in , ,

Woga wa penati AFCON

*Nahodha wa Ghana akimbia wajibu huo

HOMA ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) inayoanza Jumamosi ijayo imeanza kupanda, safari hii nyota wakiogopa penati.

Nahodha wa Ghana, Asamoah Gyan ametangaza kwamba hatapiga penati yoyote kwa taifa lake kwenye michuano hii.

Gyan mwenye umri wa miaka 27 anasema huwa kuna siku za balaa, ambapo hata wachezaji maarufu zaidi duniani kama Lionel Messi na Cristiano Ronaldo hukosa penati.

Hata hivyo, anaweka bayana kwamba atalazimika kupiga penati ikiwa Black Stars watafikishwa kwenye kwenye kupigiana penati baada ya kutoka suluhu au sare.

Gyan aliyetamba kwenye Ligi Kuu ya England (EPL) kabla ya kuchepukia Mashariki ya Kati, anasema kabla ya kufariki duniani, mama yake alimshauri aache kupiga penati.

Mchezaji huyu alikosa penati dhidi ya Uruguay, ambayo kama angepata ingewapeleka Ghana nusu fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010 na kuwa timu ya kwanza Afrika kufika kwenye nne bora duniani.

Alikosa tena penati nyingine mwaka 2010 kwenye nusu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Februari mwaka jana.

Alidhihakiwa na washabiki kiasi cha kumfanya kupumzika kuchezea Black Stars kwa muda.

“Nimeamua sasa kwamba sitapiga tena penati kwa ajili ya timu ya taifa. Wachezaji maarufu zaidi wamekosa penati – Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Diego Maradona – wote nyota.

Siku ya kufa nyani hilo hutokea, lakini miezi kadhaa iliyopita nilisema kwamba singepiga tena penati. Kabla mama yangu kufariki dunia (Novemba) aliniambia niache mambo ya penati,” anasema Gyan.

Katika mashindano haya, Ghana wamepangwa kundi moja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mali na Niger.

Nahodha huyo amekaririwa akisema: “Kwa kweli kisaikolojia ni jambo gumu sana kwangu, kukosa penati mbili muhimu mfululizo kwa nchi yangu.

“Bado sijaondokana na taharuki iliyonikumba kwenye Kombe la Dunia mwaka 2010 na hii ya mwaka jana.”

Gyan alirejea kwenye kikosi cha Ghana Agosti mwaka jana, ambapo Oktoba alipewa unahodha, akichukua nafasi ya John Mensah.

Huyu ndiye mtu anayetarajiwa kuongoza mashambulizi ya timu yake, na kwa hilo bado anapewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri.

Anasema kwamba atakuwa kiongozi mzuri kuwaandaa wenzake kupiga penati, na kwamba ikifikia kupiga zile tano au zaidi, akichaguliwa hatasita kuchukua jukumu hilo.

Imepita miaka 10 sasa tangu Ghana itwae kombe la AFCON, na Gyan anasema wananchi wa Ghana wanawasubiri warejee nyumbani na kombe. Wanaanza kucheza na Kongo Jumapili, siku ya pili ya mashindano hayo.

Enhanced by Zemanta

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Manchester City, United zalipua

Watanzania tujivunie timu zetu za Taifa, bila kujali wachezaji wanachezea timu zipi…….