in

Ubora wa Miraji unafichwa kwenye udhaifu wa Chikwende

SIMBA SC

Ilikuwa mechi kati ya FC Platnumz na Simba SC iliyochezwa kwenye ardhi ya Robert Mugabe, ardhi ambayo Robert Mugabe na wenzake waliamua kuiita Zimbabwe. Mechi hii iliwakutanisha watoto wa maswahiba wawili wakubwa duniani.

Maswahiba ambao waliwahi kushikamana kwa pamoja ili kuhakikisha bara la Africa linakombolewa. Ni ngumu sana kwa mtu yoyote kutolihusisha bara la Afrika na watu kama Mwalimu Julius Kambarage Nyerere pamoja na Robert Mugabe.

Hawa ndiyo moja ya miamba mikubwa ya Afrika. Hawa ni nembo, nguzo ambazo zishabomoka lakini bado tunaishi na busara zao. Busara ambazo zimebaki kwa faida ya vizazi mbalimbali.

Tanzania Sports
Perfect Chikwende

Ligi ya mabingwa barani Afrika iliwakutanisha watoto wa wazazi wakubwa kuwahi kutokea duniani (Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Robert Mugabe).

Kwenye mechi iliyochezwa mjini Harare huko Zimbambwe, FC Platnumz ya Zimbabwe iliifunga Simba SC ya Tanzania kwa goli moja kwa bila.

Inshu kubwa haikuwa FC Platnumz kushinda ila inshu kubwa ilikuwa kwa mfungaji wa goli hilo ambaye alikuwa ni Perfect Chwikwende. Kwenye mechi hiyo alionesha kiwango kikubwa sana.

Kiwango ambacho kiliwavutia Simba SC mpaka wakaamua kumsajili. Usajili ambao mpaka sasa hivi unaonekana ni usajili wa kawaida kwa sababu hajawahi kuonesha kiwango kikubwa tulichokuwa tunakitarajia.

Kiwango ambacho kingetufanya tusiwe na mashaka hata kipindi ambacho anamweka benchi Miraji Athumani “Chogo”.

Miraji Athumani huyu huyu ambaye alikuwa mfungaji bora wa michuano ya mapinduzi Zanzibar iliyofanyika mwezi wa kwanza.

Miraji Athumani ana jicho zuri la goli pamoja na uwezo mzuri wa kutengeneza nafasi za magoli kuzidi Perfect Chikwende.

Inawezekana uwezo wa Miraji Athumani unafichwa na jina la Perfect Chikwende. Jina ambalo lilianza kututisha tangu akiwa Zimbambwe.

Kwa bahati mbaya inawezekana hatukumfuatilia vyema kabla ya kumsajili. Hatukutaka kujipa muda wa kumtazama kama anauwezo mkubwa kuzidi hata wachezaji wazawa.

Perfect Chikwende inawezekana kitu pekee kinachompa nafasi Simba SC mbele ya Miraji Athumani ni uraia wake. Ni mchezaji wa kigeni lakini hakuna kingine cha ziada kinachompa nafasi Perfect Chikwende mbele ya Miraji Athumani.

Taifa lefu linahitaji wachezaji watu wacheze mara kwa mara ili tunufaike kwenye timu ya taifa. Wachezaji wetu wengi wana viwango vikubwa kuzidi wageni.

Pamoja na kuwa na viwango vikubwa kuna kitu kimoja ambacho wanakabiliana nacho. Neno “wachezaji wa kigeni”  linawaficha sana baadhi ya wachezaji wetu.

Siyo kwamba wachezaji wa kigeni wote siyo wazuri, hapana. Ila kuna baadhi ya wachezaji wa kigeni ambao viwango vyao ni vya kawaida na havizidi viwango vya wachezaji wa ndani.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Sarpong

Nchimbi na Sarpong wataipa Yanga SC ubingwa ?

Wazir Wazir Jr

Yuko wapi Wazir Jr ?