in

Tyson, Mwakinyo Kuunganishwa Na Ngumi

Mchezo wa ngumi umekuwa kwa kasi kubwa sana hapa Tanzania hii inatokana na vyombo vya habari kuutilia maanani mchezo huo.

Ukitaka kuamini kama mfanano wa mchezo wa ngumi ndio unaleta kwa pamoja mabondia wote duniani kuzunguzwa kwa pamoja, leo hii Tyson na Mwakinyo tunawaelezea kwa habari moja yenye muunganiko.

Bila choyo tuipongeze Azam TV kwa kuurudisha mchezo huu katika ramani yake, wale wa zamani watakuwa wanafahamu mchezo hu ulivyokuwa na wadau wengi pamoja  na mvuto mkubwa.

Ndio maana mapambano mbalimbali yanaongezeka wakati huo mabondia kutoka nchi za nje wanakula nakozi wanarudi kwao.

Ukitaka kupima au kujua nani anaongelewa zaidi hapa Tanzania au yupi ni bora unaweza kuweka mjada mkubwa sana kati ya mashibiki wa mabondia hao.

Hadi kufikia leo hii bondia Hassani Mwakinyo mkazi wa Tanga yeye ndio namba moja kwa uzito wa kilogram 69 akfuatiwa na Twaha Kiduku wa Morogoro.

Katika nafasi za tatu na kuendelea unaweza kuweka wako ila yupo Abdallah Pazi akifuatiwa na  Mfaume Mfaume pamoja na Ibrahim Class katika zile tano bora zangu.

Sasa leo kazi yangu kukupa habari mbalimbali za mchezo huu zilizotokea wiki nzima na zinazoenda kutokea.

Tyson dhidi ya Roy Jones JR

Tanzania Sports
Mike Tyson

Kwa mara ya kwanza tangu mara ya mwisho mwezi Juni mwaka 2005, apoteze pambano lake dhidi ya Kevin McBride, hatimaye bondia bingwa wa zamani aliyewahi kushikilia mataji manne kwa pamoja ya WBC,WBO,IBF na WBA (Undisputed) kwa uzito wa juu MIKE TYSON atapanda ulingoni Jumamosi hiii kumvaa Roy Jones JR.

Tyson atapanda ulingoni kuzichapa na lejendari mwenzake ROY JONES JR, ambaye ni bingwa wa zamani wa dunia katika mizania minne, pambano litakaloligwa kwenye ukumbi wa Staples Center, Los Angeles Marekani

Pambano hilo la maonyesho la raundi nane, lililobeba jina la ‘FRONTLINE BATTLE’,ni onyesho la kwanza la mfululizo wa ligi ya malejendari wa masumbwi, kwa ajili ya kuwania mkanda mpya ulioanzishwa na WBC (WBC Frontline Battle Belt).

Kwa mujibu wa Mkurugenzi mtendaji wa California State Athletic Commission (CSAC), Andy Foster, Tyson na Jones hawatovaa kikinga kichwa (headgear), na pia mabondia hao watavaa gloves za 12-ounce.

Katika historia yake Tyson amecheza mapambano 50, amepoteza 6. 44 ameshinda kwa KO, ambapo taji lake la kwanza la ubingwa wa dunia la WBC alishinda akiwa na miaka 20, alipomsimamisha TREVOR BERBICK katika raundi ya pili novemba 22 mwaka 1986.

Kwa upande wa Jones yeye amecheza mapambano 66 amepoteza 9, 47 akishinda kwa KO, amewahi kushinda mataji manne ya dunia katika mizania tofauti (Middleweight, Super middleweight, Light heavyweight na Heavyweight) pia Jones anasadikiwa kuwa moja ya mabondia wenye ustadi mkubwa katika kizazi chake.

Hassani Mwakinyo atua Zanzibar

Bondi nambari moja nchini HASSANI MWAKINYO, amewasili visiwani Zanzibar kwa lengo la kuiomba serikali ya mapinduzi Zanzibar, kuruhusu mchezo wa ngumi kuchezwa visiwani humo.

Hapo zamani mchezo wa ngumi ulikuwa ukichezwa visiwani Zanzibar, lakini baadae Hayati Sheikh Abeid Aman Karume aliupiga marufuku mchezo huo kutochezwa katika visiwa hivyo.

