in , ,

TUNA DUNIA YA RONALDO NA DUNIA YA MESSI

Ureno na Argentina ndizo nchi ambazo kwa sasa zinaonekana zinamiliki
wafalme wa soka duniani.

Wafalme ambao wamefanikiwa kujenga nguzo imara katika falme zao.

Nguzo ambazo zinaonekana ngumu kwa kizazi kinachokuja kuzivunja,
inawezekana mikono yao hawa watu wawili ilikuwa dhabiti kwenye ujenzi
wa nguzo hizi.

Ujenzi ambao umefanyika kwenye mashindano mengi ambayo miguu yao ilikanyaga.

Miguu yao ilifanikiwa kufanya maajabu kwenye michuano ya klabu bingwa
barani ulaya ndiyo maana Cristiano Ronaldo amefanikiwa kuwa mfungaji
bora wa wakati wote katika michuano hii akiwa na magoli 119

Lionel Messi hakuingiwa na wivu ndani ya moyo wake alichokifanya ni
kuwekeza nguvu kwenye ligi kuu ya Hispania , La Liga na kuwa mfungaji
bora wa wakati wote wa La Liga akiwa na magoli 374 huku Cristiano
Ronaldi akiwa na magoli 303

Hii yote inaonesha hawa watu wapo katika dunia zao za peke yao, dunia
ambazo unatakiwa ufurahie kuziishi kwa sababu hakuna kizuri unachoweza
kukosa kati ya hizi dunia mbili.

Dunia ambazo zimeundwa kwa maumbo tofauti tena na watu wenye ujuzi
tofauti. Kuna watu wawili wamehusika kuunda dunia hizi mbili.

Msanii ni mtu wa kwanza aliyetumia muda wake mwingi kuunda dunia yake
ambayo aliona inafaa kutoka na mafikirio yake.

Aliweka vitu vingi kwenye dunia yake, naksi nyingi zilihusika ili
kupendezesha dunia hii, nakshi ambazo zilimwezesha kumpata mtu mwenye
uwezo mkubwa wa kukokota mpira , kupiga vyenga na sanaa zingine
nyingi, mtu huyu ni Lionel Messi.

Mtu ambaye anatofautiana kubwa ambaye ni Cristiano Ronaldo. Mhandisi
ndiye mtu aliyetumia muda wake kumuumba mtu huyu.

Alitumia nguvu na akili nyingi kuhakikisha anapata mtu ambaye ana
uwezo wa kufanya kazi kwa bidii bila kuchoka tena kwa kiwango kikubwa
kama mashine, akafanikiwa kupata mtu ambaye anauwezo mkubwa wa kufunga
magoli kwa wingi.

Sanaa aliiweka ndani ya mwili wa huyu mtu, lakini sanaa yake ilikuwa
ya muda mfupi kiasi kwamba kadri muda ulivyokuwa unazidi kwenda ndivyo
hivo sanaa ilikuwa inapungua miguuni mwake lakini magoli yakawa
yanaongezeka katika miguu yake, ndipo hapo tukampata Cristiano
Ronaldo.

Binadamu kwenye hat tricks 50 mpaka sasa hivi, hat tricks zinazonesha
kuwa yeye ni muhimu zaidi kwenye kila timu aliyocheza katika maisha
yake kama alivyo Lionel Messi.

Umuhimu wao ni mkubwa sana katika kuamua matokeo kutokana na uwezo wao
binafsi, hakuna kigumu kinachoshindikana kipindi Lionel Messi na
Cristiano Ronaldo wanapokuwa uwanjani.

Unatakiwa uwe na imani kuwa lolote linaweza kutokea kwa sababu yupo
Criastiano Ronaldo na Lionel Messi, watu ambao ni timu waliopo ndani
ya timu.

Kama ilivyo kwa Barcelona ilivyo na timu mbili yani Barcelona yenyewe
na Lionel Messi, ndivyo hivo ilivyo kwa Real Madrid wanatimu mbili
pia ambazo ni Cristiano Ronaldo na Real Madrid.

Hii ni mihimili mikubwa sana katika mpira na timu zao, washindi mara
tano kila mmoja wa Ballon D’or.

Hutakiwi kujitesa kuchagua kuishi dunia moja pekee na kuichukia dunia
nyingine, kama utaamua kuwa dunia ya Lionel Messi unatakiwa ufurahie
kuona ustawi wa dunia ya Cristiano Ronaldo.

Kuwepo kwako katika dunia ya Cristiano Ronaldo kusifanye ukuze chuki
kwenye dunia ya Lionel Messi.

Kuwekeza chuki katika ya dunia ambayo wewe hauishi hakukusaidii
chochote , unachotakiwa kufurahia kumuona anachokifanya Lionel Messi
huku mapenzi yako yakibaki kwa Cristiano Ronaldo.

Mapenzi yako yasikutie upovu na kuacha kuona kizuri anachokifanya
mpinzani wako, hawa ni wachezaji bora kwa sasa na wamedumisha kiwango
chao kwa miaka 10 mfululizo bila kushuka

Wameshinda tunzo nyingi binafsi, wakashinda makombe mengi huku
wakivunja na kuweka rekodi mpya ambazo unatakiwa ujivunie kuzishuhudia
zikiwekwa na miamba hii miwili.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

MAN CITY v UNITED: DHAMIRA YA KUWEKA REKODI DHIDI YA HITAJI LA KULINDA HESHIMA

Tanzania Sports

YANGA WAMETUPA TULICHOKUWA TUNAKITAKA