WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda atakuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mashindano ya taifa ya netiboli yatakayofanyika kuanzia Juni 29 hadi Julai 2 kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katibu mkuu wa Chama cha Netiboli (Chaneta), Mwajuma Kisengo alisema hadi sasa ni mikoa 13 tu ndio imethibisha kushiriki mashindano hayo.
”Maandalizi yote yamekamilika,” alisema.”Tunatarajia Waziri Mkuu Mizengo Pinda ndiye atakayetufungulia mashindano haya. Natoa wito kwa wakazi wa Dar es Salaam kufika kwa wingi kushuhudia mashindano haya.”
Awali walipanga tarehe ya mwisho ya kuthibisha kushiriki wa mashindano hayo kuwa ni Juni 15 lakini waliamua kusogeza mbele hadi leo ili baadhi ya mikoa iliyokuwa haina uhakika wa kupata fedha kwa ajili ya kufanikisha ushiriki wake.
Alisema baada ya tarehe ya mwisho ya kuthibisha kushiriki ambayo ni leo, mikoa ambayo itakuwa haijathibitisha itakuwa imejitoa katika mashindano ya mwaka huu na kwamba siku mbili baadaye ratiba nzima ya mashindano hayo itapangwa.
Aliitaja mikoa iliyothibitisha kuwa ni Dar es Salaam, Iringa, Kilimanjaro, Tanga, Dodoma, Mwanza, Lindi, Mbeya, Manyara, Kagera, Morogoro na Pwani.
Comments
Loading…