in , , ,

Wazazi wa Gareth Bale waingilia usajili


*Mwenyekiti Spurs arudi London kuzuia

Sakata la nyota wa Tottenham Hotspur, Gareth Bale kuhamia Real Madrid limefika hatua mpya, baada ya wazazi wake kuingilia.
Mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy mwenye ushawishi mkubwa, alikatisha mapumziko ya kifamilia Florida, Marekani kurudi kushughulikia sakata hilo.
Levy anayejua kunasa wachezaji wazuri kwa bei ndogo au hata bure, amekasirishwa na dau kubwa linalovunja rekodi ya dunia lililotolewa na Real Madrid kumchukua Bale.
Levy ameungana na kocha Andre Villas-Boas kukataa kumuuza Bale, lakini baada ya mchezaji mwenyewe kusema anataka kuondoka, hali imekuwa tete White Hart Lane.
Levy alikuwa akutane na wawakilishi wa Bale, lakini wengi walishangazwa mwanzoni mwa wiki hii kuona baba na mama yake nao wakitinga kwenye chumba cha mkutano.
Inaaminika wanalenga kumtia shinikizo Levy ili akubaliane na matakwa ya mtoto wao, ikiwa anataka kuhama. Levy, hata hivyo, angeweza kumshawishi vinginevyo Bale, japokuwa huenda amechelewa.
Wawakilishi wa Bale inasaidikiwa walimweleza mwenyekiti Levy jinsi Bale alivyodhamiria kuondoka, ikiwa ni muda mfupi tangu mchezaji mwingine, Luka Modric kushinikiza na hatimaye kujiunga Santiago Bernabeu.
“Sikuamini nilipowaona wazazi wa Bale wakiingia kwenye viwanja vya mazoezi vya Spurs…Mungu tu anajua walichomwambia Levy,” chanzo cha habari kilikaririwa na The Sun kikisema.
Imedaiwa kwamba Rais wa Real Madrid, Florentino Perez atakutana na Levy mapema wiki ijayo huko Miami, Marekani kujadili zaidi usajili wa Bale, kwani Levy atarudi huko, na Perez tayari yupo na klabu yake huko.
Habari zaidi zinasema kwamba hali ikiwa ngumu kwa Spurs, Villas-Boas yupo tayari kumchukua Fabio Coentrao wa Real Madrid, kwani anaweza kucheza kama beki wa kushoto na winga.
Inadaiwa kwamba pamoja na fedha, Real wanataka kuwapa Spurs Angel Di Maria na Coentrao ili tu wamchukue Bale, anayesadikiwa kuwa wa tatu kwa ubora duniani baada ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Kallon akataliwa FA ya Sierra Leone

Christian Benitez: Dharau katika kifo