in , , ,

Waingereza wanavyojenga soka ya Ufaransa

 

Ufaransa wanauza bidhaa na huduma nyingi nje ya nchi yao, kuna mvinyo aina nyingi na nzuri, marashi ya kifahari na magari, lakini huenda mauzo muhimu zaidi kwa Uingereza kutoka huko ni wanasoka wake.

Yawezekanaje mambo haya? Ni kwa sababu ya mchango kundi kubwa la washabiki wa soka ambao ni sehemu muhimu ya wachangiaji wa mapato ya klabu za England, mapato ambayo ndiyo huja kutumika kununua wachezaji.

Nchini Ufaransa watu wa sekta za usafiri wa anga, dawa baridi, magari, vifaa vya anasa wanaweza kujidai sana, maana wanatamba kwa kutengeneza na kuuza, anzia kampuni kama L’Oréal hadi Renault, Dassault na LVMH zinazojulikana kote duniani.

Hata hivyo, leo hii kadiri soka ya ngazi ya klabu inavyotokea kuwa biashara muhimu kimataifa, klabu za Ufaransa zinapanda hadhi kwa kuwa ‘wauzaji’ wazuri wa wachezaji nje ya nchi, na wao kujitengenezea kiasi kikubwa cha fedha.

Dirisha la usajili la msimu wa kiangazi lilipofungwa hivi karibuni, zaidi ya euro bilioni moja zilikuwa zimetumiwa katika kipindi cha miezi mitatu na ushee, tangu kumalizika kwa msimu wa 2014/15.

Unaweza kuyaita marejeo ya imani kwa uchumi wa Uingereza, yakiwa ni matokeo ya klabu zenye fedha zaidi Uingereza kukiuka hata kanuni za Shirikisho la Soka la Ulaya (Uefa) za uungwana katika matumizi ya fedha, lakini zile za Ufaransa zinatumia fursa hiyo kufaidi kwa kuuza wachezaji wao.

advertisement
Advertisement

Takwimu za haraka zinaonesha kwamba kati ya fedha zilizotumiwa na klabu za England, euro milioni 200 zilikwenda kwa klabu za Ufaransa. Pamoja na kwamba siku hizi wachezaji huuzwa ghali na mtu angeweza kudai hicho si kiasi kikubwa, jambo moja kubwa tunalojifunza ni jinsi utajiri wa Ligi Kuu ya England (EPL) ulivyo na athari chanya kwa Ufaransa.

Hebu tujiulize; fedha zote hizo za EPL zinatoka wapi? Kuna dili mpya mezani juu ya haki za televisheni nchini Uingereza, litakalozingiza huko euro zaidi ya bilioni saba katika kipindi cha zaidi ya miaka mitatu kuanzia 2016.

Bado kuna dili la kimataifa linalotarajiwa kuthibitishwa hivi karibuni, ambalo litaingiza kiasi kingine cha euro bilioni nne katika kipindi hicho hicho, ikimaanisha kwamba klabu inayomaliza kwa kushika mkia EPL watapata kiasi kikubwa kuliko klabu inayotwaa ubingwa nchini Ufaransa.

Mzee wa viwango...
Mzee wa viwango…

Mapato ya EPL yatakuwa matawi ya juu sana, yakilinganishwa na yale ya NFL na NBA, lakini yakiwa yameyazidi yoyote yanayopatikana katika soka ya Ulaya. Hebu tuangalie zaidi kima hicho cha euro milioni 200 ambacho Ufaransa wanapata kutoka England.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na kampuni ya Ernst & Young mwaka 2013, wanasoka 44 wa kulipwa kutoka klabu za Ufaransa kwa pamoja walikuwa wanajikusanyia euro bilioni 1.5, lakini kati ya hizo Paris St Germain ikiwa na mgawo wa euro milioni 400, kwa maana ya wachezaji wake.

Ukiachilia mbali nyongeza iliyowekwa na wawekezaji kutoka Qatar kwenye soka ya Ufaransa, kwa ujumla mapato ya klabu za taifa hilo yamepungua katika miaka ya karibuni. Dili za televisheni nchini Ufaransa ni ndogo kuliko ilivyokuwa awali na mapato kutokana na udhamini na matangazo ya bidhaa hayakuwa mazuri kutokana na mtikisiko wa uchumi nchini Ufaransa.

Sasa je, hizo euro milioni 200 zimekwenda wapi? Tazama kwanza uhamisho wa Anthony Martial kutoka Monaco kwenda Manchester United ambao uligharimu kati ya euro milioni 50 na 80 kwa kutegemeana na yupi unamwamini zaidi.

