Wakati ligi Kuu Tanzania Bara ikitarajia kuendelea kuchezwa raundi ya tatu wiki hii vigogo Yanga, Simba na Azam nazo zitakua na jambo lao.
Yanga
Mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu Bara timu ya Yanga ama Wananchi kama wanavyojiita watakuwa na kibarua ugenini watachuana na Kagera Sugar katika uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.
Mchezo huu utakuwa mgumu hasa kwa Kagera Sugar kukosa matokeo mazuri katika michezo yake ya iliyopita, ilitoa sare ya 0-0 ilipocheza na Gwambina huku ikipoteza 1-0 dhidi ya JKT Tanzania, licha ya matokeo mabovu watengeneza sukari hawa wanapokutana na Yanga mchezo unakuwa mgumu sio rahisi kutabiri mshindi.
Katika michezo miwili ya msimu uliopita Yanga alichezea magoli 3-0 raundi ya kwanza na kushinda mchezo wa pili uliochezwa uwanja wa Kagera kwa goli 1-0 goli la Morrison.
Kikosi cha Kagera Sugar kimesheheni wachezaji wazuri wenye uzoefu.
Yanga ambayo inawachezaji wapya baada ya kupitisha fagio la kuwaondoa wachezaji 14 katika dirisha la usajili lililopita bado wanatimu yenye ushindani.
Wachezaji wapya wanauchu wa kupambania namba huku kila mchezaji akitaka kuonekana ili kocha mkuu wa timu hiyi apate kumpa nafasi ya kucheza kila wiki.
Wafungaji wa Yanga ni Michael Sarpong ingizo jipya pamoja na Lamine Moro.
Jumatano timu hiyo ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mlandege na kushinda kwa magoli 2-0.
Mchezo wao utachezwa siku ya Jumamosi majira ya saa kumi jioni.
Ikitoka hapo itachuana na Mtibwa Sugar uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Hivyo kama kuna mtu anataka kuweka mzigo atulie kwanza na aangalie hadi mchezo ukitaka kuanza kikosi kitakachopangwa ndio atabri.
Simba SC
Mnyama Simba ameshinda mchezo wake wa kwanza dhidi ya Ihefu FC ambao wamepanda msimu huu kwa magoli 2-1.
Imetoa sare ya goli 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar mbungi imepigwa uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
Simba itahitaji kutumia vizuri uwanja wake wa nyumbani baada ya kupoteza alama mbili katika michezo miwili ya kwanza siku ya Jumapili itacheza na Biashara United.
Mnyama Simba inajiandaa na michunao ya kimataifa lazima ihitaji kuonesha ukubwa wake na kujiweka sawa hivyo ni wakati wa Sven kupanga karata zake vizuri.
Maoni ya watu mbalimbali wanasema kuwa licha ya Simba kutobadilika sana kwa wachezaji ila ya msimu huu bado haijakuwa moto kama ile iliyopita kwa namna inavyocheza mechi zake.
Biashara United imetoka kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Mwadui FC pia ilishinda goli 1-0 dhidi ya Gwambina FC.
Hivyo mchezo utakuwa mgumu kwa pande zote embili hasa Biashara United itakuwa inajiamini kuwa wawnaweza kufanya jambo mbele ya bingwa mtetezi huku wakijua ukweli kuwa Simba inawachezaji wazuri sana.
Simba itaondoka na alama zote tatu katika mchezo huu weka mzigo mapema tu.
Azam FC
Azam FC moja ya timu tajiri hapa Tanzania huenda Afrika Mashariki imejaribu kuingia katika utawala wa ligi kuu bara kwa kuchukua mara moja msimu wa 2014.
Imepata ushindi mechi mbili mtawaliwa ilicheza na Polisi Tanzania ilishinda goli 1-0 kwa taabu na mchezo wa pili dhidi ya Coastal Union ilishinda magoli 2-0, magoli yote yakifungwa na Prince Dube.
Azam watachuana na Mbeya City iliyopoteza mechi mbili za mwanzo.
