in , ,

Uefa na Fifa wamechelewa: Urusi wamemaliza

Chelsea vs Liverpool

Tumechezewa kiakili kiaina na Vladimir Putin na sasa anachakaza watu na kuua huko Ukraine, na michezo ilitimiza lengo lake la kuweza sasa kujijengea wakati huu wa kutisha wengine.

Mpango ni kama umekamilika. Ingia chakulani, kusanya vito, chukua vilivyotawanywa na hakika michezo imewezesha kilichokusudiwa hapa na chochote itakachoamua kufanya kutoka hatua hii ni kwa hakika kwamba Putin wala hatakuwa akisikiliza tena.

Asanteni Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Shirikisho la Soka la Ulaya (Uefa), Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) na washirika wetu wengi wa kimataifa kwa msaada wenu kwa ujumbe, hiyo imefunikwa.

Ni vigumu kumaizi kipi chakufanya juu ya habari kwamba Uefa wamepanga kuhamisha fainali  za Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) kutoka St Petersburg, mji wa nyumbani kwa Putin kama namna ya kutokubaliana na kitendo cha Putin kuivamia Ukraine. Hii, bila shaka, ni hatua ya lazima.

Hata hivyo, eneo ambalo fainali zimepelekwa wakati risasi zikirindika Kyiv ni jambo linaloacha ukakasi na linatakiwa kutazamwa nasi wote, kuanzia mashirikisho ya soka hata yale yasiyokuwa na uti wa mgongo hadi kwa wale wasiokuwa na uelewa, achilia mbali wenzetu wa vyombo vya habari walio hapa.

Tanzania Sports
St Petersburg’s Gazprom Arena

Mtu pekee anayeonekana kwamba anatofautiana na kamati maalumu ya Fifa iliyokutana Ijumaa ni Alexander Dyukov, Rais wa Shirikisho la Soka la Urusi na Mwenyekiti wa Bodi ya Gazprom, japokuwa hata yeye hatakuwa akijali sana kwa wakati huu. Kuna uwezekano wa Schalke kuondoa nembo ya Gazprom kwenye jezi zake na Uefa huenda wakafikiria upya dili la udhamini wa wazalisha gesi wa Urusi.

Lakini siku tayari zimesogea na mchango wa michezo umeonekana. Biashara, siasa na burudani za kuoneshwa michezo kwenye televisheni vimefanya yao. Urusi ya Putin imepata ushawishi, mamlaka laini na uhalali, umma wa nyumbani umetulizwa. Sochi na Moscow zimegawa mdogo mdogo kwa watumishi waaminifu wa Putin.

Tupo kwenye hatua ambayo ni kana kwamba kuhamisha kituo cha fainali zile ni kama kutegemea kuokoa aliyekwisha elekezwa kooni na wanaume waliovaa barakoa ambao tayari wamepanda ngazi na kufika nusu wakiwa na silaha. Putin tayari anamwaga mvua ya vifo kwa watu wa Ukraine, hajali, katika hatua hii, kwamba ni wapi hasa soka inaenda kuchezwa.

Ikiwa soka inaweza kujifunza lolote kutokana na kitisho hiki ni kwamba sasa tunajua sana kuwa pasipo shaka yoyote hili ni la ukweli. Kwamba wale wanaozungumza kwa kuchoka, mchezo upo sasa, juu ya udikteta na haki za binadamu vinazungumzwa kutoka sehemu hasa inayodhurika.

Hali ya mkanganyiko kisoka, bila shaka, inaanzia kwenye makao makuu ya Fifa nchini Uswisi. Tayari Rais wa Fifa, Gianni Infantino tayari ametoa kauli yake inayokwenda mbali sana, akipinga machafuko pasipo kutaja jina la Putin wala Urusi, akisema waliamka na kushitushwa na kile walichoona.

Historia itamhukumu Infantino kwa ujumla kuhusu matendo yake. Tukumbuke kwamba miaka mitatu iliyopita Infantino alikuwa Ikulu ya Kremlin (Urusi) akitamka kwamba ulimwengu sasa ulikuwa katika mapendo na Urusi, huku akimkumbatia Putin kama kama yake, na walikuwamo pia Rio Ferdinand na Peter Schmeichel.

Mwaka mmoja baadaye,  rais huyu wa Fifa alirejea kule kwa ajili ya mawasilisho ya medali kwa taifa hilo.

“Uliukaribisha ulimwengu kama marafiki … ulimwengu umejenga fungamano na upendo na Urusi litakalodumu daima,” Infantino alimwambia rais huyu huyu Putin ambaye kwa sasaamepeleka jeshi kubwa zaidi hapo Ulaya kuliko ilivyopata kuwa tangu Vita ya II ya Dunia.

Infantino aweza kuwa amejionesha kuwa mtu wa kuchekwa, lakini somo hilo ni la karibu sie wote pia, somo katika kitu kigumu na baridi yabisi katika mchakato ambao haukueleweka ungeishia wapi. Amnesty International ni kati ya wale walioanzisha usemi wa kutumia michezo kujisafisha miaka mine iliyopita.

Mwaka 2018, katika makala Fulani juu ya Abu Dhabi, Manchester City na suala la Matthew Hedges walitumia usemi huo katika fungo, na walitenga muda kueleza ulitokana na nini.

Wakati mwingine imekuwa ikionekana kama propaganda, lakini hakuna namna ya kujificha kutoka kule ambao ukweli unaweza kuelekeza, mchakato ambao wengi wetu tungeweza kupendelea. Baada ya Fainali za Kombe la Dunia kiliandikwa kitabu juu ya kutembea sehemu mbalimbali nchini humo na kukutana na Warusi katika maisha yao ya kila siku.

Kukutana nao na kujua hali zao ni kwamba kwa uhakika ni kuwa Putin ni muaji na dikteta na ukweli ni kwamba Fainali za Kombe la Dunia zilikuwa moja ya mipango yake kiutawala. Na Urusi imekuwa ikicheza hivyo katika hatua mbalimbali. Miaka minne iliyopita, bungeni nchini England kulikuwa na mwito wa kugomea Kombe la Dunia baada ya suala la kulishwa sumu kule Salisbury.

Hata hivyo, kwa wakati ule ilikuwa ngumu kuona sababu na athari ambazo zingeweza kuwa kwa Urusi.

Katika kitabu chake ‘Putin’s People’, Catherine Belton anaandika juu ya maeneo ya kifedha na kisia ya Uingereza juu ya Urusi, pale London ilipotokea kujulikana kama ‘Moscow-on-Thames’, miaka ile ya meli za kifahari na ndege.

“Katika miaka ya kati ya 2000 London ilikuja kupata sifa ya kuwa kituo cha dunia cha kusafisha mabilioni ya pauni chafu. Njia ilikuwa imefunguliwa kwa KGB kujipanga na kufanya kazi yao kwa urahisi kuliko mtandao waliokuwa wameweka kabla enzi za Sovieti,” akaandika Belton.

Tajiri wa Kirusi ananukuliwa akisema: “Kule London, fedha zinatawala kila kitu. Kila mmoja na kila kitu vyaweza kununuliwa. Warusi walikwenda Londonkuwatia doa wanasiasa wa Uingereza.”

Je, hii ni kweli, ikiwa ndivyo, ni kwa vipi? Ukweli ni kwamba walio madarakani Moscow wanaamini hivyo, inawezekana kabisa kuwa ndiyo eneo sahihi la kuanzia. Na ndiyo, michezo ni eneo dogo tu katika haya, japokuwa hupanda juu sana katika masuala ya dunia. Lakini hiyo ndiyo thamani ya propaganda tunayojidai kujipa nafasi za mbele.

Katika Fifa House kule Zurich 2010 ilishuhudiwa Putin akiingia, ikashitusha watu kiasi kutoka nyuma ya kile chumba cha mkutano wa waandishi wa habari, kwa ajili ya kupokea na kujibu maswali ya waandishi wa habari baada ya Urusi kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia.

Alionekana mdogo na mpweke peke yake akiwa pale lakini mwenye kujiamini. Leo hii Ukraine wanaomba klabu za Urusi ziondolewe kwenye mashindano ya Uefa na hiyo ifanyike haraka.

Na kuanzia sasa tumeshaonywa. Tunajua, pasipo shaka yoyote kipi kitafuata. Vlad hatakuwa akijibu wala kumpigia tena simu Infantino, wala kuhangaika na voicemails zake. Mchezo umeisha, tumeshachezewa tayari.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Kwanini Marefa wa Tanzania hawachezeshi AFCON ?

Tanzania Sports

Soka inaanza kuamka