in

UEFA ya kutisha kuwadia mwaka 2024

UEFA

Wakati kukiwa na vuguvugu la kuanzishwa Super League barani Ulaya, Shirikisho la Soka barani humo limetangaza kufanya mabadiliko makubwa ya Ligi ya Mabingwa.

Super League ni vuguvugu linalowahusisha viongozi wa timu kubwa barani Ulaya ambazo zinataka kuanzisha Ligi yao kwa maslahi yao pamoja na kuendeleza mchezo wa kandanda dunaini.

Florentino Perez rais wa Real Madrid ni miongoni mwa wadau wakubwa wa kuanzishwa Super League, huku akiungwa mkono na viongozi wenzake kutoka timu vigogo barani Ulaya.

Shirikisho la Soka barani Ulaya UEFA limekuwa likipinga mpango huo na kudai utakuja kuvurugha ladha ya soka barani humo. hata hivyo vigogo wa Super League wanaamini njia pekee ya kuwazuia ni kuongeza malipo ya fedha kwa washindi, kuongeza haki za televisheni na marupurupu mbalimbali yatakaowafanya vigogo hao kusitisha mipango yao.

Hadi sasa Super League haijafutwa wala kuanzishwa lakini vuguvugu lake si jambo dogo. Kutokana na hatua hiyo UEFA sasa imepanga kuja na muundo mpya wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ikiwa ni njia ya kuongeza ladha na kuchochea ushindani pamoja na manufaa ya kiuchumi miongoni mwa vilabu nan chi wanachama.

JE MUUNDO MPYA UTAANZA LINI?

Tanzaniasports unafahamu kuwa UEFA imepanga kuanzisha muundo mpya wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ambaomunatarajiwa kupitishwa ifikapo mwezi Machi mwaka huu wa 2021 ambapo Ligi ya Mabingwa itakapoanza kunguruma msimu wa mwaka 2024 utakuwa na mwelekeo mpya ambao utachochea timu nyingi kuonesha umahiri wao?

MUUNDO HUO NI UPI?

Kwa mujibu wa taarifa ambazo Tanzaniasports imepata ni kwamba Shirikisho la soka Ulaya UEFA limepanga kuongeza timu za kushiriki hadi 36.

Kwa muundo mpya maana yake timu shiriki 36 zitapatikana katika Ligi Kuu za nchi zao ambao ni wanachama wa UEFA. Muundo huo utategemea Ligi za nchi kama zilivyo sasa bila kuongeza idadi ya timu kwenye ligi hizo lakini kwa kutocheza mwishoni mwa wiki ama kupunguza idadi ya timu,

Sababu za kubadilisha muundo wa sasa ni kutokana na hatari ya kuanzishwa Super League kama tulivyoeleza hapo mwanzoni.

MASHARTI YA UEFA

UEFA inafahamu kuwa inatakiwa kufanya mabadiliko katika muundo wa Ligi ya Mabingwa kwa sasa, lakini wataheshimu maeneo makuu matatu; kwanza, kuendelea kuchezwa katikati ya wiki; pili, kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa itatokana na msimamo wa timu katika Ligi kuu za nchi husika; tatu,idadi ya timu zitakazoshiriki Ligi Kuu katika nchi zao zinatakiwa kuwa zilezile, ikiwa na maana katika Ligi ya nchi fulani inazo timu 18 au 20 zitalazimika kuwa na idadi hiyo hiyo bila kupunguza wala kuongeza.

UEFA imebainisha kuwa muundo mpya utafanyika kwa kipindi cha miaka mitatu hadi mwaka 2033.

TIMU ZA KUSHIRIKI

Katika hatua nyingine Tanzaniasports imeambiwa na UEFA kuwa timu zitakazoshiriki Ligi ya Mabingwa kwa muundo mpya zitakuwa tano au sita kwa kila nchi, na nafasi nyingine nne za ziada zitatolewa kwa utaratibu ufuatao; timu mbili kutokana na kiwango cha ubora kwa mujibu wa UEFA, moja itaingia katika nafasi ya Ligiya tano kwa ubora ambayo ni Ligue 1 ya Ufaransa, na timu nyingine itapata nafasi kutoka Ligi bora anbayo haina mwakilishi kwenye Ligi ya Mabingwa.

MUDA WA KUCHEZA

Awamu ya kwanza ya kushiriki mashindano hayo itakuwa kutoka mwezi Septemba hadi Januari, na kila timu itacheza mechi 10 dhidi ya wapinzani tofauti.

Timu nane zitakazofanya vizuri zitakuwa zimefuzu kuingia raundi ya 16, na nafasi ya 9 hadi 24 timu zitachuana katika mechi za mtoano kupatikana timu zingine nane za kuingia hatua ya 16. Kama ilivyo kawaida mechi zitachezwa siku za jumanne na jumatano, na vile vile siku ya alhamis zitakuwa mechi nne za Ligi ya Mabingwa Ulaya.

USHINDANI

Kwa utaratibu huu UEFA inaleta ladha ya ushindani mkubwa kuanzia ngazi za chini hadi juu. Kuwapa nafasi timu inayotoka Ligi bora kwa mujibu wa viwango vya EUFA wenyewe maana yake wamepanua uwakilishi barani Ulaya.

Kwa mfano chukulia timu za nchi kama zile Austria, Romania, Uswisi, Sweden, Urusi, Slovenia, Czech, Latvia, Ugiriki, Norway, Denmark kwa kutaja chache huwa hazifui dafu, na hiyo haina maana kwamba hawana timu nzuri, lakini kwa muundo huu bila shaka kutakuwa na mabadiliko kwenye kandanda. Ushahidi wa kuwepo kwa timu zingie zenye ushindani ni Europa League ambako nyingi zimekuwa zile kutoka mataifa ya niliyoeleza hapo juu, na ambazo zimekuwa zikitetemesha zile kubwa zinazodondekea ligi hiyo.

Kwa kawaida na imekuwa hivyo kwa miaka mingi timu za England, Hispania, Ufaransa, Ujerumani,Italia zimekuwa zikitamba kwenye mashindano hayo miaka mingi au kupokezana kutwaa ubingwa wa UEFA kila msimu.

Ubingwa wa UEFA unaweza kutwaliwa Hispania kisha ukahamia Ujerumani, ukarudi Italia na baadaye ukaenda England, kabla ya kurejea tena Hispania. Kunyang’anyana huko kuna maana kuwa timu zingine zinakuwa hazina nafasi. Naamini Ligi za nchi zingine nazo ni bora kama nilivyotaja hapo juu.

Kwa muundo huo wa kushirikisha timu nyingi naamini kabisa utaamsha ari ya kandanda kwa mataifa megingine ambayo kila msimu yalikuwa ya wasindikizaji. Kwahiyo nafasi 36 ni fursa ambayo kila timu kutoka Ulaya inatakiwa kuitumia. Kuwa na mechi nyingi maana yake uwekezaji na manufaa ya kiuchumi yataongezeka.

Na zaidi muundo huu unakwenda kushusha presha ya kuanzishwa kwa Super League kwani kuhusisha timu nyingi Ligi ya Mabingwa kutatanua utazamaji na kuongeza mapato kutoka mataifa mengine kwa msimu.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Kina Ajib hawaoni wivu kwa kina Chama ?

JO

Amsha amsha ya wageni kuwazindua wazawa?