in , , ,

WAKIMATAIFA WATOLEWA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Wakimataifa (Yanga) wameondoshwa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika usiku huu kufuatia kipigo cha mabao mawili kwa moja walichopokea kutoka kwa Al-Ahly huko Alexandria.

Al-Ahly walifanya mashambulizi mengi wakitumia kasi ya wachezaji wao kwenye kipindi cha kwanza lakini Vincent Bossou na wenzie walifanya kazi nzuri kuwadhibiti huku gilikipa Deogratius Munishi akifanya kazi ya ziada kuokoa michomo kadhaa ya hatari na kufanya kipindi hicho kimalizike matokeo yakiwa 0-0.

Kiungo wa kati Hossam Ghaly akawapatia Al-Ahly bao la kuongoza ndani ya dakika ya 52 akiunganisha mpira wa kona uliopigwa na winga Abdallah Said. Ghaly aliruka akiwa huru na kutumbukiza mpira huo wavuni kwa kichwa kiurahisi.

Dakika 15 baadae Yanga wakasawazisha bao hilo kupitia kwa Donald Ngoma ambaye pia alifunga kwa kichwa akiunganisha krosi safi iliyopigwa na mlinzi wa kulia Juma Abdul baada ya kumtoka mlinzi wa Al-Ahly.

Bao hilo liliwaamsha Yanga ambao walionekana kufanya mashambulizi zaidi wakijaribu kutafuta bao la ushindi. Mnamo dakika ya 73 mwalimu Hans de Pluijm akafanya mabadiliko kwa kumtoa Donald Ngoma na kumuingiza Malimi Busungu.

Makali ya Al-Ahly yalionekana kupungua kwa kuwa walihtaji kujilinda kuepuka kuruhusu bao la pili ambalo lingewalazimu kutafuta mabao mawili kwenye dakika zilizokuwa zimesalia ndipo waweze kusonga mbele.

Hata hivyo vijana hao wa mwalimu Martin Jol walifanya shambulizi kali mnamo dakika ya 87 ambapo golikipa Deo Munishi alisimama vizuri langoni na kuokoa mashuti ya washambuliaji.

Baada ya dakika tisini za sheria za mchezo kumalizika mwamuzi Mahamadou Keita kutoka Mali akaongeza dakika tano za nyongeza. Pengine alijaribu kufidia dakika zilizopotezwa na matukio kadhaa likiwemo la vurugu kwenye dakika za mwishoni.

Al-Ahly wakapata bao la ushindi kwenye dakika ya 95 kupitia kwa Abdallah Said aliyepasia vyema mpira wavuni.
Ushindi huo unawapeleka mabingwa hao mara nane wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye hatua ya makundi. Yanga wao wanashuka mbaka kwenye Kombe la Shirikisho Afrika kutafuta nafasi ya kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

AZAM NJE KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

Tanzania Sports

AZAM YATINGA FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO