in , , ,

‘Wilshere ataendelea kuumia’

 

Utimamu wa mwili wa kiungo wa Arsenal na England, Jack Wilshere unatia wasiwasi baada ya kuumia na sasa atakuwa nje ya dimba kwa muda.

 

Katika kuongeza hofu juu ya hatima ya mchezaji huyo, kocha Arsene Wenger amesema Wilshere ataendelea kuumia, akimfananisha na gari isiyo na breki ya mkono.

 

Wenger amesema ni vigumu kubadilisha aina ya uchezaji wake kwa ajili ya kuzuia kupata majeraha zaidi. Atakosa wiki nne za mwanzo za Ligi Kuu ya England (EPL) baada ya kuumia kifungo cha mguu.

 

Mwaka huu Wilshere, 23, amecheza dakika 219 tu kwenye mechi za ushindani kutokana na kuumia mara kwa mara, ambapo Wenger anadhani anakaa mno na mpira badala ya kutoa pasi hivyo kukabwa na wapinzani kiasi cha kumuumiza.

 

“Jack anavyocheza ni kwa namna ya kukaa na mpira na kuwachokoza wapinzani wake kwa kujipenyeza kati yao, hiyo ndiyo nguvu yake lakini ndiyo sababu ya kuumia kwake. Ukimbadili aina ya uchezaji maana yake umempokonya nguvu yake,” anasema Mfaransa huyo.

 

Anaongeza kwamba kila mtu hupata elimu juu ya jinsi ya kukabili hali mbalimbali kwa jinsi alivyozoea. Kutokana na umri na uzoefu huweza kukabiliana nazo kwa ufanisi zaidi pasipo kubadili aina ya uchezaji.

 

“Alipokuwa mdogo zaidi alikuwa jasiri mno. Alipokuwa na umri wa miaka 17 wakati mwingine nilikuwa namwambia; ‘hutakiwi kwenda pale’. Lakini nadhani Jack amezaliwa na ubongo wa soka na ubunifu, hana breki ya mkono,” anasema Wenger.

 

Wenger anaonesha kwamba hana nia ya kusajili mchezaji mwingine kwani anao wengi wenye kiwango cha juu katika kiungo na anasema ikiwa ni kusajili atafanya hivyo kwa mchezaji mwenye kipaji cha kipekee.

 

Kwa upande wa ushambuliaji bado hajaongeza pia japokuwa alikuwa akihusishwa na kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema, anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 35.

 

Arsenal wataanza EPL pia bila Alexis Sanchez aliyepewa mapumziko zaidi kutokana na kushiriki na Timu ya Taifa ya Chile kwenye michuano ya Copa America ambapo walitwaa ubingwa, akiwa na mchango mkubwa huko.

 

Shujaa wa Arsenal, Thierry Henry amekuwa akishauri Arsenal wasajili wachezaji zaidi ili wachuane na Chelsea kupata ubingwa wa England.

 

Wenger pia anaonesha kutofurahishwa kwa ligi kuanza mapema nchini England, akisema ni kosa kubwa, kwa maelezo kwamba hata madaktari wanashauri wachezaji wapate mapumziko ya muda mrefu.

 

Manchester City walikuwa na mpango wa kumsajili Wilshere, lakini Wenger akawafunga mdomo kwa kuwaambia hauzwi na muda mfupi tu baadaye akamwongezea mkataba wa ‘muda mrefu’ Emirates.

 

Hata kuumia kwake hakuwezi kumbadilisha mawazo Wenger, anayemuamini sana kiungo huyo wa England, japokuwa amekuwa akikosa mechi muhimu kutokana na kuwa majeruhi.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

TUTAENDELEA KUPOROMOKA VIWANGO VYA FIFA

MANCHESTER UNITED 1 – TOTTENHAM – 0