, asante sana”. Juventus walijaribu wameshindwa. Manchester United wlaijaribu bila mafanikio. Bayern Munich walipiga hodi lakini nao walikataliwa. Wadhani wa Zidane wanadai kuwa kocha huyo huwa anaweza kusikilzia simu za viongozi wa sehemu mbili pekee; Timu ya Taifa ya Ufaransa na klabu ya Real Madrid.
Katika nadharia za uongozi Zidane anabaki kuwa mwajiriwa wa aina yake ambaye ana nguvu katika kuamua wapi hatafanya kazi na wapi atafanya kazi. Kila taasisi zenye nguvu zinapojaribu kumtaka kocha huyo amekuwa akikataa. Zidane amefanikiwa kutwaa mataji sio hayo matatu ya Ligi ya Mbaingwa Pekee bali hata mengine kama vile La Liga (mara mbili, 2017, 2021), mataji mawili ya Super Cup, mataji mawili ya Super Cup ya EUFA na mataji mawili ya klabu bingwa dunia.
Kimsingi ana wasifu mkubwa kuwashinda baadhi ya makocha waliopo leo kwenye vilabu mbalimbali,. Kwa mfano Zidane ana wasifu mkubwa kuwazidi Dider Deschamps(Ufaransa), Ruben Amorim (Manchester United), Arne Slots(Liverpool),Vienent Kompany(Bayern Munich),Simeone Inzaghi (Inter Milan), Mikel Arteta (Arsenal), Luis Enrique (PSG), Enzo Moresca(Chelsea) hata Hans Flicks (Barcelona) hata hivyo mfaransa huyo amekataa vibarua vingi vinavyomjia.
Simu zote za vibopa mbalimbali zimejaribu bila mafanikio. Vilabu kutoka sehemu nyingi kuanzia Italia hadi Ujerumani, England hadi Ufaransa, Italia hadi Marekani lakini Zinedine Zidane amekataa of azote hizo. Amekuwa kocha wa aina yake ambaye viongozi na wadau wa soka wanazidi kuumiza kichwa kwanini mwalimu huyo amekuwa nje na mwenye sifa zote anakataa fursa nyingi za kuinoa timu?
Ingelikuwa kocha mgeni tungelisema labda anaohofia, lakini Zidane ana sifa kubwa kuwazidi wachezaji wote anaowafundisha. Kwanza mwenyewe amekuwa bingwa wa dunia, amekuwa mchezaji bora wa Ulaya na dunia, anazo rekodi nyingi kwenye mchezo wa soka kuliko wachezaji ambao angepewa kuwoangoza. Kimsingi wachezaji wenyewe wanaweza kujiuliza ni jambo wangeweza kumtambia Zidane na wakaona lina maana? Kifupi hakuna. Lakini Zidane amekuwa kuwa kocha wa aina yake, kwani suala la ajira limemfuatua kwa wengi l;akini mwenyewe hataki kabisa kuchukua fursa hizo. Pengine ndiye kocha ambaye bado ana mvuto mbele ya vyombo vya habari na wachezaji pamoja na wadau kutokana na staili zake za maisha. Mvuto ameutengeneza kwa kuwa mtu yaani kama wasemavyo vijana wa mjini “amekuwa keki” na hivyo thamani yake imepanda maradafu. Ni mtu wa aina yake.
Comments
Loading…