Azam na Yanga watashuka dimbani leo siku ya Jumamosi uwanja wa taifa kusaka alama tatu kila mmoja
Ni mchezo muhimu hasa kwa upande wa Yanga kuliko Azam ili kuendelea kufufua matumaini ya kutetea matumaini ya kunyakua taji kwa mara ya tatu mfululizo.
Timu zote mbili zinatarajiwa kuwakosa nyota wake muhimu wa kikosi cha kwanza kutokana na majeruhi wanayo uguza, Ngoma, Tambwe, Yondani kwa upande wa Yanga wanatarajiwa kukosekana huku Bocco, Kapombe, Kingue kwa upande wa Azam nao watahukosa mchezo huo
Makala hii inakuletea wachezaji wa kuchungwa kuelekea mchezo wa Yanga na Azam.
Simon Msuva
Kinara wa mabao Ligi Kuu kwa mabao yake 12, Msuva ndiye mchezaji hatari kwa sasa hapa nchini kasi yake, krosi murua na umakini wa kufunga amekuwa akiwapa tabu mabeki wengi hivyo safu ya ulinzi ya Azam inaitaji umakini wa kumdhibiti
Ramadhani Singano
Tangu apewe nafasi kwenye kikosi cha kwanza, nyota huyo ameonesha samani yake, katika mechi 4 za hivi karibuni amefunga magoli 2 na kusaidia mengine mawili
Obrey Chirwa
Ni mshambuliaji mwenye kasi na mzuri kwenye mashambulizi ya kushutukiza, ana tazamiwa kuwa mwiba kwa Azam kama asipowekewa ulinzi dhabiti wa kumzuia
Yahya Mohammed
Ana tazamiwa kuziba pengo la Bocco ambaye atakosekana kwenye mchezo huo, kutokana na makosa ya safu ya ulinzi ya kucheza mipira ya krosi anaweza kuwaletea madhara sababu ni mzuri kwenye mipira hiyo
Juma Abdul
Licha ya kucheza nafasi ya mlinzi ila beki huyo ana sifika kwa kutengeneza nafasi nyingi za kufunga kwa krosi zake nzuri, Gadiel Michael anaitaji kuwa makini kutompa nafasi Abdul ya kupanda na kupiga krosi