Nyota mpya wa ufaransa, anayewika na Man Utd...
Nyota mpya wa ufaransa, anayewika na Man Utd…

Euro milioni 150 zilitumiwa kwa ajili ya wachezaji wengine 28 kutoka klabu 18 tofauti za Ufaransa. Suala si kwamba wachezaji nyota wanahamishwa kutoka klabu moja kwenda nyingine kwa kiasi cha kushitusha cha fedha, hoja ni kuwa kiwango anuai cha fedha kinagawanywa miongoni mwa wadau wa soka ya Ufaransa.

Utafiti uliofanywa na umoja wa wanasoka wa kulipwa wa Ufaransa unakadiria kwamba mwaka 2013, ajira 26,000 nchini Ufaransa ziligharimiwa moja kwa moja na klabu 44 zenye wachezaji wa kulipwa na kwamba mauzo yao yanatakiwa kuzidishwa mara nne ili kupata jinsi klabu zilivyosaidia uchumi mahalia.

Mara euro milioni 200 zinageuka kuwa euro milioni 800 na kiasi kikubwa miongoni mwa hiki kinawekezwa kwenye klabu za Ufaransa na si Paris pekee. Kwa minajili ya uwekezaji wa kigeni, hili ni suala kubwa na si kitu cha wakati mmoja, kwani ni endelevu.

Sasa tujiuliuze, ipi athari kwa klabu za soka za Ufaransa kutokana na mwelekeo wa wachezaji kuondoka nchini? Je, hii haiui soka ya Ufaransa? Ukiangalia orodha ya uhamisho wa wachezaji kiangazi hiki, utaona kwamba walau robo ni mazao ya mfumo wa ufundishaji wa Ligi ya Ufaransa wakati waliobaki walifunzwa soka ng’ambo.

Wengi wao waliletwa si miaka mingi sana kutoka nchi zenye ligi ndogo zaidi, kama Afrika ambako klabu za Ufaransa zina wang’amuzi wazuri wa vipaji na pia mtandao wa kununua wachezaji.

Klabu za Ufaransa zimekuwa makini sana katika kutambua aina ya wachezaji ambao baada ya kukuzwa kwa muda mfupi watatengeneza fedha nzuri kwa mauzo kwenye EPL. Wakati huo huo, klabu hizo hutumia bonsai hiyo kuwekeza kwenye miradi ya soka katika ngazi za chini na pia kutumia kwenye program zao za maendeleo.

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Ufaransa.
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Ufaransa.

Mahudhurio kwenye mechi Ufaransa yameongezeka katika miaka ya karibuni na washabiki wanaotazama televisheni kwa ajili ya soka pia ni wengi. Kwa hiyo, jibu la swali nililozua hapo awali iwapo soka ya Ufarasa inakufa linajibiwa kwamba si kweli.

Badala ya kufikiri kwamba soka ya Ufaransa inakufa, ni sahihi kueleza kwamba fedha inayotoka Uingereza inaidumisha soka ya Ufaransa. Kwa maneno mengine hapa ni kwamba ubepari upo kazini na kwamba Ufaransa haitakiwi hata kidogo kuogopa nguvu za soko za uhitaji na ugavi.

Klabu za Ufaransa sasa zimekumbatia utandawazi kwa faida yao. Watu wao wamekuwa makini na kujituma katika kuchungua utajiri ulio upande mwingine wa Ulaya, yaani Uingereza, huku wakitumia ukarimu wa jirani zao hawa kuchangia kwenye maendeleo ya muda mrefu wa soka nzuri ya Ufaransa.

Ilivyo ni kwamba fedha hizo za EPL zinazoingia Ufaransa, kwa kiasi kikubwa zinatoka kwa walaji wa Uingereza walio tayari kulipa zaidi ili kuunganishwa kwenye matangazo ya mpira kwenye televisheni wazione timu zao. Soka ya ngazi za chini ya Ufaransa inagharimiwa na washabiki wa Uingereza wanaopenda kujituliza kwenye kiti wakiangalia mpira kwa raha zao. Naona kuna kitu cha kufurahia hapa juu ya jinsi ukarimu wa Ligi Kuu ya England unavyoweza tena kuwa wa Ufaransa. Yadumu makubaliano haya ya kirafiki.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

MICHUANO YA KOMBE LA LIGI:

Tanzania Sports

SIMBA v. YANGA: TUSUBIRI DAKIKA TISINI