Sababu ya kutoruhusu mchezo huo, inatajwa kwamba siku moja Mzee Karume alialikwa kama mgeni rasmi kwenye moja yapambano la ngumi, inatajwa kwamba kitendo cha kuona mabondia wanapigana kiasi cha kuumizana bila ya sababu ya msingi.

Kilimfanya muasisi huyo wa visiwa vya Zanzibar kuupiga marufuku mchezo huo, ambapo hadi leo hii mchezo huo hauchezwi visiwani humo.

Mwakinyo amesema, “Zanzibar kuna vipaji vingi sana hapa lakini hawapati nafasi ya kuonyesha vipaji vyao , kama Zanzibar wataruhusu mchezo huu basi Zanzibar itatowa mabondia wakubwa na wakimataifa.

Yapi maoni yako mdau wa ngumi?

Callum Smith v Canelo Alves

Bondia  ambaye ni bingwa wa dunia wa taji la WBA uzani wa super-middle, CALLUM SMITH anataraji kupanda ulingoni Desemba 19 mwaka huu kuzichapa dhidi ya mpinzani wake ‘CANELO’ ALVAREZ.

Pambano hilo ambalo limepangwa kufanyika nchini Marekani katika terehe hiyo ikiwakutanisha miamba hiyo ya uzani wa super-middle,bado sehemu (Ukumbi) itakayopigwa pambano hilo haijawekwa wazi.

Alvarez ambaye ni raia wa Mexico anaonekana kama moja ya bondia bora katika ndondi duniani akiwahi kushikilia mikanda ya dunia,katika mizani ya mizani minne ya uzito.

Kwa upande wa Smith, mwenye miaka 30, hajapoteza pambano katika mapambano 27 aliyocheza, akilitetea taji lake hilo la dunua mara mbili, tangu alivyoshinda taji hilo mwaka 2018 kwa kumchapa GEORGE GROVES.

‘World Boxing Council’

Shirikisho la ngumi duniani WBC ‘World Boxing Council’  ni moja kati ya mashirikisho makubwa ya ngumi duniani, yenye heshima kubwa katika tasnia ya masumbwi duniani kote.

Shirikisho hili huidhinisha taji la ubingwa la (WBC) ambalo kimsingi, linatajwa kuwa ni taji lenye thamani kubwa kuliko mataji yote makubwa yanayoidhinishwa na mashirikisho au taasisi kubwa za ngumi duniani kama WBA,WBO na IBF.

Shirikisho hili lilianzishwa mnamo Februali 14 mwaka 1963 huko jijini Mexico nchini Mexico,ambapo mataifa yapatayo 11 yalikutana nchini humo kwa lengo kuanzisha shirikisho hili (WBC).

Miongoni mwa Mataifa hayo kumi na moja nii,Marekani, Puerto Rico, Argentina, Ufaransa, Uingereza, Mexico,Ufilipino, Panama, Chile, Peru, Venezuela na Brazil.

Ambapo Wawakilishi kutoka katika mataifa hayo 11, walikutana jijini Mexico kwa mualiko maalumu wa rais wa wakati huo wa taifa la Mexico, ADOLFO LOPEZ MATEOS kuanzisha Taasisi hii ya kimataifa.

Lengo la kuanzisha shirikisho hili, lilikuwa ni kuziunganisha kamisheni zote zinazosimamia ngumi katika mataifa mbalimbali duniani, ili kutanua wigo mpana wa mchezo wa ngumi,ili kupendwa na kuchezwa duniani kote.

Kwa sasa WBC ina mataifa wanachama yanayofikia 161,miongoni mwa marais waliopata kuliongoza shirikisho hilo ni Luis Spota,Roma Velazquez,Justiniano Montono jr na Jose Sulaiman ambaye ni baba wa rais wa sasa wa WBC Mauricio Sulaiman.

Mauricio Sulaiman amerithi wadhifa huo baada ya kufariki kwa baba yake mzee Jose Sulaiman mwaka 2014,ambaye aliliongoza shirikisho hilo kuanzia mwaka 1975 hadi alipofariki dunia mwaka 2014.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Mashabiki Kurejea

Mashabiki kurejea viwanjani ni kama wametoka jela

Mike Tresor Ndayishimiye

Mipango ya Burundi iwe somo kwa sekta ya michezo Tanzania