Ka namna tulivyoiangalia Mbeya City ilivyocheza na Yanga kama itacheza kwa nidhamu ile dhidi ya Azam FC patakuwa hapatoshi.
Mchezo huu nauona mgumu na naweza kuthubutu kusema sare ya magoli 2-2.
Coastal Union v Dodoma Jiji
Dodoma Jiji ambayo imekusanya alama 6 katika michezo yake ya mwanzoni itakwaana na Wagosi wa Kaya kutoka Tanga Coastal Union.
Coastal haijaambulia pointi yoyote katika michezo mwili japo inaonekana inacheza kitimu, Dodoma Jiji itakuwa kipimo halisi kwao.
Bado naendelea kuiamini Dodoma Jiji itaweza kuvuna alama katika mchezo huo au hata kutoa sare maana itakuwa ugenini.
Polisi Tanzania v JKT Tanzania
Hawa maafande wote mmoja mwanajeshi mmoja polisi, mechi hii itakuwa tamu sana hasa kwa viwango vya timu zote mbili.
Bado nafasi kubwa naipa Polisi Tanzania kwa mpira wake na mechi mbili iliyocheza inaonekana kuimarika na bado kutakuwa na timu ya ushindani sana.
Japo zote zina alama tatu kwa kushinda mchezo mmoja mmoja katika raundi mbili bado mchezo utakuwa mgumu na mzuri wa kutizama wiki hii.
Ihefu FC V Mtibwa Sugar
Ihefu itakuwa nyumbani ilipoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Simba ambayo ubora wake kila mmoja anafahamu ila ilionesha mchezo mzuri, ikacheza raundi ya pili ikaibuka na alama tatu muhimu.
Mtibwa ilivuna alama moja katika mchezo wa kwanza na ikavuna moja katika mchezo wa pili bado itakuwa mechi kali sana.
Bado naamini Ihefu ataondoka na amatokeo katika mchezo huo kwa uwezo wao na kujiamini licha ya kuingia katika ligi msimu huu.
Mwadui v KMC
‘Kino Boy’ KMC haitaki masihara msimu huu mechi mbili imevuna magoli 6 hakuna timu nyingine iliyofanya hivyo hadi sasa.
Itaenda kuvaana na Mwadui ambayo ilibanduliwa goli 1-0 dhidi ya Biashara united mchezo uliopita wanakutana na KMC ambayo inaonekana kuhitaji nafasi za juu.
KMC itaondokana ushindi ama alama moja katika mchezo huu ambao mgumu.
Tanzania Prison v Namunog FC
Mchezo mwingine mzuri wa kuangalia kila timu ina aina yake ya uchezaji huku Prisons ikiaminika kucheza mpira wa nguvu na kushambulia tatizo umaliziaji wakati Namungo ikiwa na wamaliziaji wazuri bado sehemu ya ulinzi haijakaa poa.
Mechi hii inaenda patulo watagawana alama kutokana na vikosi vyote viwili nilivyo vitazama.
Ruvu Shooting v Gwambina
Ilitoa sare mchezo wa kwanza na kufungwa uliofuata wanajeshi kutoka mkoani Pwani Ruvu Shooting mbele ya kocha wao Mkwasa watakuwa na shughuli nyingine kuwakwaruza Gwambina ambayo inayo haikufanya vizuri mchezo wa kwanza.
Ruvu Shooting inaenda kumpapasa Gwambina katika mchezo huu.
Tuwakumbushe tu hadi sasa magoli 27 yamefungwa katika raundi mbili Yanga, Simba na Azam zikichangia magoli 8 .
Enock Jiah anabaki kuwa ndiye aliyefunga goli la mapema zaidi ikimuacha Lambert Sabiyanka wa Tanzania Prisons, Jiah amefunga goli dakika ya 7 wakati Ihefu FC ikichuana na Ruvu Shooting, lile la Sabiyanka alilifunga dakika yya 8 dhidi ya Yanga.
Comments
Loading…