in , , , ,

Wigan wawatandika Man City


*Nusu fainali ni Arsenal na Wigan
*RVP naajiandaa kuondoka Man U

Manchester City wameugulia maumivu baada ya kutandikwa na Wigan Athletic katika robo fainali ya Kombe la FA na kufuta ndoto za kocha Manuel Pellegrini kutwaa makombe manne msimu huu.

Man City walitumia kila mbinu, kubadilisha wachezaji, kuongeza kasi ya ushambuliaji lakini walichoambulia ni bao moja la kufutia machozi kupitia kwa Samir Nasri huku Wigan ambao ni mabingwa watetezi wakiondoka na ushindi wa 2-1.

Wigan waliwatoa Man City kwenye fainali ya kombe hilo mwaka jana, ambapo wiki iliyopita tu Man City walitwaa Kombe la Ligi na Pellegrini akaanza kuchekelea. Mabao ya Wigan yalifungwa na Jordi Gomez na James Perch.

Kichapo hiki kinakuja wakati man City wakisubiri kurudiana na Barcelona kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambapo kwenye mechi ya kwanza Man City walilala 2-0.

Kwa ushindi huo, Wigan sasa watakwaana na Arsenal kwenye nusu fainali katika dimba la Wemblew wakati Hull City waliowatandika Sunderland 3-0 watacheza nusu fainali nyingine na Sheffield United waliowafunga Charlton 2-0 Jumapili hii.
 
ROBIN VAN PERSIE KUONDOKA MAN U

Mshambuliaji wa kati wa Manchester United, Robin van Persie anatarajiwa kuihama klabu hiyo, ama kwa yeye mwenyewe kuamua kwenda kwingine au kwa kocha David Moyes kutumia rungu lake ili kuleta mchezaji bora zaidi.

Katika mechi ya Jumamosi dhidi ya West Bromwich Albion, Van Persie alishindwa kuonesha cheche, akapigwa kadi ya njano kwa mchezo mbaya na kuonywa tena na mwamuzi, kabla ya Moyes kumtoa dakika ya 60 na kumwingiza Danny Wellbeck.

RVP alionesha kusikitishwa na kutolewa uwanjani, na alitoka akitikisa kichwa wakati ambapo inaelezwa kuna mipango ya yeye ama kurudi Arsenal au kwenda Italia. Iwapo ataondoka Old Trafford, RVP atapoteza pauni milioni 10 ambazo ni haki yake kama atacheza vyema hadi mwisho wa mkataba wake huo. Inaelezwa yupo tayari kuondokana nazo.

Kuna habari kwamba Mdachi huyo ambaye msimu huu si mzuri kwake, anaweza kujiunga na wanaoongoza ligi nchini Italia, Juventus waliokuwa wakimhitaji kabla ya kuondoka Arsenal, lakini pia inadaiwa anaweza kurudi Arsenal anakodai ni zaidi ya nyumbani.

Juventus wapo tayari kutoa pauni milioni 24 ambazo Man U waliwalipa Arsenal miezi 19 iliyopita na pia kumlipa kiasi kinachokaribia na mshahara wake wa wiki wa sasa ambao ni pauni 250,000. United wanadaiwa kumtaka Edinson Cavani wa PSG ambaye huenda akawagharimu pauni milioni 58.
 

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Chelsea wazidi kupaa Ligi Kuu

Arsenal pigo mara mbili