in

TUTENGENEZE AKINA MOURINHO NA NUNO SANTO WETU!

Nuno Espírito Santo

Nafasi ya kocha mkuu wa timu ni nafasi nyeti sana katika maendeleo ya soka ya kilabu ama nchi yoyote ile. Katika vilabu vikubwa maoni ya kocha huwa yanachukuliwa kwa uzito mkubwa sana. Katika vilabu vilivyoendelea licha ya kuwa na maskauti wa kusaka vipaji ila kabla ya bodi za timu hizo kuamua kuvunja benki na kusajili wachezaji ambao wanakuwa wanaletwa mezani basi hupeleka majina yaliyopendekezwa kwa kocha mkuu na benchi lake la ufundi kwa ajili ya maoni yao na hii ndio maana mara nyingi bodi ikilazimisha kumsajili mchezaji ambaye hakuwa chaguo la kocha mkuu na benchi lake la ufundi basi amekuwa ni kawaida kwake kupata mapokezi ambayo sio mazuri sana kwa benchi hilo na mda mwingine hujikuta huyo mchezaji ima akikosa fursa za kucheza ama kutochezeshwa kabisa.

Kama taifa linataka kusonga mbele kisoka lazima lijiandae vyema kuwa na makocha ambao wataweza kwenda kuvuka nje ya mipaka ya kiiinchi. Yaani kama tutaweza kuwa na makocha ambao wataweza kwenda kufundisha nchi hata za ukanda mwingine wa afrika yaani ima kusini mwa afrika au magharibi mwa afrika basi tunaweza kupeleka wachezaji wetu wengi wakacheza katika ligi za nchi hizo. Kwa kugusia hivyo kuna mataifa yamenufaika kisoka kwa kuwa na makocha ambao wameweza kutengeneza njia kwa wachezaji wa nchi zao katika mataifa ambayo wanayoyafundisha. Ureno ni mojawapo ya mataifa hayo

 Ukizungumzia makocha walioweza kujitengenezea majina yao vizuri katika soka ulimwenguni huwezi kuacha kumataja Jose Mourinho. Kocha huyu ameweza kubeba makombe mbalimbali makubwa akiwa na vilabu vya FC PORTO, INTER MILAN, REAL MADRID, MANCHESTER UNITED na CHELSEA. Kocha huyu kote huko alikofundisha basi alitengeneza mazingira mazuri kwa vijana wa kireno kupata fursa ya kucheza katika vilabu hivyo. Alipokuwa Porto msimu wa mwaka 2003-2004 aliushangaza ulimwengu kwa kubeba ubingwa wa klabu bingwa ulaya huku akiwa na timu ambayo haikutarajiwa kubeba kwani haikuwa na mastaa wa kidunia alibeba ubingwa huo akiwa na wachezaji wa kawaida tena wengi wa kireno kama vile; Deo, Maniche, ricardo Cavarlho, Pepe na wengineo wengi. Aliweza kukuza na kutangaza wachezaji hao. Alipofika Chelsea aliweza kuwasajili Ricardo Carvalho, Paulo Fereira na  Deco. Alipoenda inter milan alijaribu kuwapa nafasi wareno wenzie kama Ricardo Quaresma lakini walishindwa kufanikiwa.

Ureno imeweza kumzalisha kocha wa timu ya Wolves  Nuno Esprito Santo ambaye  katika mda aliohudumu katika kikosi hicho nchini uingereza ameweza kuwapa nafasi wareno wenzake wafuatao: Rui Patricio, ruben neves, Jao Moutinho, Nelson Semedo, Miranda, Vitinha, Podence, Pedro Neto na Fabrizio Silva. Kwa kifupi Santo ameigeuza Wolves kuwa ni ureno ndogo.

Aidha mfano mwingine Mwaka 1997 Barcelona ilianza kusajili wachezaji wengi wa kiholanzi baada ya kocha mholanzi Louis van Gaal kubeba majukumu ya kufundisha timu hiyo toka jimbo la catalunya.msimu uliotangulia alifanya vizuri na kikosi cha Ajax na hii ikampelekea kupata kibarua cha kunoa Barcelona Wachezaji hao ilikuwa ni pamoja na Michael Reiziger, Winston bogarde,ruud hesp. Mwaka uliofuata alisajili waholanzi wa 5 ambao akawapeleka katika kikosi hicho ikiwemo Philip Cocu, Boudewijn zenden, frank de boer, Ronald de boer, Patrick kluivert 

Tanzania Sports
Mkwasa, mmoja wa kocha mzawa mwenye mafanikio

Arsene Wenger toka akabidhiwe Arsenal mpaka alipoachia ngazi ameweza kuwaingiza katika kilabu cha Arsenal wafaransa Zaidi ya 30 na kuwatengezea fursa ya kujulikana na kufaidika na fursa hizo baadhi ya wachezaji hao ni kama wafuatao: Nicolas Anelka, emannuel petit, Robert Pires, yaya sanogo, Thierry henry, Patrick viera,Nguilaume Norbert,Yassin Faortune, David Grondin, Guillaume Warmuz,Gilles Sunu,Armand Traore,Remi Garde,Mikael Silvestre,Sebastien squillacci,Mathieu Debuchy,Jeremie Aladiere,Gilles Grimandi, Pascal Cygan, Jeff Rene Adelaide,lassana Diarra,William Gallas,Francis Coquelin,Mathieu Flamini,Abou Diaby,Samir Nasri, Gael Clichy, Olivier Giroud,Sylvain Wiltord, Bacary Sagna na Laurent Koscielny

Mifano iko mingi sana lakini kwa leo tutosheke na hayo. Kama taifa tulitakiwa tuwe tumewatengenezea fursa akina Mkwasa, Kibaden, Ammy Ninje, na wengineo wengi wafundishe timu zilizo nje ya mipaka ya nchi yetu. Wangekuwa wana mchango mkubwa sana katika kutengeneza njia kwa wachezaji wa kitanzania kupata fursa za kucheza katika nchi hizo. Chama cha makocha kitafyte wadau wakisapoti kianzishe kozi zenye dira ya kuandaa makocha wa kwenda kufundisha nje ya nchi nili wachezaji wetu wauzike.

Report

Written by Kahema Fimbo

Mwandishi wa habari wa kujitegemea mwenye uzoefu wa kuandika kuhusu habari za michezo anayeishi Dar es salaam Tanzania. Ana uzoefu wa miaka 2 wa kufanya kuandika na kasha kuchapisha Makala zake katika mitandao kadhaa nchini Tanzania. Ni mpenzi na pia ni mdau wa michezo. Amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi kwenye vyama vya michezo nchini Tanzania ikiwemo katibu mkuu taifa chama cha mchezo wa kabaddi Tanzania (Tanzania kabaddi sport association), mwenyekiti kamati ya habari chama cha shule za michezo Tanzania (Tanzania sport centres and academies association- TASCA) na pia makamu mwenyekiti wa chama cha soka wilaya ya mkuranga( Mkuranga district football association- MDFA).
Nje ya michezo ni mwanajamii na amewahi kujitolea na pia kuwa kiongozi katika taasisi mbalimbali nchini Tanzania za vijana kam vile YOA, TYVA, YUNA, na kadhalika.

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
DITRAM NCHIMBI

UKISHANGAA YA DITRAM NCHIMBI UTAYAONA YA FREDDY ADDU

Cristiano Ronaldo

Ronaldo kurudi Real Madrid?