in

Tulikosea mechi ya Zambia

Taifa Stars

Kwanza tunatakiwa kuwapa pongezi kubwa timu ya Taifa ya Tanzania kuanzia wachezaji wote mpaka benchi la ufundi. Kwa kiasi kikubwa wamejituma kwenye michuano hii na walionesha nia kubwa ya wao kuingia robo fainali.

Mpaka dakika ya 80 harufu ya robo fainali ilikuwa karibu na pua zetu. Kitu pekee ambacho kilitugharimu kwenye mechi ya jana dhidi ya Guinea ni sisi kuruhusu kushambuliwa sana.

Ile presha ya kushambuliwa tulishindwa kuikabili. Akili kwetu kulikuwa na mambo mawili yaliyokuwa yanazunguka kwenye zile dakika kumi za mwisho za mchezo ule.

Kitu cha kwanza kilikuwa  ile hali ya sisi kuiona robo fainali ya michuano ya CHAN. Vijana wetu walikuwa hawaamini kama wako karibu kufika kwenye hatua ya robo fainali .

Kitu cha pili kilichokuwa kinazunguka akili kwetu ni yale mashambulizi ambayo yalikuwa yanashambuliwa na Guinea baada ya sisi kuongoza kwa 2-1.

Hatukuwa na uwezo wa kuizuia ile presha ya kushambuliwa kwenye mchezo huo. Hata ule uwezo wa kumiliki mpira ndani ya dakika sekunde 6. Kila tulipokuwa tunamiliki mpira tulipokonywa na Guinea.

Kuna wakati eneo letu la ulinzi lilikuwa linabakiza uwazi mkubwa. Uwazi ambao uliwafanya washambuliaji wa Guinea kuwa huru zaidi wakati wakiwa na mpira katika eneo letu.

Uhuru ambao uliwapa nafasi ya wao kutengeneza goli ambalo  halikuwa gumu kwao kwa sababu mpigaji wa krosi alikuwa peke yake na aliyepiga kichwa cha goli alikuwa peke yake hii inatoa tafasri kuwa eneo la nyuma lilikuwa wazi sana.

Alikosekana mtu wa kuwatuliza wachezaji wenzake kwa kuwaambia muda huu tunaongoza tunatakiwa kuupoza mpira. Tunatakiwa kushusha presha kati yetu na kuanza namna pekee ya kulinda uongozi wetu.

Pamoja na kwamba jana timu yetu ya Taifa ilijitahidi kwa kiasi kikubwa, kosa pekee ambalo walilifanya ni kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Zambia. Mechi ambayo walitakiwa kupata angalau alama moja.

Kuanza vibaya kwenye michuano kama hii hutoa nafasi kwa timu kucheza kwa presha kubwa. Presha ambayo hupunguza umakini na kusababisha makosa ambayo huigharimu timu.

Jana baada ya kuongoza presha ilikuwa kubwa kwetu. Umakini ukapungua kwa kiasi kikubwa na tukawa tunafanya makosa mengi hasa kwenye eneo letu la nyuma.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
The Cranes

Eti Uingereza imeleta gundu Afrika

Bernard Morrison

Tatizo Morrison anashindana na Yanga