in , , ,

VITA USAJILI ENGLAND:

John Stones

 

*Man City £47m kwa De Bruyne

*Chelsea  £30m za John Stones

*Real Madrid wanamjia De Gea

Baada ya mechi moja moja kwenye Ligi Kuu ya England (EPL) iliyoanza wikiendi hii klabu zinaonekana kudhamiria kuimarisha vikosi vyao, na tayari madau makubwa yametengwa kukamilisha kazi.

 

Mpango mzima kwa Manchester City sasa ni kumpata kiungo mshambuliaji wa Wolfsburg, Kevin De Bruyne, ambapo tayari wamepeleka Ujerumani ofa ya pauni milioni 47 kumnasa, ili awe ingizo lao la tano kiangazi hiki.

 

Inatarajiwa kwamba baada ya dau hilo kupokewa na wakuu wa Wolfsburg kukaa chini, De Bruyne, 24, atawasilisha rasmi ombi kwao kwamba anataka kuondoka katika Bundesliga kwa ajili ya kujiunga na Man City.

 

Chelsea wameandaa pauni milioni 30 kwa ajili ya kukata kiu yao ya kusajili beki wa kati kujiimarisha eneo hilo linaloelekea kupwaya, na bado mawazo yao yapo kwa mlinzi wa kimataifa wa England, John Stones anayekipiga Everton.

 

Stones, 20, anawaniwa kwa udi na uvumba na The Blues, huku kukiwa na sauti kutoka pande mbalimbali, ikiwa ni pamoja na wanasoka wastaafu wakimshauri cha kufanya, baadhi wakimtaka abaki Goodison Park huku wengine, kama Rio Ferdinand, wakidai pazuri kwake ni Manchester United.

 

Chelsea wanakaribia kumsajili beki wa kushoto wa Augsburg, Baba Rahman, 21, katika dili linalotarajiwa kugharimu pauni milioni 21.7.

Baba, ananyemelewa na Chelsea.
Baba, ananyemelewa na Chelsea.

 

Kocha wa Everton, Roberto Martinez ameshaeleza kukasirishwa kwake na jinsi Chelsea wanavyozidi kumng’ang’ania Stones, kitendo cha John Terry wa Chelsea kumzungumzia kinda huyo hadharani na kwa ujumla dirisha la usajili kubaki wazi licha ya ligi kuwa imeshaanza.

 

Hata hivyo, katika kuhakikisha hawabaki hivi hivi iwapo watashindwa kuhimili shinikizo la matajiri hao wa London, Toffees wanaandaa mpango wa kumpata mlinzi wa AC Milan, Cristian Zapata, 28, ili kuziba pengo.

 

Hatima ya kipa namba moja wa Manchester United, David De Gea inadhaniwa kwamba ipo karibu, kwani Real Madrid wamewasilisha mezani Old Trafford dau la pauni milioni 21.2 kwa ajili ya kumsajili kipa huyo.

 

De Gea, mzaliwa wa Madrid na aliyekuwa anakipiga Atletico Madrid kabla ya kusajiliwa United, aliwekwa kando kwenye mechi ya kwanza ya msimu Jumamosi hii dhidi ya Tottenham Hotspur, kocha Louis van Gaal akieleza kwamba hakuwa timamu kuhimili mechi hiyo.

 

De Gea, 24, amekuwa gumzo kwa muda mrefu, ambapo Man U walijaribu kumtumia ili kufanikisha kumpata mlinzi wa kati wa Real Madrid, Sergio Ramos, lakini Madrid walikataa, kocha Rafa Benitez akisema haendi popote.

 

Stoke wanapanga kuvunja rekodi ya usajili klabuni hapo kwa kumtwaa kiungo wa Inter Milan kutoka Uswisi,  Xherdan Shaqiri, 23, wakiongeza dau lao hadi pauni milioni 12, ikiwa ni mara ya tatu wanaonesha dhamira ya kumchukua.

 

Spurs nao wameonesha nia ya kumchukua mshambuliaji wa Manchester United, Javier Hernandez, 27, ambaye msimu uliopita alikuwa kwa mkopo katika klabu ya Real Madrid.

 

Wanafikiria pia kuongeza mshambuliaji kwa kumsajili mchezaji wa Cameroon mwenye umri wa miaka 21, Clinton N’Jie kutoka Lyon.

 

Liverpool wanasikiliza ofa za klabu kwa ajili ya kiungo Mbrazili, Lucas Leiva, 28, ili wafidie mamilioni ya pauni walizotumia kusajili wachezaji kiangazi hiki na pia kupunguza leja ya mishahara Anfield.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Rufaa hii imetupwa…..

UBINGWA SUPER CUP: