*Mata kwenda Barcelona?
*Sagna akana kusaini Man City
*Welbeck hatihati kubaki Man U
*Rio Ferdinand afikiria kuchukwa ‘OFA’ ya QPR
*Sidwell, Colback na Zaha watakiwa Newcastle

Wakati kiungo wa Hispania Juan Mata hajamaliza miezi sita tangu ajiunge na Manchester United kutoka Chelsea, inasemakana ana mpango wa kuondoka.

Hata kama Louis van Gaal anajiandaa kurekebisha kikosi na kumweka kwenye wachezaji wanne tu wenye uhakika wa kubaki, kuna mengine yanajitokeza.

Inaelezwa kwamba Barcelona wamepanga kumwaga pauni milioni 40 kwa mchezaji ambaye Kocha Jose Mourinho alimwona si chochote.
Baada ya Mreno huyo kumwacha benchi Chelsea, alipoingia Manchester United alipewa kipaumbele, lakini hakuiva vyema na mfumo wa timu hiyo.

Leo hii Luis Enrique, kocha mpya wa Barcelona amesema atamwaga mapesa hayo ili kumpa.

Mata (26) alisajiliwa kwa pauni milioni 38, kwa hiyo akiuzwa United watapata faida ya pauni milioni mbili. Hata hivyo, Mata angeweza kuingia vyema kwenye mfumo wa Van Gaal.

BACARY SAGNA AKANA KWENDA MAN CITY

Bacary Sagna
Bacary Sagna

Beki wa kulia wa Arsenal, Bacary Sagna amesema anashangaa watu wanaodai kwamba amejisajili na Manchester City.

Akiwa kwenye kambi ya Timu ya Taifa ya Ufaransa, Sagna amesema ni kweli inawezekana kwa asilimia 90 akaondoka Arsenal lakini hajafikia uamuzi wa mwisho.

Sagna (31) amesema hajakubaliana wala kusaini mkataba na klabu yoyote ile na kwamba vyombo vya habari ya England vimekuwa vikimfukuzia kujiunga na Man City wakati hajapata kutia mguu huko.

“Hadi leo mimi ni mchezaji wa Arsenal. Ningependa tumakamaliza mambo haya kabla ya Kombe la Dunia…nimekuwa najiuliza swali hili kwa muda mrefu.

“Arsenal ni klabu ya aina yake iliyonipa fursa ya kukua kwa kila hali, ni kama klabu ya familia na najihisi vyema kuwa hapa hata kama inawezekana kwenda kukabiliana na changamoto mpya,” akasema Mfaransa huyo mwenye asili ya Senegal.

Sagna amemaliza mkataba wake Arsenal, na alikuwa akitaka kuongezwa miaka mitatu lakini Arsenal walitaka kumpa mwaka mmoja, ikidaiwa kwamba Man Cit wamekubali kumpa miaka mitatu na nyongeza ya mshahara.

WELLBECK AFIKIRIA KUONDOKA MAN U
20130810-182624.jpg

Mshambuliaji wa Manchester United, Danny Welbeck amesema kwamba hana uhakika wa hatima yake.

Welbeck anasema kwamba inamtatiza anapochezeshwa katika nafasi ambazo si zake, kisha akaongeza kwamba anajihisi furaha zaidi akiwa na kikosi cha England kuliko Man United.

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya kocha wa zamani wa Man U, David Moyes kudai kwamba mchezaji huyo hakuwa akijituma vya kutosha kiasi cha kumlazmisha afanye mazoezi ya ziada.

Hata hivyo, Welbeck amekanusha na kusema alishangazwa na kauli ya kocha huyo, kwa sababu yeye tangu mwanzo alikuwa akiongeza mazoezi juu ya wachezaji w

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Cameroon wazuri 

Spurs wamtaka Kocha Pochettino