in , , ,

Yanga, Simba, Kusuka au Kunyoa, Jumapili, 20/10/2013.

WATANI wa jadi katika Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara, Simba na Yanga zinatarajia kukutana katika Jumapili Oktoba 20 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ikiwa ni mchezo wa kwanza msimu huu wa mwaka 2013/ 20014.

Hata hivyo kwa mwaka huu timu hizo zitakuwa zinakutana kwa mara ya pili baada ya Aprili kukutana katika mchezo wa funga dimba katika msimu uliopita ambapo Yanga ilishinda magoli 2-0 huku ikiwa tayari imeshatwaa ubingwa.

Timu hizo mbili zenye mashabiki wengi, ndani na nje ya nchi ukilinganisha na klabu nyingine zinazoshiriki Ligi Kuu ya Bara Jumapili hii kuanzia saa 10:00 jioni msimu huu zinashuka huku zikiwa na mazingira tofauti kuanzia kwa wachezaji wake na benchi la ufundi.

Azam ndiyo kinara wa ligi hiyo kutokana na jana Jumamosi kufikisha pointi 20 baada ya kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya JKT Oljoro na Simba yenye pointi 18 kushuka hadi nafasi ya tatu huku Yanga yenyewe ni ya nne ikiwa na pointi 15.

YANGA

Ikiwa ndio mabingwa watetezi, Yanga itashuka dimbani ikiwa inataka kuendeleza heshima ya kumfunga mtani wake mfululizo na kumuondoa katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo yenye timu 14.

Yanga ambayo iko chini ya Mholanzi, Ernie Brandts, imejipanga kuifunga Simba ikiamini kwamba ndiyo timu yenye kikosi bora msimu huu na wachezaji wake ambao wako pamoja kwa msimu wa pili wanauwezo wa kuwapa matokeo mazuri.

Katika safu ya ushambuliajia, mabingwa hao watetezi wanatarajia kuwatumia Jerryson Tegete, Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza, Mrisho Ngasa na Haruna Niyonzima.

Hata hivyo washambuliaji hao wanaotarajiwa kubadilishwa na Simon Msuva, Shabani Kondo

bado wameshindwa kuziona nyavu za wapinzani wao kama kocha huyo wa zamani wa APR ya Rwanda anavyotaka kwa kufunga magoli matatu kwa kila mechi.

Safu ya ulinzi ya wawakilishi hao wa Bara katika mashindano ya Klabun Bingwa Afrika mwakani inatarajiwa kuongozwa David Luhende, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondani na Mbuyu Twite.

Yanga imekuwa ikiwatumia zaidi wachezaji wake viungo hasa Athumani Iddi ‘Chuji’ au Frank Domayo kuanzisha mashambulizi na kwa kupiga pasi ndefu kwa kuamini kwamba washambuliaji wake akiwemo Msuva kutumia kasi kuelekea katika lango la wapinzani wao.

Katika kujiandaa na mchezo huo, Yanga ilisafiri hadi kwenye kisiwa cha Pemba, Zanzibar kuweka kambi na ilirejea jijini Dar es Salaam Ijumaa jioni.

SIMBA

Wekundu wa Msimbazi ambao miaka 10 iliyopita walipeperusha vyema bendera ya nchi katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika kwa kufika hatua ya robo fainali, Jumapili hii inashuka tena ikiwa chini ya mshambuliaji wake wa zamani, Abdallah Kibaden ‘King’.

Mechi hii inakuwa ni ya kwanza kwa King ambaye amejiunga na Simba akitokea Kagera Sugar na akiiongoza timu iliyofanya mabadiliko makubwa kwenye usajili wake msimu huu.

Simba iliamua kufumba macho na kuwaacha nyota kadhaa kwa sababu tofauti wakiwemo aliyekuwa kipa chaguo la kwanza na nahodha, Juma Kaseja, Juma Nyoso, Haruna Moshi ‘Boban’, Felix Sunzu na Mwinyi Kazimoto.

King ambaye bado anasema kwamba hajapata kikosi cha kwanza anatarajia kushusha timu yenye wachezaji mchanganyiko ambapo baadhi yao watakuwa ni wazoefu akiwemo kiungo, Amri Kiemba, yosso ( Jonas Mkude, Ramadhan Singano ‘Messi’, Christopher Edward) na wageni Betram Mombeki na Amissi Tambwe.

Katika mechi zilizopita, Simba imekuwa ikimtumia washambuliaji wawili huku ikijaza viungo lakini kutokana na mshambuliaji wake kutoka Burundi, Tambwe kuonekana anajua kukaa kwenye nafasi yake, mchezaji huyo huenda akashindwa kutamba kwenye mchezo huo hivyo inatakiwa kujiandaa kupanga nyota mwingine ili kufanikisha wanafunga na kuibuka na ushindi.

Tambwe ambaye ndiyo kinara kwa sasa wa kupachika magoli baada ya kufunga magoli nane ameonekana si kitu katika mechi mbili zilizopita na hali hiyo huenda ikarejea kesho ambapo beki wa Yanga, Cannavaro akamdhibiti.

Kwa kawaida mechi hiyo ya watani mara nyingi hushuhudiwa wachezaji wakikamiana na kufanya rafu zisizo za msingi na kuondoa ladha ya kuonyesha vipaji vyao.

Lakini kama hilo halitaonekana basi mashabiki watakaohudhuria mchezo huo na wale watakaofuatilia kupitia vituo mbalimbali vya televisheni, watafaidi soka la kiufundi kwa sababu ni nafasi nyingine ya kila mchezaji kuonyesha kipaji na uwezo wake ili aitwe katika timu ya taifa ya Bara (Kilimanjaro Stars) au Zanzibar Heroes ambazo hivi karibuni zitaingia kambini kujiandaa na mashindano ya Kombe la Chalenji.

Pia ni sehemu ya wachezaji husika watakaopangwa kujiuza kwa mawakala na makocha mbalimbali watakaofuatilia mchezo huo.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

KAMATI YA UCHAGUZI YATANGAZA WAGOMBEA TFF

Arsenal wapeta kileleni