in ,

Yanga 1-1 Zanaco

Wachezaji wa yanga, wakifurahia goli lao.

*Mambo manne tuliyojifunza*

Yanga wamejiweka kwenye mazingira magumu ya kufuzu hatua ya makundi klabu bingwa Afrika baada ya kulazimishwa sare ya goli moja kwa moja na Zanaco.

Yanga walikuwa wa kwanza kupata goli kipindi cha kwanza kufuatia kazi nzuri iliyo fanywa na Msuva kwa kufunga goli zuri baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Mzambia Justine Zulu.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Yanga wakionekana wakizidiwa muda mwingi ws mchezo, Zanaco walifanikiwa kusawazisha goli kupitia kwa Straika wao Kwame akiunganisha krosi.

Hadi mwaamuzi kutoka Djibouti anapuliza filimbi wa mwisho Yanga moja na Zsnaco ya Zambia moja
Mambo manne tuliyojifunza kwenye mechi ya Yanga na Zanaco

1.Msuva muda wake wa kwenda kujaribu maisha ulaya ndo sasa

Winga wa klabu ya Yanga Simon Msuva amekuwa kwenye kiwango bora kuliko misimu ya nyuma, ndiye silaha ya Yanga kwa sasa, ana funga halikadhalika kusaidia mengine kwa wenzake, kwenye mchezo dhidi ya Zanaco alikuwa mwiba kwa upande wa Wazambia hao na hata kapteni wa Zanaco, Tembo alikili kuwa winga huyo ndiye alikuwa akiwapa wakati mgumu muda wote wa mchezo

2.Juma Makapu ni bora kuliko Yondani kwenye eneo la kiungo wa ulinzi

Mwalimu Lwandamina inabidi amuamini kiungo mkabaji Makapu kuliko kuendelea kumtumia Yondani kwenye kiungo wa ulinzi, dhidi ya Zanaco timu yote ilifia mikononi mwa Yondani, kiungo cha Yanga kilizidiwa kwa muda mwingi kwa sababu Yondani kukosa maarifa ya kucheza kama kiungo.


3.Uchovu ndiyo unaigharimu Yanga kwa sasa

Yanga hawajapata muda wa kupumzika tangu mwaka jana, timu imeunga kutoka msimu uliopita na msimu, hivyo wachezaji wanaonesha kuchoka hasa kwa kipindi cha pili na tatizo limekuwa likitokea hata kwenye Ligi Kuu.

4.Zanaco walikuwa wazuri kwenye utimamu wa mwili

Wachezaji wa Yanga walizidiwa kwenye matumizi wa nguvu na kasi na Wazambia hawa ndiyo maana kwa kwenye mipira yote ya kugombania Zanaco walifanikiwa kuliko Wana jangwani hao

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
MS

TUWE MAKINI NA VIPIMO VYA NDIMI ZETU KWA SAMATTA

Tanzania Sports

PAMOJA NA KADI NYEKUNDU, FAHAMU MAMBO MANNE YALIYOSABABISHA UNITED KUPIGWA