in ,

Watford wamewazuia ‘Liver’ kuifikia rekodi ya Arsenal

Kika jambo lina mwisho wake na mserereko wa ushindi wa Liverpool katika Ligi Kuu ya England (EPL) umefikishwa mwisho na timu wasiotarajiwa – Watford.

Wakiwa mbali juu kileleni kwa tofauti ya alama 22 dhidi ya wanaowafuata – Manchester City, Liverpool waliingia uwanujani wakijiamini Vicarage Road lakini Watford wakawashangaza kwa kuwakung’uta mabao 3-0.

Liverpool wanaofundishwa na Jurgen Klopp kutoka Ujerumani, walikuwa na matarajio kwamba wangeifikia rekodi ya Arsenal ya kutofungwa katika msimu mzima 2003 huko. Walitoka kushinda mechi 18 zilizopita katika ligi, wakawa kama timu wasiofungika na hata ukitangulia kuwafunga wanasawazisha na kuongeza bao au mabao na kutoka uwanjani vifua juu.

Lakini pale kwa Watford hakika walibanwa kila upande, wakishindwa kujilinda, kushambulia haikuwa na mafanikio yoyote wakaondoka wamechoka na kurudi kwao wakijiuliza juu ya kilichotokea kama ni kweli.

Watford wangeweza hata kufunga zaidi ya mabao hayo matatu kutokana na usiku ule ulivyokuwa lakini hata hayo ni mengi kwa klabu ya hadhi ya Liverpool wa msimu huu ambao wanaheshimika ndani na nje ya nchi, wakiwa pia ni mabingwa wa Ulaya.

Washabiki wa Watford waliohudhuria waliingia kwa unyonge, wakijichukulia kama wasindikizaji tu, lakini kipenga cha mwisho kilipopulizwa, hakika walikuwa kama wafalme, wakitamba kwa kila namna kwa sababu ilikuwa kama mende ameangusha kabati.

Wakati Liverpool wakiongoza ligi kwa alama nyingi, Watford walikuwa miongoni mwa timu tatu zilizo kwenye ukanda wa kushuka daraja na sasa wamejiondoa wakibaki kwneye nne za chini na watakuwa wnaajiamini zaidi kwenye mechi zijazo.

Aliyecheza vyema kuliko wengine kwa Watford, akitoka kwenye majeraha alikuwa Ismaïla Sarr aliyesisimua wengi, akifgunga mabao mawili ya mwanzo na pia kutoa usaidizi kwa lile la tatu la Troy Deeney.

Kwa ujumla alikuw akiwachachafya Liverpool kadiri alivyopenda kwa kasi na mbinu zake nyingine akitokea kwenye wingi ya kulia. Ana umri wa miaka 22 tu akisajiliwa kutoka Rennes kwa £25m kiangazi cha mwaka jana. Alipata heshima kwa washabiki kusimama na kumsalimia alipobadilishwa dakika ya 82.

Kocha wake, Nigel Pearson anasema wazi kwamba ni mchezaji mzuri na amewasaidia kuwavusha walipokuwa wakihitaji sana. Wengine waliovuta macho ya washabiki walikuwa akina Will Hughes na Abdoulaye Doucouré kwenye kiungo lakini pia Gerard Deulofeu kulembele aliyekuja kuumia wakati akikabiliana na Virgil van Dijk kuupata mpira.

Watford walipata mabao katika safu ya ulinzi iliyoongozwa na Dejan Lovren aliyepewa nafasi badala ya Mcameroon Joël Matip kwa sababu ya kuwa Joe Gomez alikuwa ameumia. Lovren alikosea kwneye mpira wa kurushwa kwa Adam Mesina katika majenzi ya bao la kuongoza la Watford dakika ya 54.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
mchezo wa soka, mahasimu wakiwa uwanjani

Kariakoo Dabi: Jua chanzo, ukali wake

Tanzania Sports

Madrid wababe wa Barcelona