in , ,

WILSHERE, KALAMU YENYE FURAHA NA MWANDISHI MWENYE MAUMIVU

Jack Wilshere alianza kama kijana aliepanda kwenye shule ya soka ya Arsenal na ameichezea klabu hiyo maisha yake yote mpaka sasa isipokuwa tu kwa kutolewa kwa mkopo mara kadhaa. Amekwenda Bolton na Bournemouth kwa nyakati tofauti.

Ni mchezaji anaeipenda hasa klabu ya Arsenal lakini safari yake ya soka imekuwa na changamoto. Jack Wilshere mara kwa mara amekuwa akiwapa furaha mashabiki wa klabu hiyo kutokana na performance zake uwanjani japo yeye mwenyewe amekuwa akipitia kipindi kigumu kufanya hivyo.

Hapa nikamwona mwandishi maarufu wa hadithi na vitabu, Charles Dickens. Vitabu na hadithi zake nyingi fupi fupi zimekuwa na mwisho mzuri lakini ukweli ni kwamba hadithi yake yeye mwenyewe ni maumivu.

Muda mwingi wa maisha yake mwanzoni alishinda akiwa jela kwa sababu baba yake hakuwa na uwezo wa kulipa madeni aliodaiwa na enzi hizo mzee akiswekwa maana yake nyote mnaenda ndani isitoshe ikabidi pia afanye kazi kwenye kiwanda kwa ajili ya kupata pesa ya kulipa madeni hayo japo mazingira hayakuwa rafiki.

Wakati mwengine mtu anajaribu kukupa furaha huku yeye mwenyewe akiwa na maumivu yake na hichi ndicho haswa akifanyacho Jack Wilshere.

Uchezaji na bidhaa ya mwisho ya Wilshere uwanjani mara nyingi imekuwa nzuri kama tu vitabu vya Dickens vilivyokuwa na mwisho mzuri kwenye kalamu yenye maumivu yake.

Muda mwingi wa maisha yake ya soka, Jack Wilshere amekuwa kwenye maumivu ya kukaa sana nje mpaka ikabidi kutoka kwa mkopo pale iliposhindikana kabisa yeye kumshawishi mwalimu wake kutokana na maumivu yaliomsumbua.

Wanamwita Jack The Lad, Jack Wilpower kwa sababu kwanza ni mtoto wa nyumbani ikisha jamaa huwa anawakosha sana mashabiki wa Arsenal. Huyu ndie mtu anayeweza kuwa anaumia zaidi uwanjani pale Arsenal wanapopoteza. Ndio mchezaji pekee kwenye EPL kwa sasa asiye na wakala kwani Arsenal ndio klabu ya mapenzi yake na hatokuja kuhamia klabu nyingine.

Wilshere ana kila sababu ya kuwa nahodha wa klabu ya Arsenal endapo maumivu yake hayatoingiliana na furaha ya mashabiki. Arsenal inaonekana kukosa kiongozi wa kuhamasisha hasa pale matokeo yanapokuwa hayaendi vizuri na ni wazi Wilshere anapokuwa mzima ni wa kuvishwa kitambaa bila ya mjadala. Anastahili kuwa nahodha wa kudumu.

Kwenye siku yake kabisa mpira unapomkubali Wilshere anakuwa hana tofauti na Iniesta, Kroos, De Bruyne kwa maana ya kwamba ni mtu anaekimiliki hasa kile kiungo cha Arsenal na kuamua timu icheze vipi na kwa kasi ipi kwa maana ya kuwa “Midfield Controller”.

Siku zote amekuwa ni mtu wa kujitoa kwa 100% kwani anacheza katika klabu anayoipenda. Jack Wilshere anapitia mengi magumu kwenye soka lake ili kuwapa furaha mashabiki wa Arsenal. Usisome tu vitabu na kumfurahia miguu pale mwisho tu jua kuna watu wana maumivu wamekabiliana nayo nyuma ya kalamu na furaha zenu.

Report

Written by haatimabdul

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

NI LAZIMA MOURINHO ATATUE TATIZO LA POGBA

Tanzania Sports

ZIMBWE ANGUSHA USO KABLA HUJAENDA MVANGE