in , ,

TUTAWASHAMBULIA YANGA-FADLU DAVIS

Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids

Leo kulikuwa na mkutano wa waandishi wa habari kuelekea mchezo wa Kariakoo Derby kati ya Simba SC na Young Africans ambapo makocha wa timu zote mbili walizungumza na waandishi wa habari kuelekea mechi hiyo. Tanzania Sports ilikuwepo kwenye mkutano huo na kocha wa kwanza alikuwa Fadlu Davis wa Simba alianza kubainisha kuhusiana na maandilizi yao .

Ambapo alisema maandalizi ya mechi yanaendelea vizuri. Wachezaji ambao walikuwa kwenye timu za Taifa wamerudi. Wachezaji kama Kibu Denis,  nahodha wetu Mohamed Hussein,  Mousa Camara wapo kambini na leo tutafanya maandalizi ya mwisho kuelekea mechi ya kesho.

Fadlu Davis alibainisha kuwa Yanga ni timu ambayo imekaa muda mrefu pamoja kwa miaka mitatu, imeshinda ubingwa kwa misimu mitatu mfululizo kitu ambacho wanakiheshimu sana kutoka kwa Yanga.

Pamoja na ubora huo wa Yanga, Fadlu Davis amedai kuwa wametazama Yanga na kuona ubora wao na udhaifu wao na wamejianda na mbinu pamoja na mpango wa kupambana nao. Fadlu Davis amedai kuwa wao ni timu kubwa kwa hiyo kwenye mechi ya kesho wataenda kumiliki mpira.

Alipoulizwa kuhusu baadhi ya wachezaji kwenda kwenye timu zao za taifa kama imeathiri maandalizi ya mchezo huo, Fadlu Davis alidai kuwa wachezaji kwenda kwenye majukumu yao ya timu ya Taifa ni sehemu ya mchezo kwa hiyo haiwezi kuathiri maandalizi yake.

Fadlu Davis alibainisha kuwa kama timu ilikuwa na maandalizi mazuri kabla ya msimu yani “pre-season” ni rahisi kwa kocha kuandaa mpango na mbinu nzuri kuelekea mechi husika, ni rahisi kwa kocha kuandaa namna watakavyoshambulia na  watakavyokaba.

Alipoulizwa kuhusu mbinu ya Yanga kukabia juu , Fadlu Davis alisema kuwa katika mechi ya ngao ya jamii aliwafanya Yanga wasikabie juu na hii ni kutokana na mbinu ambazo wao kama Simba SC walikuwa nazo kwenye mchezo huo.

Fadlu Davis aliongeza kuwa inawezekana Yanga hawakupata nafasi ya kuwaona Simba SC kabla ya mechi hiyo zaidi kwenye mechi ya Simba Day. Kwa sasa Yanga wamepata nafasi ya kuwaangalia kwenye mechi nyingi na watakuja na mbinu zao.

Fadlu Davis alibaniisha kuwa pamoja na Yanga kuja na mbinu zao, iwe wataanzia kukabia juu , watazuia au kushambulia ila wao kama Simba SC hawaendi kukaa nyuma ya mpira na kuzuia kwa sababu wao kama Simba SC hiyo siyo aina yao ya mchezo.

Alipoulizwa kama kupoteza kwao mechi tatu mfululizo dhidi ya Yanga kuna waathiri kisaikolojia, Fadlu Davis alidai kuwa historia kwenye mpira huwa haichezi, kinachocheza ni dakika 90 za siku husika. Fadlu Davis amedai kuwa asilimia kubwa ya wachezaji wa msimu huu hawakuwepo kwenye vipigo hivo vitatu kwa hiyo akili zao hazijaathiriwa.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Vita kuu tano Yanga na Simba leo

Tanzania Sports

KUNA WACHEZAJI WANA MAJERAHA-GAMONDI